Tuesday, December 9, 2014

TRA KUCHAMBUA RIPOTI YA KITUO CHA UTAFITI CHA KODI CHA KIMATAIFA (ICTD)

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade, kushoto akiwa na afisa mtendaji mkuu wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo, Prof Mick Moore, wakiongoza majadiliano juu ya mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo,mkutano uliofanyika jana jijini Arusha
 Wataalamu wa kimataifa  wa masuala ya kodi  wakiendesha mjadala katika mkutano wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha utafiti wa masuala ya kodi,mkutano uliofanyika jana  jijini Arusha ,Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Uganda (URA), Milly Nalukwago (kushoto), Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade (katikati) na  Mtaalam wa Kodi wa Uingereza, Rhiannon Mc Cluskey.
Kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA RISHED BADE kushoto akiwa na afisa mtendaji mkuu wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo Prof MICK MOORE wakiongoza majadiliano juu ya mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo,mkutano uliofanyika jana jijini Arusha


Mwakilishi  wa Channel Ten Arusha, Jamila Omar (katikati) , Mwakilishi wa kituo cha Star TV Arusha, Ramadhani Mvungi ,Iddy Uwesu wa Azam tv Arusha wakifanya mahojiano maalumu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA)  Rished Bade jijini Arusha wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo.

 ***********

Mamlaka ya mapato nchini TRA imeanza kuchambua ripoti ya utafiti uliofanywa na kituo cha kimataifa cha utafiti wa masuala ya kodi na maendeleo inayobainisha changamoto mbalimbali za ulipaji kodi katika
maendeo mbalimbali nchini.

Zoezi la uchambuzi wa ripoti hizo linatajwa kuwa na shabaha ya kuangalia mapungufu yaliyopo na kuboresha mifumo ya sheria na ulipaji kodi kwa hiari.

Sehemu ya Taarifa ya utafiti uliofanwa katika kipindi cha mwaka uliopita na kituo cha kimataifa cha kodi na  maendeleo katika mikoa mbalimbali nchini, inabainisha mazingira tofauti ya ulipaji wa kodi ambapo baaadhi ya maeneo yameonekana kuwa katika changamoto kubwa za ukwepaji kodi.

Kamishana wa TRA Rished Bade kizungumza Jijini Arusha wakati wa Mkutano wa kimataifa baina yao na kundi la wataalamu, wanaofanya utafiti kuhusu masuala ya kodi duniani amesema pamoja na mapitio ya ripoti za utafiti wa taasisi hiyo,fursa hiyo inatoa mwanya kwa wataalamu wa ndani kujifunza mbinu za kushughulikia changamoto za walipa kodi wanaofanya biashara za kimataifa.


Awali Afisa Mtendaji Mkuu wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo Profesa Mick Moore ameeleza kusudio la tafiti zao katika nchi mbalimbali za Afrika kuwa unalenga kuimarisha mifumo ya kodi hususani katika sekta za maliasili zikiwemo Madini,Gas na Mafuta.

Katika hatua nyingine Mamlaka ya mapato nchini TRA imeibuka kinara kwa kuwa na hesabu bora miongoni mwa taasisi za serikali kwa mwaka 2013-2014 zinazotolewa na bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini NBAA ambapo kamishna wa mamlaka hiyo akizungumza Jijini hapa katika hafla ya kukabidhiwa ushindi huo amesema hatua hiyo inazidi kuwajengea imani walipa kodi juu ya utendaji wa chombo hicho.

Raha tele tabu ya nini?: zinaonyesha ongezeko la idadi ya walipa kodi chini,idadi iliyopo sasa inatajwa kuwa ndogo kulinganisha na mataifa mengine kutokana na mfumo wa kibiashara usio rasmi unaopelekea kupunguza idadi ya walipa kodi wanaofikia milioni moja nukta nane hivi sasa.

No comments: