Monday, June 9, 2014

MBUNGE JOSHUA NASSARI ALIVYOMEREMETA KUELEKEA UWANJA WA USA-RIVER ACADEMY

Bw Harusi ,Joshua Nassari na Bi Harusi Anande Nnko wakapanda usafiri mwingine tofauti na ule waliofika nao katika Hotel ya Ngurdoto na safari hii ni kuelekea uwanja wa User-River kwa ajili ya sherehe.
Msafara ukaanza safari yake kutoka Ngurdoto huku njiani madereva wa Boda boda wakiwa wamezunguka gari la Maharusi na wengine wakionesha mbwembwe.
Baada ya mwendo kido Maasai nao wakaomba msafara wa pikipiki ukae pembeni wakidai ni zamu yao sasa kusindikiza Maharusi.
Huko uwanjani MC ,Masanja Mkandamizaji na Salum Mwalimu walikuwa bize kuweka mambo sawa.
Wageni mbalimbali walikuwepo uwanjani hapo wakingojea Maharausi miongoni mwao ni wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Kwa kuwa sherehe yenyewe haikuwa na kadi kila mmoja alialikwa na ili kuhakikisha watu wote wanashuhudia kinachoendelea Screen kubwa zilifungwa kila kona ili kuhakikisha wote wanafaidi matukio mbalimbali.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.

No comments: