MMOJA
wa wataalamu wa kuchunguza matatizo ya masikio,Stuart Specer kutoka
Taasisi ya Starkey Hearing Foundation ya nchini Marekani inayoendesha
kliniki ya masikio aakitaniana na mkazi wa Arusha,Ally Abdulrahman
aliyewahi kuishi nchini humo ambaye kwa sasa ana matatizo ya kusikia
kwenye kliniki inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo
PalaceJijini Arusha jana
Wanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Mount Meru na chuo cha Biashara cha Arusha (IAA)
waliokuja kujitolea wakisaidia kutoa huduma mbalimbali kwenye kliniki ya
masikio iliyoratibiwa kwa pamoja kati ya Montage Limited na Starkey
Hearing Foundation inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo Palace
jijini Arusha jana
Wagonjwa
wenyematatizo ya usikivu wakisubiri kupata matibabu kwenye kliniki ya
matibabu na uwekaji vifaa vya kuongeza kiwango cha usikivu iliyoratibiwa
kwa pamoja kati ya Montage Limited na Starkey Hearing Foundation
inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo Palace jana.
Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya MsingiMeru wakisubiri kupatiwa huduma ya
matibabu ya masikio kwenyeKliniki inayoendesha na taasisi kutoka
Marekani ya Starkey Hearing Foundation inayofanyika kwenye viwanja vya
Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha jana.
DAKTARI,
Assay Shibanda(kushoto) na John Yuccas wakimwekea mwanafunzi wa Shule
ya Msingi Elbol,Levina Innocent mashine ya kuongeza kiwango cha usikivu
kwenye Kliniki inayoendeshwa kwa pamojakati ya Montage Limited na
taasisi kutoka Marekani ya Starkey Hearing Foundation ya kuwawekea vifaa
vya kuongeza usikivu inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo
Palace jijini Arusha jana
Mtaalamu
wa matatizo ya usikivu kutoka Taasisi ya Starkey Hearing Foundation ya
nchini Marekani, Derek Johson akimfanyia uchunguzi wa awali wamasikio
mmoja wa watu wenye usikivu hafifu waliokuja kuhudhuria Kliniki
inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha jana
Mratibu
wa Taasisi ya Starkey Hearing Foundation kutoka Marekani, Derek Johnson
akitoa maelezo ya awali kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mount Meru na
chuo cha Biashara cha Arusha, (IAA) waliokuja kujitolea kutoa huduma
mbalimbali ya matibabu na uwekaji vifaa vya kuongeza kiwangocha usikivu
masikioni kwenye Kliniki inayofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya Kibo
Palace jana. Kushoto ni Msimamizi Mkuu wazoezi hilo, Teddy Mapunda.
No comments:
Post a Comment