Friday, October 17, 2014

MAKOCHA JAMUHURI KIWELU (JULIO) NA AMRI SAID (STAM) WAMPIGA MKWARA MWAMUZI MECHI YA LIGI DARAJA LA KWANZA. MOSHI

Wachezaji wa timu ya Mwadui FC, wakishangilia goli lililofungwa na Bakari Kigodeko, katika mchezo wa ligi daraja la kwanza dhidi ya Panone FC, uliofanyika kwenye Dimba la Ushirika, mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 1-1.
Sehemu ya mashabiki waliojitokeza kwenye dimba la Ushirika, wakifuatilia mchezo kati ya Mwadui na Panone.
Mashabiki wa Panone wakishangilia goli la kusawazisha lililopatikana katika dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza, likifungwa na Tony Kigundu.
Shangwe zikaendelea
Kocha msaidizi wa Klabu ya Mwadui, Amri Said, akizuiwa na mwamuzi wa mezani, Thomas Mkombozi wakati akijaribu kutaka kumfuata mshika kibendera namba moja akipinga maamuzi akipinga maamuzi ya kuingia kwa bao la Panone FC alilodai lilikuwa la utata.
Ubabe ukatumika...
Hapa akimrudisha Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kiwelo 'Julio' katika eneo lake.
Benchi la Ufundi la Mwadui FC, wa kwanza kushoto ni kocha mkuu Jamhuri Kiwelo 'Julio', kulia.
Julio akitoa maelekezo kwa mchezaji wake
Mwokota mipira akiwa katika pozi.
Sehemu ya Jukwaa kuu likiwa limesheheni mashabiki
Wachezaji wakitoka mapumziko
Mmoja wa viongozi wa Benchi la Ufundi la Mwadui FC, aliamua kuwavaa maaskari wa Jeshi la Polisi.
Kocha Jamhuri Kiwelo katikati ya dimba 
Waamuzi wakiondolewa uwanjani kwa Ulinzi mkali muda wa Mapumziko.
Kocha wa Panone FC, Maka Marwisi, akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mapumziko.

Hivi karibuni Bodi ya Ligi iliamuru kujengwa Uzio kuzunguka eneo la ndani ya Uwanja 'Pitch" kwa ajili ya usalama wa wachezaji lakini cha kushngaza kama inavyoonekana hapo, hizo ni pikipiki "Bodaboda" zikiwa zimeegeshwa ndani ya uzio huo, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa wachezaji hao.
Jamhuri Kiwelo akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.
Heka heka za kuwania mpira ukiendelea katika mchezo huo mkali.
Mchezaji wa Panone FC, akikimbilia mpira
Wachezaji wa Panone FC, wakitoa huduma kwa mchezaji wao aliyeumia.
Hapa wakiwa wamembeba....hili ni tukio la kushangaza na la aibu kweli..
Benchi la ufundi la Panone FC, walipochukua jukumu ya timu ya usalama ya msalaba mwekundu.
Panone FC, wakifanya mabadiliko
 


















 
Mwadui FC wakifanya mabadiliko.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya kaskazini.


No comments: