Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania
(MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakati akiwasili eneo la Mambogo katika manispaa ya wilaya ya Morogoro tayari kukagua na kufungua rasmi mradi mkubwa wa maji ambao umegharimiwa na
Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Rais Kikwete akisalimiana na mmoja wa wataalamu walioshughulikia ufungwaji wa mtambo huowakati akiwasili eneo la Mambogo katika manispaa ya wilaya ya Morogoro tayari kukagua na kufungua rasmi mradi mkubwa wa maji ambao umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Rais Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Morogoro mjini Mhe Aziz Aboud wakati akiwasili eneo la Mambogo katika manispaa ya wilaya ya Morogoro tayari kukagua na kufungua rasmi mradi mkubwa wa maji ambao umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Rais Kikwete akisalimiana na mmoja wa wadau wa mji wa Morogoro wakati akiwasili eneo la Mambogo katika manispaa ya wilaya ya Morogoro tayari kukagua na kufungua rasmi mradi mkubwa wa maji ambao umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Jengo la mradi mkubwa wa maji ambao umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Vijana wakishangilia wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa mradi mkubwa wa maji ambao umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Baadhi ya wafanyakazi wa MORUWASA wakishangilia wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa mradi mkubwa wa maji ambao umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Burudani wakati wa sherehe hizo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakati wa sherehe hizo
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Joel Bendera akifungua pazia la sherehe hizo
Sehemu ya jengo la mradi huo
Kwa ubavuni
Afisa Mtendaji Mkuu wa MCA-Tanzania Mhe Bernard Mchomvu akitoa muhtasari wa mradi huo
Bango linajieleza
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhe Mbogo Futakamba akipokea kwa niaba ya serikali hati rasmi ya kukamilika kwa mradi kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa MCA-Tanzania Mhe Bernard Mchomvu
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhe Mbogo Futakamba akimkabidhi hati hiyo Mkurugenzi Mkuu wa MORUWASCO Bw. Nicholaus Angumbwike
Mkurugenzi Mkuu wa MORUWASCO Bw. Nicholaus Angumbwike akifurahia
Mkurugenzi Mkuu wa MORUWASCO Bw. Nicholaus Angumbwike akimshukuru Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakati wa sherehe hizo
Rais Kikwete akimpongeza Afisa Mtendaji Mkuu wa MCA-Tanzania Mhe Bernard Mchomvu kwa kufanuikisha mradi
Mkurugenzi Mkuu wa MORUWASCO Bw. Nicholaus Angumbwike akiongea machache
Mama Salma Kikwete akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa MORUWASCO Bw. Nicholaus Angumbwike
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher akisoma hotuba yake kwa Kiswahili wakati wa sherehe hizo
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhe Mbogo Futakamba akiongea wakati wa sherehe hizo na kumkaribisha Rais Kikwete aongee na wananchi
Rais Kikwete akizungumza na kuzindua rasmi mradi huo mkubwa
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakifunua pazia kuzindua mradi huo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakifurahgia baada ya kuzindua mradi huo
Rais Kikwete akibofya kitufe kupiga king'ora kuzindua rasmi mradi huo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher na viongozi wengine wakielekea kukagua mradi huo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakikata utepe kuzindua mradi huo
Rais Kikwete akipata maelezo ya mradi toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa MORUWASA
Sehemu ya mitambo ya mradi huo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakikagua mitambo ya mradi huo
Mkurugenzi Mkuu wa MORUWASCO Bw. Nicholaus Angumbwike akiendelea kutoa maelezo ya mradi
Ukaguzi ukiendelea
Ukaguzi wa sehemu ya kusafishia maji
Ukaguzi ukiendelea
Namna maji yanavyosafishwa
Mitambo ya kisasa ya kuendeshea mtambo wa mradi huo
Eneo la mitambo
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa wamemaliza kutembelea mradi huo wa maji
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher na viongozi wengine katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na watendaji wa MCA-Tanzania
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher na viongozi wengine katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na wafanyakazi wa MORUWASA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher na viongozi wengine katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na wafanyakazi wa MORUWASA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher na viongozi wengine katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na wafanyakazi wa MORUWASA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher na viongozi wengine katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na wafanyakazi wa MORUWASA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher na viongozi wengine katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na wakanfdarasi wa mradi huo
Rais Kikwete akiwa katika hatua ya mwisho ya sherehe hizo ambayo ni kufungua bomba na kujaza maji kwenye ndoo...kisha kumtwika mmoja wa kinamama wa mkoa wa Morogoro wataonufaika na mradi huo. PICHA NA IKULU
JK: Acheni woga na udhaifu wa kusimamia sheria
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewataka
viongozi nchini kuacha woga na ulegevu katika kusimamia sheria za kulinda
mazingira na vyanzo vya maji ambayuo ni namna ya uhakika ya kuwawezesha
wananchi kuendelea kupata maji ya uhakika, safi na salama.
Aidha,
Rais Kikwete amewataka watu wanaokopa fedha katika vyama vya ushirika vya akiba
na mikopo kuhakikisha kuwa wanarudisha fedha hizo kwa wakati kwa sababu
kushindwa kurudisha mikopo hiyo kwa wakati kunawarudisha nyuma wengine ambao
pia wanahitaji mikopo hiyo.
