Wasaniiwa muziki wa asili wakitoa burudani katika
tamasha la Jambo festival.
Mwenyekitiwa Tamasha la sanaa na utamaduni Arusha
maarufu kama JamboFerstival Augustine Michael
Namfua
Jiji la Arusha litatikiswa na tamasha la sanaa na utamaduni la
kimataifa maarufu kama Jambo festival litakalojumuisha ngoma za asili,mavazi ya asili ,muziki wa asili,mavazi na vyakula ,tamasha hilo litatikisa viunga vya jiji la Arusha ambalo ni kitovu cha utalii.
Takribani watu 3000 kutoka sehemu mbali mbali nchini na nje ya nchi
wanatarajia kuhudhuria tamasha hilo ambalo hutoa burudani isiyo kifani
na lenye kila aina ya ubunifu .
Wageni kutoka nchi za Afrika Mashariki Kenya,Rwanda,Burundi,Nchi za
Ulaya,Marekani na Asia wanatarajia kuhudhuria huku wenyeji wao wakiwa
ni wakazi wa Arusha.
Mwenyekiti wa Tamasha la Jambo Festival , Augustine Michael Namfua
anaeleza kuwa tamasha hilo limekua likifanyika miaka 2 mfulululizo na
kwa sasa linasubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa sanaa na utamaduni.
Augustine anaeleza kuwa kila mwaka wamekuwa wakifanya tamasha hilo
lengo ni kuonyesha kazi za sanaa hususani tamaduni.
Tamasha hili limekua likiwaunganisha kwa pamoja wapenzi wa sanaa na
utamaduni wa Watu wa Arusha,Tanzania na Afrika kwa ujumla hasa
ukizingatia kuwa Arusha ni makao makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki
na ni mji wa utalii.
"Katika matamasha yetu kumekuwa na uwepo wa jamii ya kimataifa ambao
wamekuwa wakifuatilia kwa karibu matamasha kwa njia ya mtandao na hata
kushiriki kwa wingi pia wapo wanaotuunga mkono" Alisema
Augustine
Mwenyekiti huyo anaeleza kuwa lengo la tamasha hilo kukuza sanaa na
utamaduni,kukuza uchumi wa Arusha mathalani katika kipindi cha tamasha
watu kutoka kona mbali mbali za dunia watakuja na kulala,kula na
kununua bidhaa zinazotokana na utamaduni.
Vikundi mbali mbali vya ngoma vitatoa burudani ya kukata na shoka
katika tamasha hilo la aina yake.
Wasanii kutoka nchi za Afrika Mashariki watapanda jukwaani na
kutumbuiza mziki wa live utakaokonga nyoyo za mashabiki na wapenzi
watakaojitokeza katika tamasha hilo ambapo kundi la Jambo Squard
wanaotamba na nyimbo ya Mamong'o watatoa burudani.
Wasanii wengine ni kama Santuri DJs CAB (kutoka Ufaransa), Damian
Soul, Christian Bella,DJ Kahlil, Msafiri Zawose, Jambo Squad, Maia Von
Lekow, Warriors from The East,Aqua Sound Band, Hisia,Jhikoman &
Afrikabisa Band, Heart Band, G Nako kutoka WEUSI,Nash MC,
Chaba,Shamsila.
Pia kutakua na maonyesho ya mavazi
ya kitamaduni ambapo yataandaliwa
na wabunifu mashuhuri ambao watakuwepo ikiwamo Ally Rehmtullah, Diana
Magesa,Salim Ally,Martin Kadinda,Nahuja Nuhu,Neema Meena,Zakia Ally.
Vile vile Kutakuwa na vyakula vya asili kutoka makabila mbali mbali ya
Tanzania na Afrika Mashariki pamoja na nchi washiriki bila kusahau
Nyama choma.
"Arusha ni mji
unaosifika kwa nyama choma katika tamasha hili
tumejiandaa
vyema watu wafike wapate nyama choma nzuri na
vinywaji
huku
wakifurahia mziki wa asili unaopigwa live" Alisema
Kwa upande wa
kiingilio ni bure kwa nyakati za mchana na baada ya
hapo
jioni
watatakiwa kulipa shilingi 5000 kama kiingilio
ambacho
kinasaidia
tamasha kuendesha shughuli zake.kutakuwa na sehemu
mbili
mchana na
usiku.
Tamasha la
Jambo Festival litafanyika jijini Arusha katika viwanja
vya
Nane Nane
vilivyopo eneo la Njiro jijini Arusha , litaanza siku
ya
ijumaa tarehe 3
hadi 5 octoba mwaka huu.Watu wote
wanakaribishwa
kufurahia sanaa
na utamaduni ambayo ni burudani isiyo na
kifani.
Jambo Festival
itapambwa na ngoma za utamaduni,muziki wa
jukwaani,vyakula vya asili,soko za sanaa za mikono pamoja
na michezo
ya watoto.
Tamasha hilo limedhaminiwa na Ubalozi wa
Ufaransa,Kituo cha Utamaduni
cha Ufaransa na wadhamini wengine na kuandaliwa na shirika la Idea
Afrika.habari picha kwa hisani ya woindeshizza blog
cha Ufaransa na wadhamini wengine na kuandaliwa na shirika la Idea
Afrika.habari picha kwa hisani ya woindeshizza blog
No comments:
Post a Comment