Mkurugenzi
wa Usalama wa Mazingira Majini Bw. Tumpe Mwaijande kutoka Wizara ya Uchukuzi
kwaniaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Shaaban Mwinjaka akiongea na
wajumbe wa Umoja wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na
Kusini mwa Afrika (WOMESA) wakati wa ufunguzi wa mkutano wao wa mwaka unaofanyika
jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
Msaidizi kutoka Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Mambo ya Bahari (IMO)
Pamela Tansey akiwasilisha mada wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Umoja
wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika
(WOMESA) uliaofanyika leo jijini Dar es salaam.
Veronica Maina
akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Umoja wanawake
walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika (WOMESA)
uliaofanyika leo jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja ya
wajumbe wa mkutano wa mwaka wa WOMESA mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo. (Picha na Eleuteri
Mangi –MAELEZO)
Mjumbe wa sekretarieti ya Umoja
wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na Kusini mwa Afrika
(WOMESA) Bi. Veronica Maina akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa
mwaka wa Umoja wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki na
Kusini mwa Afrika (WOMESA) uliaofanyika leo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa
WOMESA kutoka Mauritius Bi. Meenaksi Bhirugnath-Bhookun akitoa mada wakati wa ufunguzi
wa mkutano wa mwaka wa Umoja wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari
Mashariki na Kusini mwa Afrika uliaofanyika
leo jijini Dar es salaam.
Dkt. Faustina
Ncheye kutoka WOMESA Tanzania akimpima afya Bi Tumaini Namoya mjumbe wa mkutano
huo kutoka Kenya.
Na Eleuteri Mangi-
MAELEZO
Wanawake wameaswa kutumia
fursa iliyopo katika sekta ya bahari kwa kupata elimu na mafunzo ya sekta hiyo ambayo
ni msingi wao katika kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia ukuaji sayansi na
teknolojia inayoongezeka kwa kasi duniani.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi
wa Usalama wa Mazingira Majini Tumpe Mwaijande kutoka Wizara ya Uchukuzi
kwaniaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Shaaban Mwinjaka wakati wa ufunguzi
wa mkutano wa mwaka wa Umoja wanawake walio katika Sekta ya masuala ya Bahari Mashariki
na Kusini mwa Afrika (WOMESA) unaofanyika leo jijini Dar es salaam.
Akisoma hotuba kwa
niqaba ya Katibu Mkuu huyo, Mwaijande amewataka wajumbe wa mkutano huo (WOMESA),
wawe tayari kujadili masuala yanayojenga na kukuza ushiriki wa wanawake katika
sekta ya bahari katika nchi zao.
Katika mkutano huo wa
siku nne ambao umeanza leo oktoba 28 na unatarajiwa kumalizika Oktoba 31 mwaka
huu, mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo mpango mkakati wa WOMESA kuhusu
ushiriki wa wanawake katika masuala ya sekta ya bahari katika nchi wanachama.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Msaidizi kutoka Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Mambo ya Bahari (IMO) Pamela
Tansey amesema kuwa WOMESA imekuwa msatari wa mbele katika kumwendeleza
mwanamke kwenye sekta ya bahari.
Pamela amesisitiza kuwa
wajumbe wa mkutano huo ni vema waelewe na kusimamia dira ya WOMESA ambayo lengo
lake ni kuwawezesha wanawake kupata ajira katika sekta ya masuala ya bahari kwa
njia ya kupta elimu na mafunzo katika kuendeleza taaluma yao juu ya masuala ya
bahari.
Mkutano huo wa WOMESA
unajumuisha wajumbe 52 kutoka nchi mbalimbali wanachama zikiwamo Ethiopia,
Namibia, Komoro, Visiwa vya Shelisheli, Zambia, Mauritius na Kenya.
Nchi nyingine ni
Angola, Sudani, Lesotho, Uganda, Somalia, Eritrea, Botswana, Rwanda, Madagaska,
Afrika Kusini, Msumbiji, Burundi, Malawi, Djibout, Zimbabwe na wenyeji Tanzania.
Mkatano huo wa siku nne
unafanyika nchini chini ya ufadhili wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Taasisi
ya Masuala ya Bahari Tanzania (DMI), shirika la mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF)
kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa
linaloshughulikia Mambo ya Bahari (IMO) na Shirika la Kimataifa la Maendeleo
(UNDP).
No comments:
Post a Comment