Ofisa
Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mohammed Dewji (Mb) (wa pili kushoto) na
Mkurugenzi Mtendaji wa Rand Merchant Bank (RMB), Bw. Bruce Macfarlane
(wa pili kulia) wakitiliana saini ya mkopo huo wa bilioni 300 za
kitanzania. Kushoto ni Makamu wa Rais wa MeTL GROUP, Vipul Kakad na
kulia ni Gregory Havermahl wa RMB wakishuhudia tukio hilo la utiliaji
saini wa mkopo baina ya RMB na MeTL Group.
Kampuni
ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) imetiliana saini
mkataba na benki ya Rand Merchant (RMB) ya Afrika Kusini utakaoiwezesha
kupata mkopo wa zaidi ya sh bilioni 300. Mkataba huo umetiwa saini
nchini Afrika Kusini na Ofisa Mtendaji Mkuu MeTL GROUP, Mohammed Dewji.
Akizungumza
kabla ya kutiwa saini kwa mkataba huo,Dewji alisema kwamba mkataba huo
wa kihistoria unatokana na RMB kuiamini kampuni yake ya MeTL tangu
walipoanza mahusiano ya kibiashara mwaka 2007.
“MeTL
na RMB tulianza mahusiano yetu mwaka 2007, wakati RMB ilipotukopesha
dola za Marekani milioni 7.5million. Wakati huo MeTLilikuwa na bidhaa
mbili tu,ngano na sukari! Toka wakati huo, MeTL imekuwa ikikua na
kuongeza bidhaa zaidi.” Alisema Dewji na kuongeza kuwa mwaka jana 2013,
uwezo wa MeTL wa kukopa sasa umefikia dola milioni 100.
Dewji
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini amesema kampuni yake
imekuwa na mafanikio makubwa kibiashara mpaka kuaminiwa na benki
mbalimbali za ndani na nje ya nchi. Pamoja na mkopo huo kwa MeTL hivi
karibuni kupitia kampuni yake dada ya kuingiza, kuhifadhi na kusambaza
mafuta nchini ya Star Oils Ltd, ilipata mkopo wa sh. bilioni 100 kutoka
kwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).
“Mwaka
1999 wakati najiunga katika kampuni hii ya kifamilia biashara yetu
ilikuwa ni ya dola za marekani milioni 26 na sasa tumejiongeza mara
zaidi ya 60 kwani sasa pato letu litafikia dola za Marekani bilioni 1.5
ifikapo mwishoni mwa mwaka”, alisema Dewji.
Alisema
mafanikio yalkiyopatikana ya kulipa mikopo husika yamewezesha yeye
kusaini mkataba wa mkopo wa dola za Marekani milioni 200 ikiwa ni mwaka
mmoja tu tangu wafikie uwezo wa kukopa dola milioni 100 za Marekani.
“Ninataka kusema kwamba maendeleo makubwa ya MeTL yasingelifikia hapa
bila RMB kutuamini katika hatua za awali” alisema ofisa mtendaji huyo
ambaye pia alielezea kazi mbalimbali zinazofanywa na MeTL.
Alisema
kampuni yake inafanya shughuli anuai kwenye sekta mbalimbali, ikiwemo
kilimo na viwanda, lojistiki, huduma za fedha,majumba ya biashara,
petroli,vinu vya kusindika nafaka,vifaa vya plastiki, usambazaji na
masuala ya simu.
Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mohammed Dewji (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji wa Rand Merchant Bank (RMB), Bw. Bruce Macfarlane wakinywa shampeni baada ya kufanya "Toast" kama ishara ya kutakiana kheri na mafanikio kwenye biashara zao.
Akisaini
mkopo huo, Dewji aliwashukuru wote waliohudhuria hafla hiyo ya kusaini
kati ya kampuni yake MeTL na RMB huku ikijivunia kufanya biashara katika
nchi za Ethiopia, Malawi, Msumbiji, Zambia, Dubai, Uganda, Rwanda,
Burundi, Congo, Sudan Kusini na Kenya.
Alisema
kwamba kampuni hiyo inataka kujiimarisha zaidi katika sekta
mbalimbali.MeTL kwa sasa ina viwanda zaidi ya 31 nchini Tanzania pekee;
huku ikiwa imetawanyika katika nchi 11 zilizopo Kusini mwa jangwa la
Sahara. "Tumejitanua katika nchi mbalimbali barani Afrika, nashukuru kwa
ushirikiano mzuri ambao umechangia mafanikio makubwa ya kampuni yetu",
alisema Dewji.
Dewji
maarufu kwa jina "MO" anasema elimu aliyoipata katika Chuo Kikuu cha
Georgetown nchini Marekani ndio iliyomfumbua macho na kuona umuhimu wa
kutumia fursa za ushindani wa kibiashara duniani. “Nia yetu ni kuwa na
nguvu kubwa ya kibiashara Afrika Mashariki na Kati tukipania MeTL kuwa
na pato la zaidi ya dola za Marekani bilioni 5 kwa mwaka ifikapo mwaka
2018 na kutengeneza ajira za watu 100,000.” Alisema Dewji.
Alisema
katika hotuba yake hiyo kuwa siri ya mafanikio ya kampuni ya MeTL ya
kukua kwa zaidi ya mara 60 katika kipindi cha miaka 15 tangu alipojiunga
nayo kuwa ni kutumia vyema fursa zilizopo na pia hamu yangu ya
kuwatumikia na kuboresha maisha ya watanzania.“Falsafa yangu kama
mfanyabiashara sio kuridhika na mafanikio niliyonayo bali kuendelea
kufanyakazi kwa bidii na kufanikiwa zaidi.” Alisema.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mohammed Dewji (Mb) (katikati)
akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Rand Merchant Bank
(RMB), Bw. Bruce Macfarlane (kulia). mara baada ya kutiliana saini mkopo
wa Bilioni 300 za Kitanzania.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mohammed Dewji (MB) akisoma risala yake
kwenye hafla ya utiliaji saini wa mkopo wa Bilioni 300 za kitanzania
kutoka Benki ya Rand Merchant ya Afrika Kusini (RMB) iliyofanyika kwenye
hoteli ya Saxon jijini Johannesburg Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment