Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akizungumza na uongozi wa
polisi Mkoa wa Pwani na Wilaya ya Kipolisi ya Chalinze pamoja na
wananchi waliojitokeza katika hafla ya makabidhiano ya vifaa mbalimbali
kwa jeshi hilo zikiwemo kompyuta, mifuko ya Saruji pamoja na fedha
vilivyotolewa na mbunge huyo, Kwa ajili ya kutatua matatizo mbalimbali
yanayolikabili jeshi la polisi katika utekelezaji wa majukumu yake ya
ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
Pamoja
na kukabidhi kompyuta hizo zitakazosaidia katika utunzaji wa
kumbukumbu, pia mbunge huyo ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo
vya polisi vya Mbwewe na Kiwangwa ambavyo thamani inafikia zaidi ya
shilingi milioni 11, Kushoto kwake ni Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani
ACP Ulrich Onesphory Matei.Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika jana
kwenye kituo kikuu cha polisi Chalinze.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete kompyuta Kamanda wa polisi
mkoa wa Pwani Kamanda ACP Ulrich Onesphory Matei zilizokabidhiwa na
mbunge huyo kwa ajili ya kuboresha shughuli za jeshi hilo jimbo la
Chalinze katikati ni Mkuu wa kituo cha polisi Chalinze Afande J. S.
Magomi.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akikata utepe kufungua ili
kuonyesha kompyuta hizo huku viongozi wa jeshi hilo mkoani Pwani na
jimbo la Chalinze wakishiriki shghuli hiyo.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimuonyesha moja ya
kompyuta Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ACP Ulrich Onesphory Matei.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimsikiliza Kamanda wa
polisi mkoa wa Pwani ACP Ulrich Onesphory Matei wakati alipokuwa akitoa
shukurani zake kwa niaba ya jeshi la polisi mkoani Pwani mara baada ya
kukabidhiwa kompyuta hizo , katikati ni mkuu wa ituo cha polisi cha
Chalinze Afande J.S Magomi.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimsikiliza Mwalimu mkuu wa
shule ya msingi ya Chalinze Mzee Bw. Kamis Kameza wakati alipokuwa
akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa shule hiyo ambayo inajengwa na jeshi la
kujenga taifa JKT kambi ya Ruvu.
Baadhi ya wanajeshi wa kambi ya JKT Ruvu wanaoshiriki katika ujenzi wa shule hiyo.
Moja ya madarasa ya shule hiyo ambayo yako katika hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi wake.
Baadhi ya madarasa na maktaba ya shule hiyo yakiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi wake.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na wanafunzi wa
darasa la saba wa shule ya msingi ya Chalinze Mzee wakati alipokagua
ujenzi wa shule hiyo.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akiendelea kufanya ukaguzi
wa ujenzi shuleni hapo kushoto ni Diwania wa kata ya Bwilingu Chalinze
Bw. Ahmed Nasser.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikweteakikagua ujenzi wa Maktaba ya
shule hiyo akiwa ameongozana na Diwani wa kata ya Bwilingu Ahmed Nasser
mbele na Mwalimu mkuu wa shule hiyo Khamis Kameza.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria wakati wa hafla kukabidhi kompyuta kituo cha polisi Chalinze.
Diwani
wa kata ya Bwilingu Chalinze Bw. Ahmed Nasser akizungumza wakati mbune
wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete alipolokabidhi jeshi la
polisi kompyuta kwa ajili ya kuboresha shughuli za jeshi hilo..(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-CHALINZE)
No comments:
Post a Comment