Katibu na Mshauri Mkuu wa Makapuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP), Bw. Joseph Makandege, (mwenye suti nyeusi kushoto) akipongezwa na Mdhamini na Mlezi wa kwaya ya Patano la Usharika wa Likamba kanisa la KKKT la Arumeru, mkoani Arusha, Bw. Philip Makini baada ya kukabidhi mfano wa hundi ya Shilingi milioni 10 kati ya Silingi milioni 20 (Tsh 20m/-) iliyotolewa na kampuni ya IPTL/PAP, kusaidia kwaya ya Patano la Usharika wa Likamba kuweza kurekodi albam ya nyimbo za injili. Wakishuhudia ni Mwinjilisti wa Kanisa hilo, Bi Martha Musa Kivuyo (mwenye nguo nyeupe), na Meneja Uhusiano wa Jamii wa IPTL/PAP Bw. Sylvester Joseph pamoja na wanakwaya.
Katibu na Mshauri Mkuu wa Makapuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP), Bw. Joseph Makandege, (kulia) akizindua albam mpya ya nyimbo za injili ya kwaya ya Patano la Usharika wa Likamba Kanaisa la KKKT la Wilaya ya Arumeru, Arusha. Kati kati ni Meneja Uhusiano wa Jamii wa Makampuni ya IPTL/PAP Bw. Sylvester Joseph akifuatwa na Bi.Hellen Zelothe.
Katibu na Mshauri Mkuu wa Makapuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP), Bw. Joseph Makandege, (kulia) akionyesha albam mpya ya nyimbo za injili ya kwaya ya Patano la Usharika wa Likamba Kanaisa la KKKT la Wilaya ya Arumeru, Arusha mara tu baada ya kuuzindua. Wakishuhudia kutoka kulia ni Mfadhili na mlezi wa kwaya hiyo Bw. Philip Makini, ambaye pia ni Afisa Mwandamizi wa jumuia ya Afrika Mashariki, akifuatwa na Meneja Uhusiano wa Jamii wa Makampuni ya IPTL/PAP Bw. Sylvester Joseph akifuatwa na Bi.Hellen Zelothe.
Moja wa waumini katika Kanisa la KKKT Usharika wa Likamba iliyopo Wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha, Bw. Thedayo Zelothe (kulia) akitoa mchango wake wa fedha pamoja na jogoo wawili wakato wa harambee ya kuchangia kwaya ya Patano la kanisa hilo mwishoni mwa wiki kwa lengo la kurekodi albam ya nyimbo za injili. Aliyebeba majogoo ni Mgeni rasmi katika harambee hiyo ambaye ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Makapuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP), Bw. Joseph Makandege. Wakishuhudia ni Mfadhili na mlezi wa kwaya hiyo Bw. Philip Makini (wa pili kulia), Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CCK) Bw. Renatus Mwabih (wa pili kushoto) akifuatwa Bi.Hellen Zelothe.
Katibu na
Mshauri Mkuu wa Makapuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited
(IPTL) na Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP), Bw. Joseph Makandege,
(wa pili kulia) akimpongeza mototo aliyeonyesha umahiri wake wa kucheza na
kuimba nyimbo za injili akiwa ni mwanakwaya ya Edeni ya Kanisa la Morovian la
Mjini Arusha. Mgeni rasmi alitoa Shilingi milioni moja (Tsh 1m/-) kama mchango
wa ada yake ya shule.
Wananchi wametakiwa kuwa makini na
kauli za wanasiasa kwani sio kila kitu wanachosema ni cha kweli bali baadhi yao
hupotosha jamii kwa maslahi yao binafsi.
Akizungumza wakati wa harambee ya
kuchangia kwaya ya Patano la Kanisa la KKKT Usharika wa Likamba Wilayani
Arumeru-Magharibi, Mkoani Arusha mwishoni mwa wiki, Wakili ambaye pia ni Katibu
na Mshauri Mkuu wa Sheria wa makapuni ya kufua umeme ya Independent Power
Tanzania Limited (IPTL) na Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP), Bw. Joseph
Makandege, (ambaye alimwakilisha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPTL/PAP,
Bw. Harbinder Singh Sethi) alionya kuwa kauli za upotoshaji katika maswala mbali
mbali nchini, hususan ya kisheria zinaweza kuleta madhara makubwa sana kwa
taifa.
“Kama mwanasheria, ningependa
kuwashauri wanasiasa wetu kuacha kuingilia mashauri yaliyopo mahakamani au
ambayo yameamuliwa na vyombo halali vya kimahakama kwa kutoa kauli ambazo
zinawapotosha wananchi. Wakiendelea na tabia ya kuhoji uhalali wa maamuzi ya
mahakama, itapelekea hata wananchi kutokuwa na imani na mahakama zetu, jambo
ambalo linaweza kusababisha haki za watu wanyonge kupotea na amani ya nchi yetu
kutoweka,” alisema Bw. Makandege.
