Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiutangazia umati wa watu
waliofurika kwenye uwanja wa mikutano Sunga kurejea rasmi kwa Charles
Kagonji (mwenye shati la kitenge) kwenye Chama Cha Mapinduzi akitokea
Chadema,wengine katika picha hii ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana ,na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lushoto Balozi Abdi Hassan Mshangama
Mzee Charles Kagonji akiwasalimia wananchi na kutamka rasmi kurejea CCM yeye pamoja na wafuasi wake aliokuwa nao Chadema.
Katika
mkutano huu wengine waliorudi CCM kutoka Chadema ni aliyekuwa
Mwenyekiti wa Jimbo Ismail Semkunde,aliyekuwa Katibu wa Jimbo Mzee
Julius Kavurai na aliyekuwa mgombea wa udiwani kwa tiketi ya Chadema
Ndugu Ally Gaha
Wananchi wakinyoosha mikono juu kama ishara ya kumkaribisha CCM Mzee Charles Kagonji
Mzee Charles Kagonji akishukuru kurudi nyumbani CCM
Mzee
Julius Kavurai aliyekuwa Katibu wa Jimbo la Mlalo Chadema akiwapungia
mkono wananchi kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana ambaye yupo kwenye ziara wilayani Lushoto ya kujenga na
kukiimarisha chama pamoja na kuangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi
ya CCM 2010 inavyoendelea.
Umati wa watu waliohudhuria mkutano.
CCM juu!!!
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha juu kadi ya CCM tayari
kumkabidhi Mzee Charles Kagonji ambaye ameorudi CCM kutokea Chadema.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya CCM Mzee
Charles Kagonji kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Sunga
jimbo la Mlalo wilayani Lushoto.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pongezi Mzee Charles Kagonji kwa uamuzi wake wa kurudi CCM.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pongezi Ndugu
Ismail Semkunde aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo la Mlalo Chadema na kuamua
kurejea CCM.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lushoto Balozi Abdi Hassan Mshangama akihutubia wakazi wa kata ya Sunga kwenye mkutano wa hadhara.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lushoto Balozi
Abdi Hassan Mshangama (katikati) akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya
Lushoto Majid Hemed Mwanga (kulia) pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa
Jimbo la Mlalo Chadema Ndugu Ismail Semkunde.
No comments:
Post a Comment