Monday, October 13, 2014

KAGERA WAANZA VYEMA COPA COCA COLA 2014, WAICHAPA GEITA BAO 2-0 KATIKA UWANJA WA KAITABA LEO

Na Faustine Ruta, Bukoba

Kagera wameanza vyema Mashindano ya soka kwa vijana walio chini ya miaka 15, Copa Coca Cola, Leo Jumapili 12.10.2014 Asubuhi baada ya kuichapa Timu ya Geita bao 2-0 kwenye Uwanja wa Nyumbani Kaitaba.
Bao za Kagera zimefungwa kipindi cha kwanza na cha pili. Bao la kwanza limefungwa kipindi cha kwanza dakika ya 28 na Avith Frolian aliyekuwa amevalia jezi namba 10. Na bao la pili lilifungwa kipindi cha pili dakika ya 61 na Kepteni wao Patrick Amos baada ya Kagera kupiga kona na Kepteni wake kuruka juu na kufunga kwa kichwa.

Kagera watarudiana na Geita kwao jumamosi tarehe 18 wiki ijayo.
Wachezaji wa Kagera Waliochini ya Miaka 15 wakishangilia baada ya mpira kumalizika kwenye Uwanja wa Kaitaba dhidi ya Geita kwenye Mashindano ya Copa Coca Cola, Mchezo uliochezwa leo Jumapili 12.10.2014. Kagera wameifunga Geita Bao 2-0.
Mchezaji wa Kagera akiendesha...Mashambulizi kwa timu ya Geita leo jumapili Asubuhi.
Patashika kwenye lango la Geita, Kona ilipigwa na mchezaji Kepten wa Kagera kujitwisha kichwa na kufunga bao katika kipindi cha pili dakika ya 61.
Wachezaji wa Kagera Waliochini ya Miaka 15 wakishangilia bao lao la pili lililofungwa na Timu Kepteni wao Patrick Amos.
Wachezaji wa Kagera wakishangilia bao lao baada ya kufanya 2-0 dhidi ya Geita kwenye Uwanja wa Kaitaba
Ushindi
Kipute kikiendelea dakika za mwishoni, Geita walipania kurudisha lakini bahati haikuwa yao ngoma ilibaki pale pale 2-0 mpaka dakika 90 zinamalizika.
Kocha wa Geita akiwapa mbinu wachezaji wake
Mchezaji wa Kagera Luckman Mansuri akimlinda mchezaji wa Geita kwenye kasi kufukuzia mpira
Mansuri akitawala mpira
Waamuzi wa kipute hicho wakitoka Uwanjani baada ya dakika 90 kumalizika.
Wachezaji wa Kagera wakiomba kwa Ushindi walioupata katika mchezo wao wa kwanza katika Uwanja wa Kaitaba Dhidi ya Geita wa 2-0. Kagera watawafuata Nyumbani Geita tarehe 18 kurudiana nao kwani Michezo ya Copa Coca Cola kwa mwaka huu 2014 ni Nyumbani na Ugenini.

No comments: