Tuesday, December 23, 2014

NAIBU WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AFANYA ZIARA KATIKA WITUO VYA AFYA MKOA WA KASKAZINI ''A'' UNGUJA

Mkuu wa kituo cha Afya cha Mkokotoni Mcha Haji Makame akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo (alievaa miwani) alipofanya ziara ya kutembelea vituo vya afya vya Wilaya Kaskazini A. Wa kwanza (kushoto) mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Andymicheel Ghirmany akifuatiwa na mwakilishi wa UNICEF Zanzibar Bibi Fransisca.
Mkuu wa kituo cha Afya Mkokotoni akiwaonyesha wawakilishi wa UNICEF Bibi Fransisca na mwenzake wa WHO Ghirmany jiko la kuchoma takataka za Hospitali hiyo.
Wawakilishi wa UNICEF na WHO wakiangalia takwimu za wagonjwa waliopata matibabu katika Hospitali kuu ya Wilaya kwa kipindi cha miezi 11 kunzia Januari walipofanya ziara na Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
Daktari dhamana wa Hospitali ya Kivunge Khamis Hamad akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo na ujumbe aliofuatana nao walipofanya ziara kuangalia utendaji wa kazi na kujitambulisha.
Mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Andymicheel Ghirmany akizungumza na wafanyakazi wa kituo cha afya Chaani (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Afya Zanzibar katika vituo vya Wilaya Kaskazini A.
Baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha afya cha Chaani wakimsikiliza Mwakilishi mkaazi wa WHO Zanzibar wakati wa ziara ya Naibu Waziri kutembelea vituo hivyo.Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

No comments: