Mratibu
wa Rock City Marathon kutoka kampuni ya Capital Plus International Ltd,
Bi Grace Sanga (wa kwanza kulia) akipongezwa na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo
Tanzania (BMT) Bw. Dioniz Malinzi (Wa nne kulia) ambaye alikuwa Mgeni Rasmi
katika uzinduzi wa Rock City Marathon 2014, jana jijini Dar es Salaam
jana. Mbio hizo zitafanyika tarehe 26 Oktoba katika uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza.
Baadhi ya wawakilishi wa wadhamini wa mbio za Rock
City Marathon 2014 pamoja na viongozi wa chama cha mchezo wa riadha Tanzania,
wakifuatilia yanayojiri wakati wa uzinduzi wa mbio hizo jana iliyofanyika
Jijini Dar es Salaam. Mbio hizo zitafanyika tarehe 26 Oktoba
katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Msemaji wa Kampuni ya Capital Plus
International, ambao ni waandaaji wa mbio za Rock City Marathon, Bw. Mathew
Kasonta, akizungumuza na wageni waalikwa katika uzinduzi wa mbio hizo jana
iliyofanyika Jijini Dar es Salaam. Mbio hizo zitafanyika tarehe 26 Oktoba
katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF ) Bw. Jumanne Mbepo, ambao ndo wadhamini wakuu
wa mbio za Rock City Marathon 2014, akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa
mbio hizo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo zitafanyika tarehe
26 Oktoba katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha
Tanzania (RT), Suleiman Nyambui akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa mbio
hizo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam jana. Mbio hizo zitafanyika tarehe 26
Oktoba katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Afisa Uhusiano na mawasiliano wa TSN Group
Koiya Kibanga, ambao ni moja wa wadhamini wakuu wa mbio za Rock City Marathon
2014, akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa mbio hizo iliyofanyika Jijini
Dar es Salaam jana. Mbio hizo zitafanyika tarehe 26 Oktoba katika uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza.
====== ======= ======
Mwenyekiti wa Baraza
la Michezo Tanzania (BMT), Bw. Dioniz Malinzi, amezindua rasmi mbio za Rock
City Marathon, zitakazofanyika Oktoba 26 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza.
Akizungumza katika uzinduzi huo jana
jijini Dar es Salaam, Malinzi alisema mbio hizo zimeweza kuwa ni moja ya mbio
zinazoheshimika nchini Tanzania na kuiweka kanda ya ziwa katika kalenda ya
michezo kila mwaka.
Malinzi aliipongeza kampuni ya Capital
Plus International (CPI) kwa kuendelea kujidhatiti katika maandalizi ya mbio
hizo na kuziboresha kila mwaka licha ya changamoto nyingi zinazoukabili mchezo
huo wa riadha nchini.
“Ni kweli kwamba makampuni na
hata watu binafsi wamekuwa wakisaidia kukuza mchezo wa riadha hapa nchini,
lakini bado mchezo huu unachangamoto nyingi.
“Jitihada za pamoja zinahitajika baina
ya serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, sisi Baraza
la Michezo la Taifa (BMT), vyama vya michezo, mashirika na wadau wengine, ili
kurejesha heshima iliyopotea miongoni mwa michezo na wanamichezo wa Tanzania,
hususani riadha,” alisema Bw. Malinzi.
Bw. Malinzi alibainisha kuwa na kuwepo
kwa changamoto mbali mbali CPI imekuwa ikijitahidi kuboresha mbio hizo zifanyikazo
kila mwaka.
“Tumeshuhudia viwango vya mbio hizi
vikipanda kila mwaka, ambapo ni kielelezo cha maandalizi mazuri yanayofanywa
kwa kuzingatia viwango na sheria zilizo wekwa,” aliongeza Bw. Malinzi.
Hata hivyo, Mwenyekiti huyo wa BMT
alisisitiza kuwa vyama vya michezo pia vinapaswa kujiimarisha katika kuwaandaa
wachezaji kabla ya kuwapeleka kushiriki katika mashindano ya kimataifa ambapo
wachezaji hao wanabeba jina la nchi ya Tanzania.
“Hatunabudi kuimarisha msingi wetu
katika kila aina ya michezo hapa nchini, kama bado tunayo ndoto ya kuirudisha
ramani ya Tanzania katika ulimwengu wa michezo kama ilivyokuwa zamani,”
alisisitiza.
Tukio hilo limewavutia wadau wengi wa
michezo nchini, ikiwa ni pamoja na makampuni makubwa kama Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF), Kampuni ya TSN Group Ltd, Bodi ya Utalii Tanzania
(TTB), African Barrick Gold, Nyanza Bottlers, Mfuko wa Pensions (PPF), Sahara
Communication, ATCL, New Mwanza Hotel, na New Africa Hotel ambao wamejitokeza
kudhamini mbio hizo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa kampuni
ya Capital Plus International, Bw. Mathew Kasonta, alisema mbio za mwaka huu
zitahusisha mbio za nusu Marathon za kilomita 21, mbio za kujifurahisha maarufu
kama Corporate Race za kilomita 5, mbio za watu wenye ulemavu wa ngozi za
kilomita 3, mbio za watu wazima za kilomita 3 na mbio za watoto kuanzia miaka
saba hadi 10 ambazo ni za kilomita 2.
Bw. Kasonta alisema kuwa mbio hizo
zinaenda sambamba na kuhamasisha Utalii wa ndani kupitia sekta ya michezo,
ambapo washiriki watakua ni kutoka kanda ya ziwa Victoria na nchi jirani kama
Kenya, Uganda, Afrika Kusini na baadhi yao wakiwa na uzoefu wa kucheza
mashindano ya kimataifa ili kutoa ushindani zaidi.
“Ningependa kutoa shukrani zangu za
dhati kwa wafadhili mbalimbali wanaoshirikiana nasi ili kuyafanikisha
mashindano haya, kwa niaba ya Capital Plus International, ningependa
kuwahakikishia kuwa mashindano ya mwaka huu yataboreshwa zaidi na hivyo
yataweza kutupatia wanariadha bora watakaoiwakilisha nchi yetu kikamirifu
katika mashindano ya kimataifa,” alisema Bw. Kasonta.
No comments:
Post a Comment