|
Wanaharakati kutoka shirika la Kwieco la
mkoani Kilimanjaro wakiwa katika maandalizi ya maadhimisho ya siku 16
za kupingaukatili wa kijinsia. |
|
Maandamano ya kuadhimisha siku 16 za kupinga
ukatili wa kijinsia yakipita katika mitaa mbalimbali ya mji wa
Moshi. |
|
Mkurugenzui wa shirika la KWIECO ,Elizabeth
Minde (mwenye miwani myeusi) akiwa katika maandamano
hayo. |
|
Brass Band ya Chuo cha Polisi ikiongoza
maandamano ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
kwa kanda ya kaskazini yaliyofanyika mkoani
Kilimanjaro. |
|
Maandamano yakiingia katika viwanja vya
manyema ambako maandamano hayo yalikomea na kufuatia na burudani
mbalimbali sanjari na hotuba toka kwa mgeni rasmi. |
|
Afisa habari wa shirika la KWIECO ,Veronica
Ollomi akitoa maelezo juu ya utendaji kazi wa shirika kwa mgeni rasmi
Mtumwa Mwako alipotembelea bana la shirika hilo . |
|
Afisa habari wa KWIECO ,Veronica Ollomi
akitoa zawadi kwa mgeni rasmi Mtumwa Mwako. |
|
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku 16 za
kupinga ukatili,mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Mtumwa Mwako
akipitia hotuba yake ,shoto kwake ni mwenyekiti wa kamati ya
maadhimisho ya siku hiyo , |
|
Mkuu wa dawati la jinsia mkoa wa Kilimanjaro
,Mrakibu wa jeshi la Polisi ,Grace Lyimo pia alikuwa miongoni mwa
washiriki wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa
kijinsia. |
|
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya
maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ,Elizabeth Mushi
akisoma risala mbele ya mgeni rasmi katika maadhimisho hayo
yaliyofanyika katika viwanja vya manyema mjini Moshi. |
|
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku 16 za
kupinga ukatili wa kijinsia kwa kanda ya kaskazini ,Dk Mtumwa Mwako
akitoa hotuba yake katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika
viwanja vya Manyema. |
|
Mratibu wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga
ukatili kanda ya kaskazini ,Hilary Tesha (katikatika)akijadiliana
jambo na baadhi ya washiriki katika maadhimisho hayo katika viwanja
vya Manyema mjini Moshi. |
|
Wanaharakati kutoka mashirika mbalimbali
yanayopambana na vitendo vya unyanyasaji pamoja na ukatili wa kijinsia
katika mikoa ya Kilimanjaro ,Arusha na Manyara wakifuatilia hotuba ya
mgeni rasmi(hayupo pichani. |
NA Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii
kanda ya kaskazini.
No comments:
Post a Comment