Kiongozi wa idara ya utalii Arusha Bi.Anita Temba akiongea na washiriki wa shindano la Model of Tourism Tanzania mara baada ya kufanya ziara yao katika makao makuu ya TANAPA jijini Arusha ambapo waliweza kufahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika hilo
Meneja Mahusiano wa TANAPA Pascal Shelutete akizungumza na washiriki wa shindano la Model of Tourism Tanzania mara baada ya kufanya ziara yao katika makao makuu ya TANAPA jijini Arusha
Kiongozi wa idara ya utalii Arusha Bi.Anita Temba akiteta jambo na mratibu wa shindano hilo Samdia Charles
Mkurugenzi mkuu hifadhi za Taifa ,Tanzania Allan Kijazi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa shindano la Model of Tourism Tanzania mara baada ya kufanya ziara yao katika makao makuu ya TANAPA jijini Arusha
Mkurugenzi wa utalii na masoko Ibrahim Mussa akiwa anawasikiliza washiriki wa shindano la Model of Tourism Tanzania mara baada ya kufanya ziara yao katika makao makuu ya TANAPA jijini Arusha (hawapo pichani)ambapo aliwataka washiriki hao kutumia nafasi hiyo kutangaza utalii wa ndani
Mkurugenzi mkuu hifadhi za Taifa ,Tanzania Allan Kijazi akipata utambulisho kutoka kwa washiriki wa shindano hilo
Kiongozi wa idara ya utalii Arusha Bi.Anita Temba akiwa anatoa maelekezo kwa washiriki wa shindano la Model of Tourism Tanzania
Na Pamela Mollel wa jamiiblog
Washiriki wa shindano la Model of Tourism Tanzania wametakiwa kutumia fursa hiyo katika kutangaza utalii wa ndani hali itakayopelekea idadi kubwa ya watanzania kutembelea hifadhi za Taifa
Rai hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa utalii na masoko Ibrahim Mussa ,jana wakati washiriki wa shindano hilo walipopata fursa ya kutembelea makao makuu ya TANAPA jijini Arusha
Bw. Mussa aliwataka washiriki hao kutumia fursa hiyo katika kutangaza utalii wa ndani hali itakayo pelekea idadi ya watanzania kujitokeza kwa wingi kutembelea hifadhi za Taifa
Alisema kuwa ipo haja kwa watanzania kuona utalii ni sehemu ya starehe ambayo unaweza kujifunza hata ukiwa na familia yako tofauti na starehe zingine
Naye Maratibu wa shindano hilo Samdia Charles alisema lengo la kuanzishwa kwa shindano hilo ni kuhamasisha utalii wa ndani na kutangaza vivutio vya nchi yetu kimataifa kupitia maonyesho ya mavazai kama vile new York fashion week,Paris fashion week na Victoria’s secret fashion show
Aidha alisema kuwa katika shindano hilo washiriki wametoka katika mikoa mbalimbali ya Dar es saam, Arusha,Iringa,Mbeya,Manyara, Singida,Kilimanjaro,Tanga, Tabora,Dodoma na Mwanza
Shindano hilo lilianzishwa mwaka 2013 ambapo mwaka huu kuna jumla ya washiriki 19 kati yao 16 ni mabalozi wa hifadhi za taifa na shindano hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 22 novemba 2014katika ukumbi wa triple A jijini Arusha
No comments:
Post a Comment