Wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania na baadhi ya wateja
wakionyesha fataki kusheherekea Maadhimisho ya miaka 17 ya benki ambayo usheherekewa
kila Agosti 15. Hafla hiyo ilifanyika katika Tawi la kwanza kufunguliwa la benki hiyo la Samora
tawi, lililofunguliwa mwaka 1997.
Mkuu wa Idara ya Operesheni wa Benki ya Exim Tanzania, Eugene
Masawe (wa kwanza kulia) naMeneja Mwandamizi wa Tawi la Samora, Nancy Huggin (wa
kwanza kushoto) pamoja na wateja wa benki hiyo wakikata keki kusherehekea
Maadhimisho ya miaka 17 ya benki ambayo usheherekewa kila Agosti 15. Hafla hiyo
ilifanyika katika Tawi la kwanza
kufunguliwa la benki hiyo la Samora tawi, lililofunguliwa mwaka 1997. (Picha na
mpiga picha wetu).
Meneja Masoko Msaidizi wa Benki ya Exim Tanzania (wakwanza kulia) akizungumza wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 17 ya benki ambayo usheherekewa
kila Agosti 15. Hafla hiyo ilifanyika katika Tawi la kwanza kufunguliwa la benki hiyo la Samora
tawi, lililofunguliwa mwaka 1997
Mkuu wa Idara ya Operesheni wa Benki ya Exim Tanzania, Eugen
Masawe (Aliyenyanyua mikono) akizungumza wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 17 ya benki ambayo usheherekewa
kila Agosti 15. Hafla hiyo ilifanyika katika Tawi la kwanza kufunguliwa la benki hiyo la Samora
tawi, lililofunguliwa mwaka 1997.
Baadhi ya wafanyakazi wakongwe wa Benki ya Exim Tanzania katika picha ya pamoja iliyopigwa wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 17 ya benki ambayo usheherekewa
kila Agosti 15. Hafla hiyo ilifanyika katika Tawi la kwanza kufunguliwa la benki hiyo la Samora
tawi, lililofunguliwa mwaka 1997.
IKIJIKITA katika safari yake
tangu mwaka 1997 ikiwa na tawi moja na kupanua wigo wake mpaka matawi 27 nchini
na nje ya nchi, Benki ya Exim imepiga hatua ya kipekee katika sekta ya kibenki
nchini Tanzania. Ikidhiirishwa na miaka 17 ya historia ya Benki
iliposheherekewa Ijumaa Agosti tarehe 15 na wafanyakazi wa benki pamoja na
wateja nchi nzima.
Benki ya Exim imekuwa na mpango
kazi madhubuti wa 'upanuzi na ugunduzi' tangu kuanzishwa kwake kama benki ya
kitanzani, mali zake kwa jumla zikiwazimevuka shilingi tilioni moja ilipofika
mwezi Juni 2013. Bw. Eugene Masawe, Mkuu
wa Idara ya Uendeshaji na mmoja wa wafanyakazi wa muda mrefu alisema;
"maadhimisho ya miaka 17 ya benki yanaashiria mafanikio makubwa kwa miaka
mingi, yaliyodhiirishwa na utendaji wake mzuri wa kuwa na dhamira ya kuwa
"benki bora zaidi ya wengine".
Maadhimisho ya
miaka 17 ya benki ya Exim hayaonyeshi tu mafanikio yaliyopatikana katika miaka
hiyo lakini pia uongeza hari ya utendaji mzuri kwa wafanyakazi wote. Wakati
faida ghafi ya benki ikikua kwa asilimia 80 (shilingi bilioni 9.6), pato la
jumla litokanalo na riba likikua asilimia 36 (shilingi bilioni 14.3) na pato
kupitia biashara ya fedha za kigeni liliongezeka kwa asilimia 33 kuanzia mwaka jana ni viashirio
thabiti kwamba benki hiyo itafikia malengo katika miaka michache ijayo.
Utendaji huo wenye
mafanikio wa Benki ya Exim umetokana jitihada za benki hiyo kutoa huduma za
kipekee zikiungwa mkono na wafanyakazi mahiri pamoja na wateja waaminifu na
kuifanya benki kuwa ya kwanza katika Huduma kwa Wateja (Customer Care) nchini
Tanzania mwaka 2012 (Ripoti ya KPMG).
Ikiwa na zinazomlenga mteja za
rejareja, mikopo mbali mbali na kuanzisha huduma za kibenki za kisasa vimekuwa
na umuhimu mkubwa kwa kuendana na kauli
mbiu ya benki ya, 'ugunduzi ni maisha.’
Naye Nancy Huggin,
Meneja Mwandamizi wa tawi la Samora akasema, "sasa tumejikita katika
mpango wa kibunifunifu ujulikanao kama innovative retail model utakao tusaidia
kuboresha mawasiliano na wateja na uratibu wa matawi katika maeneo tunayofanyia
kazi."
Kwa upande wake,
Issa Hamisi, kaimu Afisa wa Fedha Mkuu aliongeza; “kipaumbele chetu kikubwa
kinabaki kuendelea kuimarisha nafasi yetu katika soko na kuboresha ufikiwaji wa
matakwa ya mteja kupitia utendaji ulio na ufanisi.”
Katika siku hiyo maalum, Benki
ya Exim iliwaalika baadhi ya wateja wake kusherehekea maadhimisho hayo katika
matawi yote nchini Tanzania kwa wafanyakazi wa jijini Dar es Salaam
wakisheherekea katika Tawi la Samora ambapo Benki ya Exim ilizaliwa.
Wakati wa tukio hilo la
kukumbukwa, Bw. Masawe aliongeza na kusema, "Baada ya kumaliza miaka 17 ya
shughuli zenye mafanikio Tanzania, tutaendelea kusimama imara, na kuendelea na
kuwa na mpango wa ukuaji tukijikita
zaidi na utoaji wa huduma zenye ubora zaidi na vile vile bidhaa na huduma zilizo
na ubunifu zaidi."
No comments:
Post a Comment