|
Wanafunzi ambao ndio wamehitimu shule ya ABEL MEMORIAL NURSERY AND PRIMARY SCHOOL leo shule ambayo ipo bunju jijini Dar es salaam hapa wakikata keki pamoja na mwalimu wao ishara ya kufurahia mafanikio waliyoyapata pamoja na mafanikio ya shule hiyo tanghu kuanmzishwa kwake |
|
Wahitimu wakiwa katika pozi za kusubiri sherehe ya kuwaaga rasmi kutoka elimu ya awali kuingia elimu ya msingi |
|
Mgeni rasmi wa mahafali hayo mama NEEMA KIBANGA ambaye ni afisa elimu wa kata ya bunju akikabidhi vyeti kwa wahitimu shuleni hapo |
|
Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja na walimu wao baada ya kukabidhiwa vyeti vyao |
|
Na Exaud Mtei
Shule ya wanafunzi wa awali ya ABEL MEMORIAL NURSERY AND PRIMARY SCHOOL leo imefanya mahafali ya wanafunzi wa awali wanaovuka kuingia elimu ya msingi huku ikiwa na mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake shule hiyo mnamo mwaka 2012.
Shule hiyo ambayo inapatikana BUNJU jijini Dare s salaam ambayo ilianza mwaka 2012 ikiwa na jumla ya watoto tisa tu na mwalimu mmoja ambapo mwaka 2013 idadi iliongezeka na kufikia watoto 13 na hatimaye mwaka huu wa 2014 shule hiyo ina watoto 31 pamoja na walimu wawili jambo ambalo limetajwa kuwa ni mafanikio makubwa kwa shule ya watoto iliyoanzishwa na watanzania wazalendo kwa ajili ya kuinua elimu ya watoto wa Tanzania.
Akizungumza katika mahafali ya shule hiyo leo meneja wa shule hiyo Bwana STANSLAUS ABED MWALONGO amesema kuwa lengo lilikuwa ni kuanzisha shule ya secondary lakini baada ya kutafakari jkwa kina akaona ni vyema kuanzisha shule ya awali na msingi ili kutoa msingi bora wa elimu kwa watoto wetu.
Bwana STANSLAUS ambaye baba yake ndiye aliyekuja na wazo za kuanzisha shule hiyo na kufanya shule hiyo kuitwa jina lake amesema kuwa moja ya mafanikio makubwa ya shule hiyo ni kuongezeka kwa watoto wanaoenda kujiunga na shule hiyo ambapo mpaka sasa watoto sita wamehitimu shuleni hapo na sasa wanaendelea na masomo ya shule ya msingi katika shule mbalimbali zenye ushindani nchini Tanzania.
Katika hali ya kutia moyo meneja wa shule hiyo amesema kuwa shule yake imekamilisha taratibu zote za usajili na kuwa mwakani 2015 shule hiyo itaanza kutoa elimu ya msingi kwa mara ya kwanza ambapo amesema kuwa wanatarajia kuanza kutoa elimu ya darasa la kwanza kwa masomo yote huku akibainisha kuwa lengo la shule hiyo ni kutoa elimu bora inayoendana na maadili ya kitanzania ili kuwasaidia watoto waweze kuwa kizazi bora hapo baadae.
|
Kwa upande wake mgeni rasmi wa mahafali hayo ambaye ni afisa elimu kata ya BUNJU mama NEEMA KIBANGA amesema kuwa ni mafanikio ya kupongezwa kwa wamiliki wa shule hiyo kwani wamefanya jambo ambalo linatakiwa kuigwa na kila mtanzania ambaye anapenda maendeleo ya watoto bila kujali rangi,dini,wala kabila analotoka huku akikumbuka kuwa watoto bni wetu sote.
|
|
Mmoja wa wamiliki wa shule hiyo ambaye ni mke wa meneja wa shule hiyo BI ROSE MWALONGO akizungumzas na watoto wa shule hiyo mapema kabla ya kuanza shughuli rasmi ya mahafali ya shule hiyo |
|
Maadili ya kidini ni moja ya nguzo kuu za shule hiyo bila kuchagua imani ya mtu mtumishi wa mungu akitoa neni la mungu kwa wazazi na watoto waliohudhuria sherehe hiyo iliyyofanyika shuleni hapo BUNJU jijini Dar es salaam |
|
Picha mbili zikiwaonyesha wazazi waliofika kujumuikana watoto wao katika kuhitimu elimu yao ya awali |
Baadhi ya wazazi waliobahatika kuzungumza na mtandao huu wamesema kuwa wameridhika kabisa na utoaji wa elimu shuleni hapo kwani unazingatia vigezo na maadili yote hivyo hawana hofu juu ya watoto wao huku wakiwahimiza wazazi walio na watoto wadogo kuwaleta ABEL MEMORIAL NURSERY AND PRIMARY SCHOOL kwa ajili ya mafunzo bora kwa watoto wao.
Katika mahafali ya leo wanafunzi takribani 6 wamehitimu shuleni hapo katika masomo yao ya awali na wataanza elimu ya msingi shuleni hapo mwakani
|
Watumishi wa bwana walitumia muda wao kubariki eneo la shule hiyo kwa maji ya baraka ili watoto wanaosoma hapo kuwa na baraka za mungu muda wote |
|
Wamiliki wa shule hiyo bwana STANSLAUS MWALONGO pamoja na mke wake RIOSE MWALONGO wakitoa neno la shukrani kwa watu mbalimbali waliojitokeza kuhudhuria shughuli hiyo |
|
Ulifika muda wa vinywaji na kufurahi ambapo watoto waliburudika |
|
Muonekano wa shule hiyo |
|
Walimu waliofanya mambo makubwa katika shule hiyo hawakuacha kuzawadiwa chochote |
|
Muda ukafika sasa wa mambo yetu yale tukakutana mezani na watoto kuhakikisha matumbo nayo yanahitimu |
No comments:
Post a Comment