Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya
Ilala, Bw. Stima Kabikile (katikati) akimkaribisha rasmi Waziri wa Fedha, Mhe.
Saada Mkuya (kulia) wakati alipofanya ziara yake ya siku moja katika Manispaa
za Ilala, Kinondoni na Temeke kwaajili ya kupata taarifa kuhusu kodi za majengo
na utendaji kazi wa wataalam wanaoshughulikia masuala hayo na mbinu za
kuboresha namna ya ukusanyaji kodi hizo ili kuwarahisishia walipaji kodi.
Waziri wa Fedha, Bi Saada Mkuya
akiweka saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwaajili ya ziara yake ya siku moja ndani ya
jiji la Dar es salaam kwaajili ya kupata taarifa kuhusu kodi za majengo na
utendaji kazi wa wataalam wanaoshughulikia masuala hayo na mbinu za kuboresha
namna ya ukusanyaji kodi hizo ili kuwarahisishia walipaji kodi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa ya (kulia) Ilala akimsomea taarifa ya makusanyo ya kodi za majengo na
mikakati yake ya kufikia malengo waliojipangia ili kuongeza mapato Mhe.
Waziri wa Fedha Bi. Saada Mkuya wakati wa ziara ya siku moja katika Manispaa za
Ilala, Temeke na Kinondoni.
Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya
akipitia moja ya taarifa alizopewa na uongozi wa Halmashauri wilaya ya Kiondoni
wakati alipofanya ziara yake ya siku moja ofisi hapo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni
Mwandisi Mussa Natty (kulia) akimpokea Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya
(kushoto) wakati alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi ya Manispaa hiyo jana
kwaajili ya kupata taarifa mbalimbali kuhusu makusanyo ya kodi za majengo
pamoja kupeana mikakati mizuri ya kuboresha mifumo ya ukusanyaji kodi hizo ili
kuwarahisishia kazi walipaji kodi ambao ni wananchi.
Mtathmini
wa Manispaa ya Temeke Bw. Victor Ndonne (kushoto) akimuonyesha nyaraka za
makusanyo ya kodi za majengo Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (aliyekaa
katikati) wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja katika Manispaa hiyo.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria
mkutano huo wakisikiliza maelezo mazuri toka kwa Waziri wa Fedha kuhusu namna
ya kuboresha makusanyo ya kodi za majengo kwa kujikita na matumizi ya TEHAMA
katika ukusanayaji wa kodi hizo kama njia rahisi ya kuwarahisishia walipaji
kodi.
Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya
(kulia) akiongozana na viongozi wa Manispaa ya Kinondoni wakati alipofanya
ziara ya kikazi katika ofisi ya Manispaa hiyo jana kwaajili ya kupata taarifa
mbalimbali kuhusu makusanyo ya kodi za majengo pamoja kupeana mikakati mizuri
ya kuboresha mifumo ya ukusanyaji kodi hizo ili kuwarahisishia kazi walipaji
kodi ambao ni wananchi. katikati ni Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Bw. Yusuph
Mwenda na kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mwandisi Mussa Natty.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Temeke Bw. Photidas Kagimbo (kulia) akisalimiana na Waziri
waFedha, Mhe. Saada Mkuya (kushoto) mara alipowasili katika ofisi za Manispaa
hiyo kwa ziara ya kikazi katika jana kwaajili ya kupata taarifa mbalimbali
kuhusu makusanyo zikiwemo njia wanazotumia kukusanya kodi za majengo pamoja
kupeana mikakati mizuri ya kuboresha mifumo ya ukusanyaji kodi hizo ili kuwarahisishia
kazi walipaji kodi ambao ni wananchi.
|
Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya (kulia)
akihutubia mkutano huku akisisitiza juu ya kujikita zaidi katika kutumia TEHAMA
katika kukusanya kodi za majengo kama njia rahisi inayomrahisishia mlipaji kodi
kuweza kulipa kodi zake katika vituo vya huduma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya
(kushoto) akiweka saini katika kitabu cha wageni mara alipowasili ofisi za
Manispaa ya Kinondoni kwaajili ya ziara ya kikazi jana kwaajili ya kupata
taarifa mbalimbali kuhusu makusanyo ya kodi za majengo pamoja kupeana mikakati
mizuri ya kuboresha mifumo ya ukusanyaji kodi hizo ili kuwarahisishia kazi
walipaji kodi ambao ni wananchi. Kulia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Kinondoni Bw. Yusuph Mwenda.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni
Bw. Yusuph Mwenda (kulia) akitoa maelezo yake kwa Waziri wa Fedha, Mhe. Saada
Mkuya (kushoto) wakati wa mkutano na viongzoi wa Manispaa ya Kinondoni jana
jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya akitoa hotuba fupi yenye kuwaelekeza viongozi wa
Manispaa ya Kinondoni huku akiwasisitizia kutumia mifumo ya TEHAMA katika kuleta
ufanisi ukusanyaji kodi kama njia rahisi inayowasaidia walipaji kodi kutopata
usumbufu wakati wa ulipaji.
Wajumbe
kutoka Manispaa ya Temeke wakisikiliza kwa makini maelezo yakiyotolewa na
Mkurugenzi wao (hayupo pichani) kuhusu taarifa aliyokuwa akiwasilisha jana
katika Manispaa hiyo.
No comments:
Post a Comment