Wednesday, May 21, 2014

WILAYA YA HANDENI NA MAENDELEO YA KILIMO NA UFUGAJI

 Mmoja ya wakulima wa Mahindi Wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Adalbertus Bubelwa wa pili kutoka kushoto akimwelezea Mkuu wa wilaya ya handeni Bw. Muhingo Rweyemamu, jinsi alivyoandaa shamba lake. Mkuu huyo wa wilaya alikuwa katika ziara ya kuwatembelea wakulima katika vijiji mbalimbali wilayani humo kuangalia mazao mashambani.
 Mkuu wa wilaya ya Handeni Bw. Muhingo Rweyemamu, kushoto ambaye ni mwenye shamba akipata maelekezo kutoka kwa Afisa Kilimo wa Wilaya hiyo Bw. Yibarik Chiza, aliyemtembelea Mkuu huyo wa wilaya shambani kwake. 
 Mkuu wa wilaya ya Handeni Bw. Mhungo Rweyemamu akiwa ofisini kwake wilayani humo.
 Mkuu wa wilaya ya handeni Bw. Muhingo Rweyemamu, akisalimiana na mmoja wa wananchi alipotembelea katika kijiji cha Kang'anta kuangalia maendeleo ya mnada wa mifugo na mazao ya chakula na biashara.
 Mkuu wa wialya ya Handeni Bw. Muhingo Rweyemamu, kulia akipokea fimbo mbili zilizotengenezwa kwa mpingo kutokaka kwa Mzee Adam Hassan Mtii wa Kijiji cha Mbagwi kilichopo kata ya Misima wilayani humo. Mzee Mtili ameagiza moja ya fimbo hizo apelekewe Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk. Jakaya Kikwete.
 Mmoja wa wakulima wa nanasi wilayani Handeni Bi Sabrina Rory Sasumua, akionyesha aina ya nanasi lenye uzito wa kilo mbini na nusu kutoka katika shambani lake eneo la Kwamsisi wilayani Handeni.

 Afisa Kilimo wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Yibarik Chiza, kulia akiwaelekeza jambo wakulima wa zao la ufuta wa Kijiji cha Misima wilayani humo.

 Baadhi ya akina mama wa eneo la Soni katika wilaya ya Lushoto mkoani Tanga wakifanya biashara za matunda na mbogamboga. 
 Mkuu wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga Bw. Muhingo Rweyemamu, kulia akishika mmoja ya mihindi katika shamba linalomilikiwa kwa pamoja na Bw. Adolf Mpanju na Bw. Stanslaus Majura, wakati wa ziara yake ya kuangalia mazao mashamabani katika kijiji cha Manga wilayani Handeni.
 Shamba la mahindi katika kijiji cha Manga likionekana kustawi vya kutosha.
 Ufugaji wa kuku wa kisasa katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga ni moja ya shughuli zinazowapatia wananchi fadhe za ziada.
 Mmoja ya wakulima wakubwa wilayani Handeni Bw. Rory Nightingale, katikati akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga Bw. Muhingo Rweyemamu kulia alipotembelea katika shamba hilo akiongozana na  Afisa Kilimo wa wilaya ya Handeni Bw. Yibarik Chiza kuona ana ya mananasi katika shama hilo lililopo katika eneo la Kwamsisi wilayani humo.
 Afisa Kilimo wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Yibarik Chiza, kulia akiwaelekeza jambo wakulima wa zao la ufuta wa Kijiji cha Misima wilayani humo.
 Mmoja wa Wakulima wa Ufuta katika Kijiji cha Misima wilayani Handeni Bw. Rashidi Dempombe, akimweleza afisa Kilimo wa wilaya hiyo Bw. Yibarik Chiza, kwa namna alivyolima na kupanda zao hilo ambalo ni la biashara.
 Mkuu wa wialya ya Handeni Muhingo Rweyemamu (katikati) akikagua shamba la shule ya sekondari Magamba wilayani humo kuangalia utekelezaji wa maagizo ya kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya iliyotaka kila shule kuwa na shamba darasa.
 Mkuu wa wialya ya Handeni Muhingo Rweyemamu (kushoto) akisalimiana na mmoja wa walimu shuleni hapo wakati wa ziara yake.
 Mkuu wa wialya ya Handeni Muhingo Rweyemamu akihudumia mifugo yake baada ya saa za kazi.
 Mkuu wa wilaya ya Handeni Muhingo Rweyemamu (wapili kushoto) akitoa maelekezo kwa walimu wa shule ya sekondari Magamba.
 Sehemu ya mashamba ya mahindi katika maeneo mbalimbali wilayani Handeni.
 Sehemu ya mashamba ya mahindi katika maeneo mbalimbali wilayani Handeni.
 Mkuu wa Wilaya Handeni Muhingo Rweyemamu akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake ya kutembelea mashamba ya mazao mbalimbali wilayani humo.
Katibu tawala wilaya ya Handeni Bw. John Ticky akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mwandishi wa habari ofisini kwake. 
Picha Zote na Mohammed Mhina

No comments: