KAMPUNI
ya Simu Tanzania (TTCL) leo imetoa msaada wa vyakula na bidhaa
mbalimbali kwa Hospitali ya Wagonjwa wa Kansa Ocean Road ya jijini Dar
es Salaam ikiwa ni kuwasaidia wagonjwa hao kusherehekea Siku Kuu ya
Chrismas pamoja na Mwaka Mpya.
Misaada
hiyo ni sehemu ya kampuni ya TTCL kuamua kushirikiana na jamii katika
maeneo mbalimbali ikiwa ni ishara ya kurejesha sehemu ya faida yao ya
kampuni kwa jamii hasa iliyo katika wakati mgumu.
Akikabidhi
msaada huo wa unga, mafuta ya kula, sukari, chumvi na maji ya kunywa,
ambayo kwa pamoja vinagharimu shilingi milioni tatu (3), Mkuu wa Huduma
kwa wateja wa kampuni ya TTCL, Laibu Leonard alisema tukio hilo ni
utaratibu wa kampuni yao hasa nyakati za sikukuu ambapo uwafariji wateja
wao waliopo katika mazingira ya uhitaji msaada kwa chochote.
Alisema
Hospitali hiyo ya Wagonjwa wa Kansa, Ocean Road ipo mbioni kufungwa
mkongo wa mawasiliano unaosimamiwa na TTCL ili kuwafanya madaktari
hospitali hiyo kuweza kutoa huduma kwa njia ya mawasiliano ya picha hata
kwa mgonjwa ambaye yupo mikoani.
Alisema
tayari maandalizi ya awali yamefanywa kati ya TTCL na hospitali hiyo
hivyo mwakani huduma ya matibabu kwa njia ya mtandao kwa kutumia mkongo
wa mawasiliano itaanza kutolewa na madaktari.
Akizungumzia
manufaa ya huduma hiyo, Leonard alisema huduma hiyo ya matibabu ya
picha kwa mawasiliano inapunguza gharama za matibabu kwa kiasi kikubwa
kwani daktari aliye nje ya nchi kama India anaweza kumtibu mgonjwa
aliyelazwa hospitali za Tanzania bila kikwazo.
"...Tumeleta
msaada huu kwa kuwa hawa ni miongoni mwa wadau wetu kibiashara, sasa
hivi tunamalizia utaratibu wa wao kutumia mkongo wetu kwa ajili ya
shughuli za matibabu...ambayo kwa kiasi kikubwa yanapunguza gharama
sana, badala ya mgonjwa asafiri kwenda nje ya nchi kufuata huduma
anaweza kutibiwa akiwa hapahapa kwa kutumia matibabu ya picha kutumia
mtandao," alisema.
Akipokea
msaada huo, Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Ocean Road, Marry Haule
alisema wamefarijika na msaada uliotolewa na TTCL kwani msaada
waliouleta ni sehemu ya matibabu kwa wagonjwa wao na kuhaidi kuutumia
kama ilivyo kusudiwa.
Alisema
wagonjwa wa kansa wanahimizwa kula sembe ili iweze kuwasaidia kama
sehemu ya matibabu jambo ambalo TTCL imelifanya, hivyo kuwapongeza na
kuomba kampuni zingine zifuate mfano wa kampuni hiyo kwa kuwakumbuka
wagonjwa.
Huduma
ya matibabu kwa njia ya mtandao (picha) inayowezeshwa na mawasiliano ya
mkongo wa mawasiliano wa taifa, imesha anza kazi katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili, Hospitali ya KCMC, Hospitali ya Tumbi Kibaha, pamoja
na Hospitali za Mwananyamala na Temeke zote za jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment