Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, James Kajugusi (mwenye suti nyeusi) aliyewamwakilisha Waziri mwenye dhamana wa wizara hiyo, akiongea na Vijana wanaofanyashughuli za kutolea wakati wa maadhimisho ya siku ya kujitolea kimataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
Alisema ingawa kujitolea kunawezesha kupata uzoezi ili vijana waweze kuajiriwa na kuendeleza taaluma,maana ya kujitolea haipo katika kuajiriwa bali katika hali ya kuona maana yake katika kusaidia jamii kujitambua na kujituma na kuwajibika .
“Usaidizi katika jamii ndio muhimu kuliko ajira. Haina maana yoyote kuwa na ajira bila kujua maana yake katika kusaidiajamii,” huku akisisitiza kwamba haina maana yoyote kama umeajiriwa na ukaendekeza umimi huku ukiwa hujali maslahi ya umma hata yanapoharibika.
Alisema Serikali ikiwa inaamini kwamba chachu ya kujitolea ni vijana ametaka watumie njia mbalimbali katika shughuli za kujitolea kwa kuona wenzetu wanafanya nini na kutumia uzoefu wao katika kujenga taifa imara la Tanzania.
Aidha alisema wakati umefika wa vijana kusaidia kurejesha moyo wa kujitolea uliokuwepo kabla ya miaka ya 1970 ambapo shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara ulifanywa na wananchi wenyewe kwa namna ya kujitolea kuanzia miaka ya 1970 moyo wa kujitolea umepungua sana.
Pichani juu na chini ni baadhi ya vijana kutoka taasisi mbalimbali na mashirika yasiyo ya kiserikali waliohudhuria maadhimisho ya siku ya kujitolea kimataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma wakisikiliza kwa umakini hotuba ya Waziri Mukangara iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, James Kajugusi (hayupo pichani).
“Nilikozaliwa wananchi ndio walikuwa wanatengeneza barabara, visima vya maji, wananchi ndio wanapeleka wagonjwa hospitali..’” na kusema kwamba sasa hali imekuwa mbaya kwa kuwa inadaiwa kitu kwanza kabla ya kufanyika kwa kazi.
Akizungumzia kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya kujitolea inayosema; Ushiriki na ushirikishwaji katika kuleta maendeleo katika ngazi zote za kitaifa na za kimataifa, amesema inaangalia ushiriki wa vijana katika maendeleo.
Alisema Tanzania imetengeneza mikakati kadha aya kuwezesha ushiriki wa vijana ikiwa ni pamoja na kuridhia mkataba wa vijana wa umoja wa Mataifa na kuanzisha baraza la vijana kwa mujibu wa katiba.
Naye Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akizungumza kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodrigues, amesema umoja wa mataifa unajisikia faraja kuadhimisha siku hiyo ikiwakumbuka watu mbalimbali waliofanya utu kwa kujitolea katika shughuli mbalimbali za ubinadamu.
Akiwasilisha neno la katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki moon alisema siku ya kimataifa ya kujitolea ni muhimu kutokana na mahitaji halisi yaliyopo sasa duniani katika ulinzi wa maisha ya binadamu na utamaduni wake.
Alisema maelfu ya wananchi waliokumbwa na madhila mbalimbali wameweza kutulizwa na wafanyakazi wa kujitolea ambao waliondoa umimi na ubinafsi na kusaidia walio katika matatizo.
Alisema Umoja wa mataifa ukiwa unathamini amani , haki sawa na maendeleo ya jamii na kwa kuwa na siku ya kujitolea ya kimataifa kunaonesha umuhimu wa juhudi za umoja huo za kusambaza malengo hayo kufanikisha maendeleo na ushiriki wa vijana katika maendeleo yao , kitaifa na kimataifa.
Katika hotuba yake ya kumkaribisha mgeni rasmi, Vuzo alisema kwamba shughuli za kujitolea za Umoja wa Mataifa zilianza nchini mwaka 1974 katika misingi ile ile ya kufunza jamii kujitolea kwa manufaa yao na maendeleo ya taifa.
Vuzo alisema programu ya kujitolea ya Umoja wa mataifa ambayo hapa nchini inaitwa UNV inasaidia kufanikisha mikakati mbalimbali inayoendeshwa na serikali ili kuboresha hali ya kujitolea nchini kwa manufaa ya taifa.
Programu hiyo ikiwa imezingwa na mikakati ya kitaifa ya kukabiliana na umaskini kama MKUKUTA na MKUZA na misaada kwa mipango ya maendeleo ya Umoja wa mataifa UN kuanzia mwaka 2011 – 2016, UNV kwa sasa inajishughulisha na masuala ya wakimbizi, utawala bora, Ukimwi vijana na maendeleo sekta binafsi.
Alisema UNV ikiwa imetimiza miaka 35 imekuwa ikiwasaidia Watanzania katika sekta hizo ambapo wamekuwa wakifanya kazi kwa moyo mmoja kuhakikisha maisha ya watanzania yanabadilika.
Aidha ametoa wito kwa vijana kujiunga na shughuli za kujitolea kutokana na umuhimu wake kwao na kwa taifa.
Mkufunzi wa ujasiriamali kutoka shirika lisilola kiserikali la Restless Development, Lawrence Ambokile, akitoa ushuhuda wake kwa vijana wenzake ambapo alisema anajisikia faraja na moyo wake una furaha kwa kufanya kazi za kujitolea kwenye jamii ambapo imemsaidia kukuza uelewa wake na pia ni baraka kwa Mungu.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana Dkt. Steven Kisui akifafanua jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya kujitolea kimataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma yaliyokutanisha vijana kutoka taasisi na mashirika mbalimbali yasiyoyakiserikali wanaofanyashughuli za kujitolea kwenye jamii.
Vijana wanaofanya shughuli za kujitolea kutoka ndanu na nje ya nchi wakiwa wamekusanyika pamoja kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kujitolea yaliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. James Kajugusi (kulia) akiwa ameongozana na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana Dkt. Steven Kisui, Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo aliyemwakilisha Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakielekea kutembelea mabanda kwenye maadhimisho ya siku ya kujitolea kimataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
Mfanyakazi wa Shirika la KOICA, Catherine Tarimo akieleza shughuli mbalimbali wanazofanya ikiwemo kujitolea kwa Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, James Kajugusi (mwenye suti nyeusi) aliyewamwakilisha Waziri mwenye dhamana ya wizara hiyo. Kushoto kwake ni Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo na kulia kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana Dkt. Steven Kisui.
Mwakilishi wa kampuni ya 4Life, Nelson Benges (mwenye tai ya damu ya mzee) akielezea virutubisho mbalimbali vinavyotumika kuimarisha kinga ya mwili wa mwanadamu kwa asilimia 437 na kuufanya mwili imara na uweze kupamba na magonjwa kwa Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. James Kajugusi Kulia kwa Bw. Kajugusi ni Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo na kushoto kwake ni Programme Officer wa Shirika la UNV, Bi. Stella Karegyesa.
Mtaalam wa Masoko wa UN Volunteer Kitaifa, Catherine Sinje (wa pili kulia) akieleza shughuli mbalimbali za kujitolea zinazofanywa na shirika lake likiwahusisha vijana zaidi katika kufanya kazi za kujitolea kwenye jamii kwa Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. James Kajugusi wakati wa kutembelea mabanda kwenye maadhimisho ya siku ya kujitolea kimataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. James Kajugusi, akizungumza jambo na wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kujitolea (UNV) alipokuwa akitembelea mabanda kwenye maadhimisho ya siku ya kujitolea kimataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
No comments:
Post a Comment