Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe. John Henjewele (kushoto) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Jopo la
Majaji kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za
Jamii na Uwezeshaji Prof. Samwel Wangwe ( wa pili kutoka kulia) mara
timu hiyo ilipofika kwenye ofisi yake kabla ya kuanza ziara yake rasmi kwenye mgodi wa North Mara.
Mwenyekiti wa Jopo la
Majaji kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za
Jamii na Uwezeshaji Prof. Samwel Wangwe (kushoto) akisalimiana na Afisa Mahusiano wa Mgodi wa North Mara Bw. Zakayo Kalebo (kulia) mara baada ya jopo hilo kuwasili kwenye mgodi huo.
Meneja Mahusiano wa Mgodi
wa North Mara Bi Fatuma Mssumi (mbele) akielezea shughuli za mgodi wa
North Mara mbele ya jopo la majaji waliotembelea mgodi huo ili kuendelea
na zoezi lake la kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji.
Afisa
Mahusiano wa Mgodi wa North Mara Bw. Zakayo Kalebo (wa tatu kutoka
kushoto) akielezea mchango wa mgodi wa North Mara katika ujenzi wa
nyumba za wauguzi wa zahanati ya Matongo (zinazoonekana nyuma) mbele ya timu ya majaji na sekretarieti iliyotembelea mradi wa nyumba hizo. Mradi wa nyumba hizo uligharimu Dola za Marekani 100,000.
Afisa Uhusiano wa Kijiji cha Matongo Bw. Magesa Wanjara akionesha jinsi ya kutumia bomba la kisima cha maji kilichofadhiliwa na mgodi wa North Mara mbele ya timu ya majaji, sekretarieti na wajumbe wengine.
Afisa
Mahusiano wa Mgodi wa North Mara Bw. Zakayo Kalebo ( wa tano kutoka
kushoto) akielezea mchango wa mgodi wa North Mara katika uwezeshaji wa
kikundi cha vijana katika mradi wa kitalu cha mboga za majani, mbele ya
majaji na sekretarieti iliyotembelea kitalu hicho. (kinachoonekana kwa
nyuma)
Mwenyekiti wa Umoja wa Kikundi cha Vijana cha Nyakegema Bw. Zacharia Mwita ( wa pili kutoka kulia) akitoa maelezo mbele ya timu ya majaji na wajumbe wengine kuhusu mchango wa mgodi wa North Mara kwa kikundi hicho kupitia mradi wake wa mboga za majani. Kikundi hicho kina jumla ya vijana 578 kutoka katika vijiji saba vinavyouzunguka mgodi huo.
Afisa
Mahusiano wa Mgodi wa North Mara Bw. Zakayo Kalebo (wa tatu kutoka
kulia) akitoa maelezo mbele ya majaji, sekretarieti na wajumbe wengine
juu ya mchango wa mgodi wa North Mara katika ujenzi wa shule ya sekondari ya Ingwe ( inayoonekana kwa nyuma)
Mwenyekiti wa Jopo la
Majaji kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za
Jamii na Uwezeshaji Prof. Samwel Wangwe (kushoto) akisalimiana na Makamu
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ingwe Bw. Alfred Joseph mara timu hiyo
ilipofanya ziara kwenye shule hiyo iliyofadhiliwa na mgodi wa North Mara.
No comments:
Post a Comment