Mfuko
wa Maendeleo ya jamii-TASAF kwa ushirikiano na Wizara ya Fedha
umempongeza na kumuaga rasmi Afisa aliyestaafu kutoka Benki ya Dunia
ofisi ya Tanzania ambaye alikuwa akisimamia shughuli za TASAF Bi. Ida
Manjolo.
Bi.
Manjolo ambaye amefanya kazi hapa nchini kwa miaka kumi amepongezwa kwa
kushiriki kikamilifu katika kuchochea kasi ya utekelezaji wa shughuli
za TASAF za kupambana na umaskini nchini .
Akizungumza
katika hafla ya kumuaga na kumpongeza Afisa aliyestaafu kutoka Benki ya
Dunia ofisi ya Tanzania ambaye alikuwa akisimamia shughuli
za TASAF (Task team Leader-TTL) Bi. Manjolo, Mkurugenzi Mtendaji wa
TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga alibainisha kuwa Afisa huyo alikuwa
akitumia falsafa yenye maneno ya "hakuna kulala hadi kieleweke" katika
kuwapa moyo watendaji na wadau wa mfuko huo katika kuwahudumia walengwa
wa Mpango wa kunusuru Kaya Maskini unaosimamiwa na TASAF.
"Wote
tunafahamu kuwa katika kipindi ambacho tumekuwa naye, TASAF sasa
imepanda chati sana na siyo ndani ya nchi tu, lakini pia hata nje ya
nchi huko kwingineko Duniani, na maendeleo ya mpango wa kunusuru Kaya
Maskini umekuwa ukiongelewa kwamba ni mpango unaofanya vizuri, lakini
haya yote ni kwa sababu ya ushiriki wake mzuri ambao ulikuwepo na
amehusika kwa kiasi kikubwa kuuandaa na kuufikisha mahala hapa pazuri
tulipo" alifafanua Bw. Mwamanga.
Naye
Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha Dakta Servacius Likwelile amemtaja Bi
Manjolo kama kiongozi hodari ambaye wakati wote amekuwa akitekeleza
majukumu yake kwa ukamilifu na kuhakikisha kuwa mafanikio yanapatikana.
"Tumekuwa
katika safari ndefu lakini yenye mafanikio makubwa kutokana na umakini
wa mmoja wa madereva wetu ambaye ni Bi. Manjolo , tulianza naye akiwa ni
msaidizi wa TTL hadi akawa TTL na katika kipindi chake chote cha miaka
kumi ameiwezesha TASAF kufikia mahala hapa kwa sababu ya uwazi , wepesi
na ukarimu wake wa kutaka kuona kwamba tunafanikiwa". Alibainisha Dr.
Likwelile.
Dr.
Likwelile ambaye pia amepata kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF kabla ya
kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha hakusita kutoa shukrani
zake za dhati kwa mafanikio yaliyopatikana kutokana na ushiriki wa Bi.
Manjolo.
"Tunamshukuru
Aida kwa uadilifu, uaminifu, ukaribu, udugu na kupenda kutimiza wajibu
na akaongeza kuwa siyo rahisi kutekeleza mpango kama huu na ukaleta
maana kwa jamii kama hakuna uongozi mzuri na mshauri mzuri". alisisitiza
Dr. Likwelile.
Afisa aliyestaafu wa
Benki ya Dunia aliyekuwa akisimamia shughuli za TASAF Bi. Ida Manjolo
akifurahia tuzo aliyopewa na TASAF kama ishara ya mafanikio makubwa
kufuatia ushirikiano alioutoa kwa TASAF katika kutekeleza mipango ya
maendeleo.
Menejimenti
ya TASAF ikiwa katika picha ya pamoja na Afisa aliyestaafu wa Benki ya
Dunia aliyekuwa akisimamia shughuli za TASAF Bi. Ida Manjolo (wa tatu
toka kulia walioketi).
Baadhi
ya wafanyakazi wa TASAF wakiwa katika picha ya pamoja na
Afisa aliyestaafu wa Benki ya Dunia aliyekuwa akisimamia shughuli za
TASAF Bi. Ida Manjolo (wa tatu toka kulia walioketi) wakati wa hafla ya
kumuaga Bi. Manjolo.
Afisa aliyestaafu wa
Benki ya Dunia aliyekuwa akisimamia shughuli za TASAF Bi. Ida Manjolo
(wa tatu toka kulia walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha Dokta Servacius Likwelile, Kamishna wa Fedha
za nje Wizara ya Fedha Bw. Said Magonya (wa pili kushoto) na Mkurugenzi
Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga (wa kwanza kushoto). Wengine ni
walioketi toka kulia ni Afisa mpya wa Benki ya Dunia anayesimamia
shughuli za TASAF Bw. Mohamed Muuderis na Naibu Katibu Mkuu ofisi ya
Rais Ikulu Bi. Suzan Mlawi pamoja na baadhi ya wanafamilia ya Bi Manjolo
(waliyosimama).
Mkurugenzi
Mtendaji wa TASAF, Bw.Ladislaus Mwamanga akitoa neno katika hafla ya
kumuaga Afisa aliyestaafu wa Benki ya Dunia aliyekuwa akisimamia
shughuli za TASAF Bi. Ida Manjolo (hayupo pichani) kwenye hoteli ya
Southern Sun.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha Dakta Servacius Likwelile (aliyesimama) akitoa
hotuba fupi ya kumuaga Afisa aliyestaafu wa Benki ya Dunia aliyekuwa
akisimamia shughuli za TASAF Bi. Ida Manjolo (aliyeketi kulia).
Afisa aliyestaafu wa Benki ya Dunia aliyekuwa akisimamia shughuli za TASAF, Bi. Ida Manjolo (kushoto) akiwa na Naibu
Katibu Mkuu ofisi ya Rais Ikulu Bi. Suzan Mlawi wakifuatilia kwa makini
hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dakta Servacius Likwelile
(hayupo pichani) katika hafla iliyoandaliwa na TASAF kumuaga Bi.
Manjolo.
Madereva
wa Magari ya TASAF waliohudhuria hafla ya kumuaga Afisa aliyestaafu wa
Benki ya Dunia aliyekuwa akisimamia shughuli za TASAF Bi. Ida Manjolo
wakifuatalia moja ya tukio (halipo pichani) katika hafla hiyo
No comments:
Post a Comment