Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakwanza
kushoto akiwa na Waziri wa Ujenzi
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Mbunge wa Mpwapwa Mheshimiwa Gregory Teu
pamoja na Mbunge wa Kibakwe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa George Simbachawene, akiweka jiwe la msingi kama
ishara ya kuzindua rasmi ujenzi wa Daraja la Mto Gulwe lenye urefu wa mita 170
litakalo unganisha kati ya Wilaya ya Mpwapwa na Kibakwe.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la
Anglicana Tanzania Jacob Chimeleja, Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli,
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi, Mbunge wa Mpwapwa Mheshimiwa
Gregory Teu, Mbunge wa Kibakwe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa George Simbachawene pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara
ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe, akikata
utepe kuashiria uzinduzi rasmi ujenzi wa Daraja la Mto Gulwe lenye urefu wa
mita 170.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakiwa
katika picha ya pamoja na Mkandarasi,viongozi
wa dini na kitaifa mara baada ya Rais kuzindua rasmi ujenzi wa daraja la Gulwe.
Daraja
la Gulwe linalotumika sasa kama linavyoonekana hali iliyopelekea Serikali ya
awamu ya nne kupitia Wizara ya Ujenzi kuanza kujenga daraja kubwa na la kisasa
la Gulwe litakalokuwa na mita 170 mara baada ya kukamilika kwake.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati akipita
mbele ya Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa Daraja la Gulwe lenye urefu wa
Mita 170.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wapili kutoka kulia akiwa na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe wakwanza kulia,
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi ERB Profesa Ninatubu Lema watatu
kutoka kulia pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini TANROADS Mhandisi
Patrick Mfugale wakifatilia ngoma za asili kabla ya uzinduzi rasmi wa Daraja la
Gulwe
Ujenzi
wa Makalvati yatakayosaidia Daraja kupitisha maji katika mto Gulwe kama
yanavyoonekana. Jumla ya Makalvati tisa yatajengwa katika daraja hilo la mita
170.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete ili kuweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi ujenzi
wa Daraja la Gulwe lenye urefu wa mita 170.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akizungumza na Mbunge
wa zamani wa Mpwapwa George Malima Lubeleje kabla ya uzinduzi rasmi wa ujenzi
wa Daraja la Gulwe lenye urefu wa mita 170.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe wakwanza kulia akiwatambulisha
Wakurugenzi, Wenyeviti, Wakuu wa Taasisi zilizochini ya Wizara ya Ujenzi kabla
ya uzinduzi rasmi wa ujenzi wa Daraja la Gulwe litakalokuwa na mita 170.
===== ========
Jiwe la msingi daraja la Gulwe-Wilayani
Mpwapwa.
Rais Jakaya
Kikwete amesisitiza kuwa ujenzi wa daraja la Gulwe katika mto Sinyasungwi ni
mwanzo wa ujenzi wa barabara ya Mbande-Kongwa-Mpwapwa-Kibakwe yenye urefu wa
kilomita 101, kwa kiwango cha lami.
Akiweka jiwe
la msingi na kuzindua ujenzi wa daraja hilo lenye urefu wa mita 170 na uwezo wa
kupitisha tani 150 rais kikwete amesema daraja hilo licha ya kuunganisha jimbo la
Mpwapwa na Kibakwe pia litamaliza kero ya muda mrefu iliyokuwa ikiathiri
barabara na reli katika eneo la Gulwe na Godegode wilayani Mpwapwa.
“Kukamilika
kwa daraja hili itakuwa jawabu la kudumu kwa reli na barabara katika eneo la
Gulwe na hivyo kazi yenu sasa ni kutunza mazingira ili maji yafuate mkondo na
hivyo kutoathiri miundombinu na mashamba ili kukuza shughuli za
kilimo”,amesisitiza Rais Kikwete.
Naye Waziri wa
ujenzi Dkt. John Magufuli amezungumzia umuhimu wa halmashauri nchini ikiwemo ya
Mpwapwa kutumia fedha za mfuko wa barabara kujenga barabara zake kwa kiwango
cha lami ili kuboresha miundombinu ya miji na kuwataka wananchi kuacha kuchimba
mchanga karibu na madaraja na barabara ili kulinda miundombinu hiyo na
kuiwezesha kudumu kwa muda mrefu.
Dkt.
Magufuli amesema ujenzi wa barabara ya Mbande-Kongwa-Mpwapwa-Kibakwe hadi Chipogoro
yenye urefu wa kilomita 120, utafanyika kwa awamu tatu ambazo ni
Mbande-Kongwa-Mpwapwa, Mpwapwa-Kibakwe na Kibakwe-Chipogoro ili kuiunganisha
barabara hiyo na ile ya tanzam na hivyo kuiunganisha wilaya ya Mpwapwa na kupunguza
magari yaendayo Morogoro na Dare s salaam kupitia Dodoma.
Afisa Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa barabara nchini (TANROADS), mhandisi Patrick Mfugale amesema
ujenzi wa daraja la Gulwe lenye urefu wa mita 170 utahusisha ujenzi wa
makalvati 9 yatakayosaidiana na daraja kupitisha maji na barabara ya kilomita
1.5 kila upande wa daraja na linatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi bilioni
3.3 litakapokamilika na litakuwa na uwezo wa kubeba tani 150 kwa wakati mmoja.
No comments:
Post a Comment