Monday, October 27, 2014

WAZIRI NYALANDU ARUHUSU WANANCHI WANOENDA KWENYE MATIBABU KITUO CHA AFRICA AMINI KUPITA BILA KULIPA HIFADHINI

Waziri Nyalandu akitoa maamuzi ya serikali kuhusiana na hadha hiyo ambapo ameruhusu wananchi wanaoelekea katika kituo hicho kwa ajili ya kupata matibabu wapite bila ya kutozwa chochote.
Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Arusha(ANAPA) Betrita Loibook akizungumza juu ya tozo hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar akizungumza juu ya Adha wanayoapata wakazi wa Vijiji vya jirani na hifadhi ya Arusha ya kutakiwa kutoa tozo kwa ajili ya kupita katika barabaara ya hifadhi hiyo wakati wakielekea katika kituo hicho cha Afya kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Waziri Nyalandu akitia saini katika kitabu cha Wageni.
Mkurugenzi wa Kituo cha Africa Amini Cornellia Walner akitoa maelezo mbele ya Waziri Nyalandu,Mbunge Nassar na Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa(ANAPA) Betrita Loibook.
Waziri Nyalandu akiteta jambo na mmoja wa wafanyakazi katika kituo hicho aliyefahamika kwa jina la Jamilah Mongi.
Waziri Nyalandu akimsalimia mmoja wa wagonjwa waliokuwa wakipata matibabu katika chumba cha matibabu cha kituo hicho cha Afya cha Africa Amini.

Waziri Nyalandu akisamia wagonjwa.
Waziri Nyalandu akizungumza na mmoja ya watu waliofika katika kituo hicho kwa ajili  ya matibabu waliyefahamiana .


Mmoja wa wauguzi katika kituo hicho aliyefahamika kwa jina moja la Nice akitoa maelezo kwa Waziri Nyalandu,wengine ni Mbunge wa Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA) Pascal Shelutete. 
Waziri Nyalandu akisalimiana na wagonjwa waliofika katika kituo hicho kwa ajili ya kupata matibabu,Pembeni yake ni Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akiwasili katika kituo cha Afya cha Africa Amini Alama kilichopo katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha(ANAPA)akiwa ameambatana na Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar.
Waziri Nyalandu akizungumza na mmoja wa wagonjwa aliyekuwa katika kituo hicho ambaye alihitaji kiasi cha shilingi 5000 kwa ajili ya matibabu pesa ambazo alisaidiwa na Waziri Nyalandu .
Waziri Nyandu pamoja na Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki  Joshua Nassar wakipata maelezo toka kwa mkurugenzi wa kituo cha Afya cha Africa Amini wakati alipotembelea kituo hicho kilichopo katika Hifadhi ya TAIFA YA ARUSHA.
Mkutano ukiendelea katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kaskazini.

No comments: