Sunday, June 8, 2014

Kuagwa na mazishi ya Marehemu Lt. Col. Mstaafu Maurice Noel Singano

 Marehemu Lt. Col. Mstaafu Maurice Noel Singano enzi ya uhai wake.
 Mwili wa Marehemu Luteni Kanali mstaafu, Maurice Noel Singano ukiwasili nyumbani kwa mtoto wake Mikocheni B jijini Dar es Salaam Alhamisi Juni 05.2014, kabla ya kusafirishwa kwenda mkoani Tanga kwa mazishi yaliyofanyika Ijumaa Juni 06.2014. Marehemu Mzee Singano alifariki Mei 31, mwaka huu huko katika Hospitali ya Apollo Chennai nchini India alikuwa akipatiwa matibabu baada ya kupata mshtuko.

 Mwili wa Marehemu Luteni Kanali mstaafu, Maurice Noel Singano ukiwasili nyumbani kwa mtoto wake Mikocheni B jijini Dar es Salaam Alhamisi Juni 05.2014, kabla ya kusafirishwa kwenda mkoani Tanga kwa mazishi yaliyofanyika Ijumaa Juni 06.2014. Marehemu Mzee Singano alifariki Mei 31, mwaka huu huko katika Hospitali ya Apollo Chennai nchini India alikuwa akipatiwa matibabu baada ya kupata mshtuko.
 Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu wakati wa kuuaga Mikocheni B jijini Dar.


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. John Haule akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu wakati wa kuuaga Mikocheni B jijini Dar.
 Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha siasa cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu wakati wa kuuaga Mikocheni B jijini Dar.
 Dada za Marehemu wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu wakati wa kuuaga Mikocheni B jijini Dar.

Maafisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kikosi cha 37 Tanga, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu wakati wa kuuaga nyumbani kwa
 Mjane wa Marehemu, Bi. Maria Singano akilia kwa uchungu wakati akiuaga mwili wa mpendwa  mume wake, nyumbani kwao katika eneo la Sahare mkoani Tanga.
Mtoto wa Marehemu, ambaye ni Mkuu wa Mahusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Bi. Beatrice Singano akilia kwa uchungu wakati akiuaga mwili wa mpendwa baba yake, nyumbani kwao katika eneo la Sahare mkoani Tanga.



Beatrice Singano akilia kwa uchungu
 Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim akiwa na wafiwa alipokwenda kuhani msiba Mikocheni B jijini Dar.
 Jeneza lenye mwili wa marehemu likiingizwa katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Martha lililopo Mikocheni B jijini Dar, kwa ajili ya misa kabla ya kuanza safari ya kuelekea Tanga kwa mazishi.
 Jeneza lenye mwili wa Marehemu, likiwa lemebebwa na askari wa JWTZ Kikosi cha 37, likitolewa nyumbani katika eneo la Sahare mkoani Tanga kwaajili ya kwenda kanisani na baadaye mazishi katika makaburi ya Bombo mkoani humo. Aliyeshika Msalaba ni mototo wa Marehemu, Bw. Billy Singano
 Jeneza lenye mwili wa Marehemu, likiwa lemebebwa na askari wa JWTZ Kikosi cha 37, likiwasili katika Kanisa Katoliki la Mt. Mathias mjini Tanga kwaajili ya misa kabla ya mazishi.
 Padri wa Kanisa Katoliki la Mt. Mathias mjini Tanga akifanya sala kwa marehemu.
 Wakati wa misa
 Jeneza lenye mwili wa Marehemu, likiwa lemebebwa na askari wa JWTZ Kikosi cha 37, likiwasili katika makaburi ya Bombo mjini Tanga kwaajili ya mazishi.
 Shughuli za mazishi zikiendelea.
 Mjane wa marehemu akiweka shada lake la maua kaburini
 Watoto wa marehemu wakiweka shada lao
 Beatrice na mumewe wakiweka shada la maua
 Askari wa JWTZ  37KJ wakifanya mazishi ya kijeshi, ikiwa ni pamoja na kupiga risasi kadhaa hewani.

No comments: