Wakimbiaji kutoka
makampuni mbalimbali na walemavu wa ngozi (albino) wakichuana katika Mbio za
Rock City Marathon (Kilomita 5) zilizowahusisha walemavu wa ngozi na watu
kutoka makampuni mbalimbali Jijini Mwanza Jana.
washindi wa mbio za
watoto wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania
(RT), Andrew Mtaka, wakifurahi na bahasha zao za zawad.
Mshiriki wa km 21
akimaliza mbio hizo.
mshiriki wa km 21
akiweka alama kwenye vidole alipofika eneo la samaki jijini mwanza.
Meneja Kiongozi wa
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mwanza, Bw. Hamis Faki (wa pili
kushoto) akitoa hotuba wakati wa kuhitimisha Mbio za Rock City Marathon
zilizofanyika jijini Mwanza Jana.
Katibu Mkuu wa Chama cha
Riadha nchini Suleiman Nyambui,akiwapa maelekezo wakimbiaji wa Km 21, kabla ya
mbio kuanza,kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
Meneja Kiongozi wa
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mwanza, Bw. Hamis Faki (wa kwanza
kushoto) na Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Bw. Andrew Mtaka (wa tatu
kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na washindi wa Mbio za Rock City
Marathon 2014 (Kilomita 21) upande wa wanaume, punde baada ya washindi hao
kukabidhiwa zawadi zao.
Mratibu wa Mbio za Rock
City Marathon 2014 kutoka kampuni ya Capital Plus International Limited (CPI),
akizungumza na waandishi wa habari juu ya muitikio mkubwa ulionyeshwa katika
Mbio za mwaka huu zilizofanyika Jijini Mwanza Jana.
Mwanariadha
kutoka Mkoani Manyara Joseph Panga,akimaliza mbio za KM 21 kwenye
Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jana,wakati wa mbio za Rock City
Marathon 2014, akifuatiwa na Sammy Nyokaye kutoka Kenya(kulia).
Wanariadha wakianza kukimbia mbio za km 21 kwenye Uwanja wa
CCM Kirumba jijini Mwanza jana,wakati wa mbio za Rock City
Marathon 2014.
Mbio za Rock City 2014 zatiafora
- Mtanzania ashinda mbio za kilometa 21
Mwandishi Wetu, Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist
Ndikilo ameagiza maofisa utamaduni na michezo kuandaa mikakati jinsi ya
kushiriki kikamilifu mashindano ya Rock City Marathon mwakani.
Akikabidhi zawadi kwa washindi wa
mbio kwenye uwana wa CCM Kirumba kwa
niaba ya Ndikilo jana, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Amina Masenza alisema licha
mbio hizo kufanyika mkoani hapa kwa miaka sita, Mwanza haijafanya vizuri na
kuagiza ofisa utamaduni kuandaa mkakati wa kutelekezwa kwa ajili ya mashindano
mwakani.
Ndikilo alisema Tanzania inaweza
kurejea ramani ya dunia kwenye michezo na kwamba, kinachohitajika ni
maandalizi hasa kuanzia shule za msingi.
Mashindano hayo yaliyoandaliwa na
kampuni ya Capital Plus International (CPI) yamefanikishwa kwa udhamini wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), TSN Group
kupitia kinywaji chake cha Chilly Willy, pamoja na African Barrick Gold, IPTL,
Air Tanzania, New Mwanza Hotel, Nyanza Bottling, Sahara Media Group,
Continental decoders, New Africa Hotel, PPF, Tanapa na Bodi ya Utalii Tanzania
(TTB).
Naye Rais wa RT, Andrew Mtaka aliagiza
waandaji wa mashindano ya riadha nchini kuanza kuwaweka wanariadha kambini kabla
ya mashindano, huku akiwataka walimu kutowachosha wanamichezo hao.
Mtaka alisema uhamasishaji wa mbio
hizo umekuwa mkubwa na kuwataka waandaji wengine nchini kuiga Kampuni ya
Capital Plus, kwani ushiriki wa watoto kwenye mashindano hayo umekuwa mkubwa.
“Waandaaji wote wa mashindano ya
riadha wahakikisahe wanazingatia ushiriki wa watoto na watu wenye ulemavu wa
ngozi (albino), nitaendelea kulea vijana walioonyesha vipaji ili wawekwe kwenye
benki yetu ya wachezaji,” alisema Mtaka.
Alisema tayari wameomba Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ili kuwaisaidia
wachezaji kuweka kambi nje ya nchi kama alivyofanya wakati wa michauano ya
Jumuiya ya Madola.
Katika mashindano hayo, Joseph Panga kutoka
Manyara ameibuka mshindi wa kwanza kwenye mbio za Rock City Marathon
zilizofanyika jijini Mwanza jana baada ya kumaliza kwa muda wa saa 1:02:36, akifuatiwa
na Mkenya Sammy Nyokaye aliyetumia muda wa saa 1:02:39.
Mbio hizo za kilomita 21 zilizofanyika
zilianzia Uwanja wa CCM Kirumba kupitia Barabara ya Uwanja wa Ndege hadi Mzunguko
wa Samakisamaki na kurudi hadi Uwanja wa Ndege Mwanza na kumalizikia Kirumba.
Nafasi ya tatu upande wa wanaume ni
Festus Talam kutoka Kenya aliyetumia muda wa saa 1:03:05, huku upande wa
wanawake Kanda ya Kaskazini ikionekana kutawala mbio hizo, mshindi wa kwanza ni
Mathalia Elisante aliyetumia muda wa saa 1:14:25 akifuatiwa na Mary Naali aliyetumia
saa 1:15:34 na Adelina Audata saa 1:23:01.
Washindi wa kwanza waliibuka na kitita
cha Sh1.5 milioni kila mmoja, washindi wa pili Sh900,000 na washindi watatu
Sh700,000.
Akizungumzia siri ya ushindi wake,
Panga alisema mashindano ya mwaka jana alishika nafasi ya sita na kwamba, hiyo
ilikuwa chachu ya kujituma kufanya zaidi mazoezi na kula vizuri.
“Maandalizi ya mwaka huu ni mazuri ila
washiriki ni wachache na hiyo imetokana na wengi wamekwenda kwenye vilabu yao
kwa ajili ya mashindano, lengo langu ni kuhakikisha nakimbia Olimpiki ya
kimataifa,” alisema.
Hata hivyo, Nyokaye alisema mwaka jana
alishika nafasi ya nne ingawa washiriki walikuwa wengi tofauti na mwaka huu,
huku akishauri Chama cha Ridhaa Tanzania (RT) kujikita zaidi shuleni ambako
wanaweza kupata wanariadha wazuri.
Mahindano hayo yanayoandaliwa na
Kampuni ya Capital Plus kila mwaka yamo kwenye kalenda ya RT, huu ni mwaka sita
tangu kuanzishwa.
Washindi wa kilomita tano wanaume
ambazo ni maalumu kwa walemavu wa ngozi (albino) ni Pascal Charles, Pascal
Emmanuel wote kutoka Wilaya ya Magu, mkoani Mwanza na George Joseph kutoka
Ilemela.
Upande wa wasichana mshindi ni Irene
Joseph, Asterina Abel na Saidati Haji wote kutoka wilayani Ilemela, mkoani
Mwanza.
Mita 100 washindi wasichana ni Kabula
Hamis, Anita Elias na Damari Charles na wanaume ni Erick Charles, Jumanne Roche
na Lugera Machumu. Washindi wa mita 400 upande wa wasichana ni Leticia Richard,
Pili Hamisi na Paschalia Sylveter.
No comments:
Post a Comment