Aliongeza kuwa kauli hizo zinachangia
kuiathiri jamii ambayo pengine hawajui ukweli kuhusu jambo linaloongelewa kwa
kuwa wengi wao wanaamini kuwa kila kauli ya mwanasiasa ina ukweli na inapotokea
mwanasiasa anaipotosha jamii madhara yake huwa makubwa sana.
Mwanasheria huyo akitolea mfano tuhuma
zinazo endelea kuhusu kutwaliwa kwa kampuni ya IPTL na PAP pamoja na fedha za
IPTL zilizokuwa katika Akaunti ya Escrow ya Tegeta (IPTL Tegeta Escrow Account)
katika Benki Kuu ya Tanzania, alisema licha ya wanasiasa kutambua ukweli kwamba akaunti hiyo na fedha
zote zilizokuwemo hazikuwa za umma, bado wanaendelea kuiongopea jamii kwamba
fedha hizo zilikuwa mali ya umma, bila hata kuhofia madhara yanayoweza
kusababishwa na kauli zao, jambo ambalo alisema kuwa linakinzana hata na
maandiko matakatifu.
Aliongeza kuwa kauli kama hizo sio tu
zinahatarisha amani ya taifa letu kwani ni za kichochezi kwa sababu zinaweza
kuwafarakanisha wananchi na serikali yao, bali pia zinaweza kuathiri uwekezaji katika
nchi yetu kwa kuwakatisha tamaa wawekezaji jambo ambalo linaweza kuhatarisha
uchumi wa taifa letu.
Akifafanua, Bw. Makandege alisema
ukweli ni kwamba fedha zote zilizokuwa katika akaunti hiyo ya Escrow hazikuwa za
umma bali zilikuwa fedha halali za IPTL, ambazo zilihifadhiwa katika akaunti
hiyo ya Escrow kufuatia mgogoro baina ya wabia wa IPTL, Mechmar Corporation
(Malaysia) Berhad (“Mechmar”) na VIP Engineering & Marketing Limited
(“VIP”). Baada ya mgogoro kuisha kufuatia uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu ya
Tanzania (Mh. Jaji Utamwa) tarehe 5 Septemba 2013, fedha hizo zililipwa
kihalali kabisa kwa IPTL kutokana na mauzo ya umeme kwa Tanesco.
“Iweje wanasiasa wahoji tu fedha hizo
zilizolipwa kwa IPTL kihalali kulipia umeme ambao IPTL ilizalisha na kuiuzia TANESCO
na kusambazwa kwa wananchi? Kwani IPTL ni mali ya umma? Je, ilitaifishwa
lini?”, alihoji Bw. Makandege.
Kwa upende wake Katibu Mkuu wa Chama
Cha Kijamii (CCK) Renatus Mwabhi, ambae pia alishiriki katika hafla hiyo,
amewataka wananchi kuchambua kwa umakini matamshi ya viongozi kabla ya
kuyaamini kwakuwa siyo viongozi wote wanalitakia kheri taifa hili.
Mbali na hilo, katibu huyo wa CCK
amewataka wananchi na waumini kuliombea taifa kwani kina kila dalili kuwa
matendo yanayoendelea hivi sasa hapa nchini yanaweza kuliingiza taifa katika
machafuko yasiyo ya lazima.
Katika harambee hiyo zaidi ya shilingi
milioni 30 (Tsh 30,000,000/-) zilikusanywa huku kampuni ya IPTL na PAP
wakishirikiana na kampuni ya mawakili ya Bulwarks Associate Advocates
wakichanga zaidi ya shilingi milioni ishirini (Tsh 20,000,000/-) ambazo
zitachangia katika maendeleo ya kanisa na kuwezesha kwaya hiyo kurekodi
albam yake mpya yenye ujumbe wa neno la Mungu ili kuwawezesha kutimiza azma yao
ya kueneza injili kwa watu wote.
Kwa upande wake, mlezi wa kwaya hiyo ya
Patano na kwaya ya Edeni ya Kanisa la Morovian la Mjini Arusha, Bw. Philip
Makini ambaye pia ni Afisa Mwandamizi wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), aliwapongeza
IPTL/PAP na Bulwarks Associate Advocates kwa msaada waliotoa ambao alisema
utawawezesha wanakwaya na Usharika kwa ujumla kufanikisha malengo yao.
Naye Mwinjilisti wa Kanisa la KKKT
Usharika wa Likamba, Bi. Martha Musa Kivuyo, kwa niaba ya wanakwaya na
wanausharika wote, aliwashukuru Makampuni hayo kwa mchango wao uliowawezesha
kuvuka malengo ya harambee hiyo iliyotazamia kukusanya Shilingi milioni 20 (Tsh
20m/-)
No comments:
Post a Comment