Mkurugenzi wa Operesheni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Asumpta Malya,
akionyesha tuzo ambayo PPF ilipata kwenye shindano la Afrika
linaloandaliwa na taasisi ya ISSA, kuhusu utoajin bora wa huduma wa
mifuko ya hifadhi ya jamii barani Afrika, hususan kwenye fao la elimu.
Alikuwa akiwaonyesha wahariri wa vyombo vya habari kwenye semina ya
siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo mjini Bagamoyo, mkoa wa Pwani
Jumamlosi Desemba 13, 2014 baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii
kwa utoaji huduma bora kwa wanachama wake.Alikuwa akiwaonyesha
wahariri wa vyombo vya habari kwenye semina ya siku moja ya Wahariri
wa vyombo vya habari iliyofanyika mjini Bagamoyo , mkoa wa Pwani,
Jumamosi Desemba 13, 2014.
Mkurugenzi wa Mifumo ya Computer wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Robert
Mtendamema, akitoa mada kuhusu huduma za Mfuko huo zinavyotolewa
kimtandao.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akitoa
hotuba ya ufunguzi wa semina ya siku moja ya wahariri wa vyombo vya
habari nchini, iliyofanyika Jumamosi Desemba 13, 2014, huko Bagamoyo
mmkoani Pwani.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akizungumza
kwenye semina ya simu moja ya wahariri wa vyombo vya habari
iliyuolenga kutoa elimu zaidi ya huduma zitolewazo na Mfuko huo na
mafanikio ambayo Mfuko imepata katika kipindi cha uhai wake. Semina
hiyo ilifanyika mjini Bagamoyo, Jumamosi Desemba 13, 2014
Mkurugenzi wa fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Martin Mmari,
akionyesha tuzo ya ushindi wa juumla (Overall winner) ya utunzaji
mahesabu inayotolewa na Bodi ya Ukaguzi wa Mahesabu (NBAA), hivi
karibuni. Alikuwa akiwaonyesha wahariri wa vyombo vya habari waliokuwa
wakishiriki semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo mjini
Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumamosi Desemba 13, 2014.
Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Steven Alfred, akitoa mada kwenye semina hiyo.
Sehemu ya Wahariri waliohudhuliwa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumamosi Desemba 13, 2014.
No comments:
Post a Comment