Mkurugenzi
Msaidizi Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma kutoka Wizara ya Afya na
Ustawi ya Jamii, Said Makora (kulia), akielezea jinsi Wizara hiyo
inavyopambana kutoa elimu ya ugonjwa wa Ebola kwa wananchi wakati wa
kongamano lililoandaliwa na UNESCO, WHO, UNICEF, Wizara ya Afya na
Ustawi ya Jamii, uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania (OUT), Novemba 11,2014 jijini Dar es Salaam mkutano huo
uliowakutanisha wamiliki wa Redio za kijamii kuwaelimsha Radio za
Kijamii za Mikoani ni namna gani wanavyoweza kushirikiana na Wizara ya
Afya na Ustawi ya jamii ili kutoa taarifa sahihi kwa wananchi kuhusu
ugonjwa wa Ebola, Ebola ni nini namna ya kujinga na dalili
zake.(kushoto), Kushoto ni Mwenyekiti wa COMNETA ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Redio FADECO, Sekiku Joseph.(PICHA NA PHILEMON SOLOMON).
SERIKALI
, Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) na vyombo vya habari nchini hapa
vimekubaliana kufanyakazi kwa pamoja kwa ajili ya kuelimisha watanzania
kuhusu ugonjwa hatari wa Ebola. Katika juhudi za kuwekana sawa
kuhusu uelimishaji wa umma kuhusu ugonjwa huo, kumefanyika kongamano la
mafunzo kwa siku mbili, Chuo Kikuu huria jijini Dar es salaam.Kongamano
hilo lilifanyika Novemba 10 na 11.
Kongamano hilo liliwashirikisha viongozi wa radio za wananchi zaidi ya 28 kutoka Visiwani na Tanzania Bara. Katika
kongmano hilo kulitengenezwa mikakati mbalimbali yenye kuleta uelewa
kwa umma na kuwafanya kuchukua hatua za tahadhari na kuzuia ugonjwa huo
usiingie nchini.
Mshauri
wa Redio Jamii na Mkufunzi kutoka Shirika la Kimataifa la Elimu Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Mwalimu akiendesha majadiliano kuhusu
mikakati endelevu itakayowezesha kuihusisha jamii katika upatikanaji wa
taarifa sahihi juu ya ugonjwa wa Ebola wakati wa kongamano hilo
lililowakutanisha wamiliki wa radio za kijamii lengo ni kuwaelimsha
Radio za Kijamii za Mikoani ili kutoa taarifa zilizo sahihi kwa wananchi
kuhusu ugonjwa wa Ebola.
Kwa
mujibu wa mmoja wa watu wanaounda kikundi kazi chenye lengo la
kukabiliana na ugonjwa huo mafunzo hayo yaliandaliwa na Shirika la
sayansi, elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) . Aidha
mafunzo hayo yaliwezeshwa kwa pamoja kati ya wizara ya afya na Umoja wa
Afya duniani (WHO), na Shirika la kusaidia watoto la UNICEF.
Mafunzo
hayo yaliyokuwa na washiriki walikuwa ni pamoja na wanachama wa
wanamtandao wa vyombo vya habari Tanzania (COMNETA), yaligusa zaidi
redio ambapo 25 kati yake zinaohudumiwa na Umoja wa Mataifa. Wakati
lengo kuu ni kuwafanya watanzania waujue ugonjwa huo na kuanza kuchukua
hatua za tahadhari, mafunzo yalilenga kushawishi vyombo hivyo kutenga
muda mchache kwa ajili ya elimu hiyo ili kuzuia mlipuko wake nchini.
Mkurugenzi
wa Redio Kwizera ilioko Ngara-Kagera, Damas Missanga akichangia mada
yake wakati wa kongamano la kuwaelimsha wamiliki wa Redio za Kijamii za
Mikoani ili kutoa taarifa zilizo sahihi kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa
Ebola.
Katika
mafunzo hayo washiriki walidadavua ebola nini na jamii inaweza
kujijenga namna gani ili kukabiliana na janga hilo la kidunia. Matumizi
ya elimu ya mawasiliano yalitiliwa mkazo hasa kwa kubaini kwamba elimu
hiyo ndiyo itakayoweza kutengeneza mkakati wa kuwabadili wengine na
hivyo kuzuia kuingia kwake na kusambaa.
Washiriki
na wawezeshaji walikubali kufanyakazi ya pamoja na Tume ya taifa
inayoratibu mapambano dhidi ya Ebola katika kuelimisha umma kwa kuweka
wazi taarifa za ugonjwa huo na namna ya kukabiliana nao. Iliamuriwa
kwamba radio hizo za jamii zitatumika kuanzisha midahalo yenye lengo la
kuwasilisha taarifa mbalimbali kutoka kwa kikosi kazi cha kukabiliana
na ugonjwa huo.
Meneja wa Redio jamii FADECO ya wilayani Karagwe, Adelina Lweramula akichangia mada wakati wa kongamani hilo.
Radio
hizo ambazo zina changamoto ya aina yake kuanzia zile za wafugaji wa
Serengeti ambako mara nyingi nyama ndizo zinazoliwa hadi kwenye jamii
mbalimbali na hasa makorido yenye wageni wengi kama Zanzibar. Aidha
kongamano hilo limeboresha ushirikiano kati ya vyombo vya habari na
serikali za mitaa ili kuendelea kutoa taarifa sahihi na zinazozingatia
utamaduni wa eneo husika huku kukiwa na wito wa mabadiliko.
Katika
kukabiliana na janga la Ebola na virusi vya Marburg, mafunzo hayo
yaliangalia pia umuhimu wa kushirikiana katika kuhakikisha kwamba
ugonjwa huo unashughulikiwa na kila mtu na kuondokana na hofu
zinazofanya watu wayakimbie maeneo husika.Kumeelezwa ni lazima
juhudi za makusudi zichukuliwe ili jamii kuelimishwa na wao kushiriki
katika kukabilina na tishio la Ebola hata kwa vijiji ambavyo vipo
pembezoni.
Kama
alivyosema Dk. Said, Mwenyekiti mwezeshaji kutoka wizara ya afya na
ustawi wa jamii alisema anafurahishwa ushirika na wadau umepelekwa hadi
katika radio za jamii ambazo ni muhimu sana katika kuimarisha juhudi za
kufikia wananchi waliopo pembezoni.
Wamiliki
wa Redio za Kijamii wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na UNESCO, WHO,
UNICEF, Wizara ya Afya na Ustawi ya Jamii ili kuwaelimsha wa wamiliki
hao kutoa taarifa zilizo sahihi kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Ebola.
No comments:
Post a Comment