Msimamizi wa Mauzo katika duka la Vodacom Tanzania Mlimani City,Salim Salmin(kushoto)akielezea mifumo mbalimbali iliyopo kwenye simu aina ya Vodafone 875 yenye mfumo Adroid inayopatika sasa kwa bei ya shilingi 100, 000/- katika maduka yote ya kampuni hiyo. Simu hiyo ni ya kisasa iliyounganishwa na 3G mteja anaweza kuperuzi mitandao ya Facebook, Whatsap, Twitter, Viber, na Instagram.Pamoja naye ni mfanyakazi wa duka hilo Jihan Dimachck.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (kushoto)akionesha moja ya simu aina ya Vodafone 875 yenye mfumo Adroid inayopatika sasa kwa bei ya shilingi 100, 000/- katika maduka yote ya kampuni hiyo. Simu hiyo ni ya kisasa iliyounganishwa na 3G mteja anaweza kuperuzi mitandao ya Facebook, Whatsap, Twitter, Viber, na Instagram.Pamoja naye ni Mkuu wa Idara ya bidhaa kwa wateja wa Vodacom Tanzania Samson Mwongela.
Wakati dunia ikishuhudia mapinduzi ya kiteknolojia na sayansi bado nchi za bara la Afrika zinasuasua, Afrika ya Kusini ndiyo nchi ya pekee inayokwenda sambamba kimaendeleo kwenye sekta hiyo sawa na nchi za Ulaya na Marekani.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kuhusu idadi ya watumiaji wa simu za mkononi na intaneti kwa Afrika ya Mashariki mwaka 2013 na mtandao wa WhiteAfrican tawkimu zinaonyesha kwamba, Kenya inayoongoza kwa maendeleo ya mawasiliano ya simu na intaneti kwa nchi za kusini mwa jangwa la sahara ikifuatiwa na Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi.
Kenya inawakazi 44, 037,656 kwa takwimu za mwezi wa Julai mwaka 2013 ambapo watumiaji wa simu za mkononi ni 30,429,351 na intaneti ni 16,236,583 sawa na asilimia 41. Tanzania inafuatia kwa kuwa na wakazi 48,261,942 kwa takwimu za mwezi wa Julai mwaka 2013 ambapo watumiaji wa simu za mkononi ni 27,395,650 na intaneti ni 5,308,814 sawa na asilimia 11 tu.
Hivyo basi kutokana na takwimu hizo zinahitajika jitihada za ziada zifanyike ili kuweza kuziba pengo hilo la majirani zetu ili kenda sawa na kasi ya maendeleo ya ukuaji wa teknlojia ya habari na mawasiliano duniani.
Zipo changamoto nyingi ambazo zinasababisha maendeleo duni katika matumizi ya intaneti barani Afrika zikiwemo; watu wengi kuwa na uelewa mdogo wa kompyuta, miundombinu duni na gharama kubwa za matumizi ya intaneti.
kampuni ya mawasiliano ya simu ya Vodacom Tanzania imekuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha watanzania hawaachwi nyuma na maendeleo hayo ambapo wanatoa simu za kisasa za smartphones kwa bei nafuu kabisa.
Akizungumzia juu ya ofa hiyo Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa amesema kuwa wameamua kuja na smartphone hizo ili kuchochea matumizi ya intaneti nchini ambayo yanakuwa kwa kasi duniani kote.
“Simu hii aina ya Vodafone 875 yenye mfumo Adroid inapatika kwa bei ya shilingi 100, 000/- taslimu katika maduka yote ya Vodacom. Simu hiyo ya kisasa imeunganishwa na 3G na inampatia mteja uwezo wa kuperuzi mitandao ya Facebook, Whatsap, Twitter, Viber, Instagram na mingineyo.” Alisema Twissa
Twissa alimalizia kwa kusema “Mbali na uwezo wa simu hiyo inayopatikana kwa bei nafuu pia pindi mteja anunuapo simu hiyo atapatiwa MB 500 na SMS 200 bure kwa kila mwezi ndani ya miezi sita mfululizo. Ili kupata ofa hiyo mteja atatakiwa kutuma neno CIMEI kisha kuacha nafasi ikifuatiwa na namba ya CIMEI ya simu kwenda namba 15300.”
Matumizi ya intaneti yamekuwa siyo anasa tena kama ilivyokuwa ikichukuliwa na wengi hapo awali ambapo watu hujiunga kwa ajili ya kuwasiliana na watu walio nje ya nchi au kwa burudani nyinginezo. Hivi sasa kwa uwezo wa intaneti umekuwa kutoka watu kuwasilaina mpaka kwa matumizi ya biashara ambapo watu wa mataifa mbali mbali hukutana mtandaoni kuuza ama kununua bidhaa na huduma.
Kampuni hiyo inayoongoza kwa mawasiliano ya simu za mkononi nchini yenye wateja zaidi ya milioni 10 inaamini kwamba inayo nafasi kubwa ya kuwashawishi wateja wake kukumbatia matumizi ya intaneti kupitia mtandao wake wenye kasi, kuaminika na gharama nafuu. Kwa kuuza simu hizo inampa kila mtanzania uwezo wa kumiliki simu za kisasa na zinazoendana na dunia ya leo.
Wateja wote wa Vodacom na wananchi kwa ujumla wanashauriwa kutembelea maduka yote ya kampuni hiyo yaliyotapakaa kila kona nchini ama kwenye magari yake ya promosheni ili kuweza kujipatia simu hizo.
No comments:
Post a Comment