Na Francis Godwin Blog KAMPUNI ya maziwa ya Asas Dairies Ltd ya mkoani Iringa kwa mara ya pili mfululizo imefanikiwa kuongoza kwa ubora wa uzalishaji wa maziwa baada ya kukabidhiwa tuzo ya mshindi wa kwanza kwa viwanda vya maziwa bora nchini Tanzania kwa kuzibwaga vibaya kampuni 30 zilizoshiriki.
Asas Dairies Ltd yenye makao yake makuu mkoani Iringa imekabidhiwa tuzo ya ushindi wa kwanza kwa mwaka 2014 katika viwanda bora vya maziwa katika maonyesho ya wiki ya maziwa yaliyofanyika mkoani Mara ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr. Titus Kamani.
Akiipongeza kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd kwa kuendelea kufanya vizuri katika mashindano hayo ya ubora wa maziwa nchini ,waziri Dr Kamani alisema kuwa jitihada zilizoonyeshwa na kampuni hiyo ni kubwa na zinapaswa kuigwa na makampuni mengine hapa nchini.
Kwani alisema kuwa kuongoza katika nafasi zote zilizoshindaniwa na jambo dogo ni jitihada kubwa zimefanyika na ni hatua ya kujivunia kwa kampuni hiyo.
Pia alisema kwa aliipongeza bodi ya maziwa Tanzania kwa kuandaa mashindano kama hayo kwani ni sehemu ya kipimo kwa wamiliki wa viwanda vya maziwa nchini kujitathimini .
Kwa upande wake afisa masoko wa kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd Jimmy Kiwelu alisema kuwa mbali ya kampuni hiyo kuongoza kwa mwaka huu bado ilipata kuongoza katika mashinadano kama haya yaliyofanyika mwaka jana mkoani Ruvuma na kuwa lengo la kampuni ni kuendelea kuongoza daima
Katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na bodi ya maziwa Tanzania( TDB) jumla ya makampuni 30 yalishiriki ikiwemo kampuni ya Tanga fresh,Musoma Dairies,Kilimanjaro creamer,Engingten,Arusha,Ammy Dairies Njombe cefa,Victoria dairies ,Uvingo dairies na mengine mengi kampuni ya Asas Dairies iliweza kuibuka na ushindi wa jumla baada ya kushinda tuzo zote tatu zilizokuwa zikishindaniwa na hivyo kufanikiwa kuondoka na tuzo nne zote ikiwemo ya mshindi wa jumla.
Kiwelu aliwataka watanzania kuendelea kuzipenda bidhaa za Asas Dairies Ltd kutokana na kuendelea kuongoza katika ubora na kuwa lengo la kampuni hiyo ni kuona ubora huo unaendelea zaidi na kila mwaka kuendelea kufanya vema.
Pia alipongeza watanzania na watumiaji wa bidhaa za Asas Dairies Ltd kutokana na ushirikiano mkubwa wanaoutoa kwa kuendelea kutumia maziwa yanayozalishwa na kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd Iringa. |
No comments:
Post a Comment