.Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk. Shukuru Kawambwa(kulia)akikabidhiwa
Usinga unaomtambulisha kama mzee wa jamii ya Kimaasai(Laigwanani) na
Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi
ya Kaskazini Kati mkoani Arusha,Solomon Masangwa wakati wa harambee ya
kuchangia ukarabati wa Miundombinu iliyochakaa ya Shule ya Sekondari ya
Enaboishu,Shule hiyo imeanzishwa miaka 48 iliyopita na KKKT.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk. Shukuru Kawambwa akitoa hotuba yake
wakati wa harambee ya kuchangia ukarabati wa Miundombinu ya Shule ya
Sekondari Enaboishu,kushoto ni Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la
Kirutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini Kati,Solomon Masangwa,Mkuu
wa Shule hiyo,Lesion Ole Sekioni na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo ambaye ni mhitimu wa Shule
hiyo,Elisante Ole Gabriel.
Askofu
wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini
Kati,Solomon Maswangwa akimpongeza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Profesa Elisante Ole Gabriel
aliyebuni mpango wa kuwakutanisha wanafunzi waliosoma Shule hiyo
kuchangia maendeleo ya elimu,yeye akiwa mmoja wao.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk. Shukuru Kawambwa akiwa katika picha
ya pamoja na viongozi mbalimbali na Wafanyakazi wa Shule ya Enaboishu
Baadhi
ya Walimu wa Shule hiyo wakifatilia kwa makini harambee ya kuchangia
maendeleo ya Shule ya Sekondari Enaboishu mkoani Arusha.
Waimbaji wa Empowered Girls Club wakitoa burudani iliyovuta hisia za watu waliohudhuria hafla hiyo.
Waimbaji
wa Empowered Girls Club wakifurahia kitita cha Sh.200,000 walizopewa na
mgeni rasmi,Waziri wa Elimu,Dk Shukuru Kawambwa kwa kutoa burudani
iliyovuta hisia za watu waliohudhuria hafla hiyo.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk. Shukuru Kawambwa akipongenzwa na
wanafunzi wa Shule ya hiyo baada ya kufanikisha harambee .
No comments:
Post a Comment