Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa
akizungumza na wananchi jana wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya
Vijana yanayofanyika katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora.
Katibu Mkuu wa Wizaraya Habari.Vijana, Utamaduni
na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akisalimia wananchi jana wakati wa uzinduzi wa
maadhimisho ya wiki ya Vijana yanayofanyika katika viwanja vya Ali Hassan
Mwinyi Mkoani Tabora.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Kudra Mwinyimvua
akisalimia wananchi jana wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Vijana
yanayofanyika katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa
akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya wiki ya Vijana jana
mkoani Tabora.Kushoto ni ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga,Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Bibi. Kudra
Mwinyimvua na wa mwisho kulia ni Mwakilishi wa UNFPA Tausi Hassan.
Baadhi ya Vikundi vya Burudani
wakitumbuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Vijana jana
mkoani Tabora.
Baadhi ya wadau wa wiki ya Vijana
wakifuatilia Burudani kutoka kwa Kikundi cha JKT hakipo pichani jana mkoani
Tabora wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Vijana ambayo kitaifa
inafanyika mkoani hapa.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa
akielezea jambo alipotembelea banda la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo jana mkoa Tabora mara baada ya kuzindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya
Vijana.Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bibi. Sihaba Nkinga na mwisho kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya
Filamu Bibi. Joyce Fissoo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa
akisikiliza maelezo kuhusu mfumo wa kuwajengea uwezo Vijana kujitengenezea
makampuni yao na kumiliki Biashara alipotembelea banda la Kampuni ya GODTEC jana
mkoa Tabora mara baada ya kuzindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Vijana.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa
akiweka saini katika kitabu cha wageni katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF) jana mkoa Tabora mara baada ya kuzindua rasmi maadhimisho ya
Wiki ya Vijana.
Baadhi ya wananchi wakipata huduma ya
upimaji wa afya zao katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya jana mkoani
Tabora ambapo maadhimisho ya wiki ya Vijana yanaenedele.
Na
Jonas Kamaleki - MAELEZO
Serikali yaweka Mkakati kupunguza changamoto
ya ajira kwa Vijana
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania imeweka mkakati kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa
vijana kwa kutenga fedha katika halmashauri mbali mbali nchini kwa lengo la
kusaidia miradi ya vijana.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa
Tabora, Bibi Fatma Mwassa wakati wa sherehe za uzinduzi wa Wiki ya Vijana mjini
Tabora leo (jana). Bibi Fatuma amesema kuwa Mkoa wa Tabora umetenga jumla ya
shilingi 1.8 kwa ajili ya kusaidia miradi ya vijana.
“Serikali inatambua changamoto zinazo
wakabili vijana ikiwemo ukosefu wa ajira ata hivyo tumekuwa tukijitahidi
kukabiliana nazo ikiwemo kwa kutenga fedha kwa ajili ya kusaidia vijana ambapo
hapa mkoani kwetu jumla ya shilingi bilioni 1.8 zimetengwa katiak halmashauri
zote.” Alisema Bibi. Fatma. Aidha Bibi Fatma aliongeza kuwa Serikali
ipo tayari kusaidia Vijana katika kuendeleza shughuli zao na kuwataka kuwa
wabunifu na wenye dhamira ya kweli katika kutekeleza miradi ya maendeleo.
Mkuu huyo wa Mkoa amewataka vijana
wasitumiwe tu na watu wasioitakia mema nchi bali wajitambue ili waweze kufanya
shughuli za uzalishaji mali na kuacha tabia ya kukaa vijiweni. Pia amewaasa vijana
kutojihusisha na mada ya kulevya. “Msitumike katika kubeba madawa hayo
matumboni mwenu au kuyauza reja reja,kataeni kutumikishwa,” alisisitiza Bibi
Fatma Mwassa.
Amewataka vijana watumie fursa zilizopo
ili waweze kujiendeleza badala ya kulalamika. Amewaasa watumie ujana wao vizuri
kama alivyoutumia Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere ambaye
tunaadhimisha miaka 15 ya kifo chake. Alisema Mwalimu aliutumia ujana wake
vizuri katika shughuli za kisiasa na kujipatia heshima kubwa.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga amesema kuwa Wiki ya
Vijana imekuwa jukwaa muhimu kwa Vijana wengi hapa nchini kwani upata fursa ya
kukutana na kujifunza kupitia maonyesho yanayoambatanana maadhimisho hayo.
Bibi. Sihaba aliongeza kuwa kumekuwapo
na matokeo chanya yanayotokana na maadhimisho hayo ambapo baadhi ya vijana
wenye dhamira wemepata kuwa wajasiriamali kupitia wa kubwa na wakati kupitia
maadhimisho hayo.
Wiki ya Vijana inaadhimishwa ikiwa
inatimizwa umri wa miaka 15 tokea ilipoanzishwa mnamo mwaka 2000 Mkoani
Kilimanjaro. Katika Wiki hii Vijana mbalimbali ujumuika pamoja katika
maadhimisho hayo ambayo kwa mwaka huu yanafanyoika mkoani Tabora na yatafikia
kilele chake tarehe 14 Oktoba ambayo ni siku ya Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na
kilele cha mbio za Mwenge.
No comments:
Post a Comment