Rais
Kikwete amesema hayo jana, Ijumaa, Agosti 22, 2014 kwenye siku yake ya tatu ya
ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Morogoro ambako ametembelea, amekagua na
kuzindua miradi ya maendeleo ya wananchi katika Wilaya ya Morogoro na Manispaa
ya Morogoro.
Akizindua
mradi mkubwa wa maji ambao umbao umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia
Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) katika Manispaa ya Morogoro,
Rais Kikwete aliwaambia viongozi wa Manispaa ya Morogoro na wengine nchini:
“Aacheni
ulegevu, acheni woga, kazi yenu haiwezi kutoa simulizi kwa sababu mamlaka yote
ya kuzuia watu kulima na kujenga katika maeneo ya vyanzo vya maji mnayo.
Yatumieni.”
Rais
Kikwete ambaye pia alirudia ujumbe huo kwa viongozi kwenye mkutano wa hadhara
kwenye Uwanja wa Jamhuri aliwaambia viongozi hao:
“Shughuli
za binadamu za kilimo na makazi haziwezi kuruhusiwa katika vyanzo vya maji.
Acheni tabia hii ya kushindwa kusimamia sheria na kutumia mamlaka ambayo mnayo.
Mkiendekeza tabia hii iko siku wananchi wa Morogoro mjini watakosa maji
kabisa.”
Rais
Kikwete alikuwa anajibu malalamiko ya awali ya uongozi wa Manispaa ya Morogoro
ambao ulikuwa umemwomba Rais alitangaze eneo la Milima ya Uluguru na Bwawa la
Mindu kuwa hifadhi za taifa kutokana na kuwa vyanzo vikuu vya maji kwa wakazi
wa Manispaa ya Morogoro.
“Hamna
mtu wa kumnung’unikia. Kazi yake hawezi kuwa kumsubiri Rais ili kumsimulia
kuhusu haya. Najua mkichukua hatua wako wanasiasa ambao watajitia wanawatetea
wananchi, lakini kwenye hili la kulinda vyanzo vya maji hakuna la msalie
Mtume.Kama sehemu nyingine kama kule Kinole (Wilaya ya Morogoro) wameweza, nini
kinawashinda nyie kuwaondoa watu kwenye vyanzo vya maji?”
Mradi
huo wa Ukarabati wa Miundombinu ya Maji Safi katika Manispaa ya Morogoro
ulioanza kujenga mapema mwaka 2011 kwa gharama ya sh bilioni 56 kutoka Serikali
ya Marekani na kupitia MCA-Tanzania, utaongeza kiwango cha kupatikana kwa maji
safi na salama kwa wakazi wa Manispaa kutoka mita za ujazo 29,000 hadi 33,000 kwa
siku na kunufaisha maelfu ya wananchi.
Hata
kama ni kweli kuwa mradi huo hautamaliza mahitaji yote ya maji kwa Manispaa ya
Morogoro, ambayo ni mita za ujazo 39,400 bado zitawezesha upatikana wa maji kwa
kiasi cha asilimia 85 kwa wakazi wa Manispaa hiyo na hivyo kuboresha maisha ya
wakazi hao.
Rais
Kikwete amewaomba wananchi wa Manispaa ya Morogoro na viongozi wao kutunza
miundombinu hiyo na kuhakikisha kuwa maji yanaendelea kupatikana kwa wakazi wa Manispaa.
“Tukifanya hivyo, hata hao waliotusaidia wataona kuwa tumewaheshimu.”
Mapema
jana hiyo hiyo, Rais Kikwete alitembelea eneo la Kinole na kuzindua Chama cha
Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Kinole – SACCOS- ambacho kilindikishwa rasmi
mwaka 2001 na mpaka sasa kimetoa mipoko ya kiasi cha sh bilioni nne kwa
wanachama wake wapatao 1,700.
Rais
Kikwete amekuwa kiongozi mkuu wa pili wa Tanzania kutembelea Kinole tokea Baba
wa Taifa Mwalimu Nyerere ambaye alitembelea eneo hilo mwaka 1961 na wananchi
walionyesha furaha yao kwa ujio huo kwa kumsimika Rais Kikwete kuwa Chidukila,
yaani chifu msaidizi wa eneo hilo.
Rais
Kikwete aliwapongeza wananchi wa Kinole kwa kuendesha SACCOS yenye mafanikio
makubwa na manufaa kwa wakulima wa eneo hilo ambao miongoni mwa mambo mengine
huingiza sokoni kiasi cha fuso 10 za ndizi kila siku.
“Huu
ni ukombozi kwenu. Haya ndio maisha bora kwetu kwa sababu hii mikopo ambayo
mnapata msingeweza kuipata kwa mabenki. Benki hiyo rafiki wa masikini. Benki
haikopeshi masikini, asiyekuwa nacho hapati kutoka benki.”
Rais
Kikwete alihimiza kurudishwa kwa wakati kwa mikopo inatolewa na chama hicho
akisisitiza kuwa wale ambao wanachelewesha kurudisha mikopo “wanawarudisha
nyumba wenzao ambao nao wanataka mikopo.”
Rais
Kikwete amekatisha ziara hiyo ya siku saba Mkoani Morogoro kwenda Arusha, Tanga
na Dar Es Salaam kwa siku moja kwa shughuli nyingine za kitaifa. Ziara hiyo
itaendeleo tena kesho, Jumapili, Agosti 24, 2014.
No comments:
Post a Comment