Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiwasili kwenye Ubalozi wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Washington, DC nchini Marekani alikokaribishwa
chakula cha jioni wakiwemo viongozi mbalimbali wa Wizara ya Fedha na
Benki Kuu ya Tanzania. Mhe. Ombeni Sefue ndiye aliyewezesha ununuzi wa
jengo hilo la Ubalozi wakati alipokua Balozi wa Tanzania nchini Marekani
mwaka 2007
Balozi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata
Mulamula akimpokea Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue siku ya
Jumatano Oct 8, 2014 siku Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
ulipomkaribisha chakula cha jioni wakiwemo viongozi mbalimbali wa Wizara
ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea mawili matatu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dr. Servacius Likwelile.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akisalimiana na Naibu Gavana Dr. Natu Mwamba.
Mkuu
wa Utawala na Fedha Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini
Marekani Mama Lily Munanka akiongea machche na baadae kumkaribisha
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula.
Mhe.
Liberata Mulamula akimkaribisha Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni
Sefue na kumshukuru kwa kuwezesha upatikanaji wa jengo hilo la Ubalozi.
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akimshukuru Balozi Liberata Mulamula
na kuelezea ununuzi wa Jengo hilo ulivyofanyika yakiwemo majengo mengine
ya Ubalozi Canada na New York huku akisema ni jambo jema kwa Serikali
kuangalia uwezekano wa kununua majengo ya Ubalozi na makazi ya maafisa
wake badala ya kukodisha kwani kufanya hivyo kunapunguza gharama kwa
kiasi kikubwa sana yeye aliliona hilo ndio maana alipendekeza na hatimae
kuwezesha ununuzi wa majengo hayo.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akijichukuli chakula.
Wageni wakiendelea kupata chakula cha jioni. Picha na Vijimambo Blog.
No comments:
Post a Comment