Mkuu wa Wilaya ya Igunga,Mh.Elibarik Kingu akizungumza
mbele ya washiriki wa kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari
kuhusiana na mpango mzima wa wananchi wake kutumia bima ya Afya,na pia
alifafanua kuhusiana na mikakati mbalimbali anayotumia kuwahamasisha
wananchi wake katika suala zima la kuhakikisha kila mtu anakua Bima ya
Afya,lakini pia alieleza kuwa Wilaya yake ya Igunga ina vijiji 98,vijiji
78 vimejengwa zahati,lakini mpaka sasa zahanati 31 hazijasajiliwa,hivyo
ameiomba Serikali kupitia wizara ya Afya kuhalakisha suala la usajili
wa zahanati hizo katika kuwasaidia wananchi.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,Bwa.Hamisi Mdee akifafanua jambo katika
kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa Habari,lililofanyika leo
Dodoma hotel,ikiwa ni siku ya pili ya hitimisho la Kongamano hilo,Kauli
mbiu ya kongamano hilo ni ''Tanzania
na Huduma bora za matibabu inawezekana''.Kongamano hilo lilizinduliwa
jana na Waziri wa Afya Dkt Seif Rashid,ambapo pia Kabla ya uzinduzi wa
kongamano hilo Wanahabari walishiriki kutembelea miradi mbalimbali ya
afya,ikiwemo hopsitali ya Mkoa wa Dodoma pamoja na Kituo cha kisasa cha
uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya binadamu kilichopo ndani ya chuo
kikuu cha Dodoma (UDOM),ambacho imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 36
zilizotolewa na NHIF,kituo hicho kinatarajiwa kuanza kazi rasmi mapema
mwakani.
Mmoja wa Maofisa kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA),Bi.Gaudensia Semwanza akifafanua jambo katika kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari,ndani ya Dodoma hotel leo,ikiwa ni siku ya pili.
Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Athman Rehani akizungumza mbele
ya washiriki wa kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari ndani
ya Dodoma hotel leo,ikiwa ni siku ya pili,kuhusiana na mchango wa
Wanahabari katika kuboresha sekta ya Afya na umuhimu wa Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya kwa watoa Huduma
Pichani kulia ni Mkuu wa wilaya ya Igunga,Mh.Elibarik Kingu,Mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahya Nawanda pamoja na Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Athman Rehani kwa pamoja wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika kongamano
la tisa la NHIF na Waandishi wa habari ndani ya Dodoma hotel leo,ikiwa
ni siku ya pili,kuhusiana na mchango wa Wanahabari katika kuboresha
sekta ya Afya na umuhimu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa watoa
Huduma
Pichani shoto ni Mmoja wa Maofisa kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA),Bi.Gaudensia Semwanza na Mdau wakifuatilia mada mbalimbali ndani ya kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari,ndani ya Dodoma hotel leo,ikiwa ni siku ya pili.
Pichani
kulia ni Mkuu wa wilaya ya Igunga,Mh.Elibarik Kingu pamoja na Mkuu wa
wilaya ya Iramba,Yahya Nawanda wakijadiliana jambo.
Washiriki katika
kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa Habari,lililofanyika leo
Dodoma hotel ikiwa ni siku ya pili ya kilele chake huku likiwa limebeba
kauli mbiu ''Tanzania
na Huduma bora za matibabu inawezekana''.Kongamano hilo lilizinduliwa
jana na Waziri wa Afya Dkt Seif Rashid,ambapo pia Kabla ya uzinduzi wa
kongamano hilo Wanahabari walishiriki kutembelea miradi mbalimbali ya
afya,ikiwemo hopsitali ya Mkoa wa Dodoma pamoja na Kituo cha kisasa cha
uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya binadamu kilichopo ndani ya chuo
kikuu cha Dodoma (UDOM),ambacho imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 36
zilizotolewa na NHIF,kituo hicho kinatarajiwa kuanza kazi rasmi mapema
mwakani.
Baadhi ya Wanahabari na Wahariri waandamizi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari,ndani ya Dodoma hotel leo,ikiwa ni siku ya pili.
Mmoja wa Wanahabari Wakongwe,kotoka gazeti la Habari Leo Beda Msimbe akiuliza swali kwenye Kongamano hilo.
Baadhi ya Wanahabari na Wahariri waandamizi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari,ndani ya Dodoma hotel leo,ikiwa ni siku ya pili.
Baadhi ya Maofisa kutoka NHIF wakijadiliana jambo wakati wa Kongamano .
Mkurugenzi
Mtendaji wa shirikisho la Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania
(UTPC),Bwa.Abubakar Karsan akichangia jambo katika kongamano la tisa la NHIF na Waandishi wa habari,ndani ya Dodoma hotel leo,ikiwa ni siku ya pili.
No comments:
Post a Comment