Thursday, March 8, 2018

NIDA KUZINDUA USAJILI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA KIGOMA, RUKWA NA KATAVI

Kaimu Ofisa Uhusiano Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Rose Joseph akielezea mikakati ya kuzindua usajili wa vitambulisho Kigoma, Rukwa na Katavi sambamba na ndani ya mgodi wa Tanzanite.

MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA)  inatarajia kuzindua usajili na utoaji wa  vitambulisho hivyo katika mikoa mitatu ya Katavi, Kigoma na Rukwa.

Pia  NIDA  kwa kushirikiana na  Wizara ya Madini , imeanza  kuwasajili watu wote watakaoishi, kufanya kazi au biashara ndani ya eneo lililozungushiwa ukuta lenye madini ya TANZANITE huko Mererani mkoani Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, leo, Kaimu Ofisa Uhusiano  wa NIDA,  Rose Joseph, alisema   mpaka sasa mamlaka hiyo imaendelea  na  usajili na utoaji vitambulisho vya  uraia  katika mikoa 20.

“Hivi karibuni tutafanya uzinduzi katika mikoa mitatu iliyobaki ambayo ni Kigoma,  Rukwa na Katavi . Wananchi katika mikoa hii watakuwa na muda wa miezi mitatu wa kujisajili,  na hivyo  tutakuwa  tumeifikia nchi nzima,”alisema Rose.Ofisa huyo alisema  pia NIDA taangu Novemba   mwaka uliopita  ilianza  usajili wa mkupuo katika mikoa mbalimbali   na muda ulikuwa ukiongezwa  kadri ilivyokuwa uinaruhusu.

“Tayari baadhi ya mikoa imemaliza kazi ya kusajili  kwa mkupuo ikiwemo mikoa ya Mara na Iringa,”.alieleza  Rose.Alisema  katika kazi hiyo ya usajili NIDA kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji  wanapeleka  maofisa hadi  ngazi ya kata na vijiji,  ili  kuhakikisha  kazi hiyo inakwenda kwa mchujo sahihi na wale wote wanaosajiliwa wawe na sifa  na vigezo kuwa raia  wa Tanzania. “Tunasajili  vitambulisho vya aina tatu ambavyo ni vya uraia, mkimbizi na mgeni na kumekuwa na ufanisi mkubwa,”alifafanua ofisa  uhusiano huyo.

Alisema, pia NIDA kwa kushirikiana na  Wizara ya Madini, imeanza usajili na kutoa vitambulisho kwa wafanyabiashara, wakazi na watu wote watakao kuwa wakiendesha shughuli zao ndani ya ukuta wa madini ya TANZANITE huko Mererani.“Kila mtu atasajiliwa na kupewa kitambulisho  cha taifa. Hakuta kuwa na ruhusa ya mtu kuingia na kufanya  shughuli yoyote  ndani ya ukuta huo  bila kuwa na kitambulisho hiki,”alibainisha Rose.

Alisema lengo ni  kuona kuna kuwa na utaratibu maalumu wa kulitumia eneo hilo pamoja na kuwatambua wachimbaji wote wadogo na wakubwa na wafanyabishara wa madini katika eneo hilo.“Lengo ni kutambua watu wanaonufaika na shughuli zozote katika eneo hilo la madini. Tunataka kuona vijana wa Tanzania ndiyo wanufaika wakubwa , hivyo kutoa vitambulisho kutadhibiti wageni kuvamia eneo hilo,”alisema Rose.

Pamoja na hayo, Rose libainisha kuwa NIDA,  kwa kushirikiana na  wakala wa Usajili wa Makampuni (BRELA) kwa sasa wanaendelea na usajili na kuwapa vitambulisho vya uraia  watu wote waliofungua makampuni kupitia wakala huo.“Utaratibu uliopo hivi sasa ni kwamba mtu yoyote ambaye hana kitambulisho taifa hawezi kupata usajili wa kampuni BRELA. Ni marufuku na wale ambao tayari walifungua wanatakiwa kufika BRELA kuchukua vitambulisho hivyo katika madawati yetu,”alifafanua ofisa huyo.

Aliongeza; “Changamoto  kubwa tuliyonayo watanzania  tunapenda njia za mkato, lakini katika kazi hii  ni lazima tuwe wakweli , kwani kuwa na kitambulisho cha taifa  kunakupa hadhi ya utanzania,”Alisema  watu wengi wanataka  kusajili kampuni kwa haraka hivyo kupita nijia za mkato  kisha kukwama katika hatua za mwisho.

“Zoezi lingine  ambalo NIDA tunalitekeleza ni la kuwasiliji wananchi wanaotaka  Paspoti  na hati za kusafiria za kielektroniki.Kwa sasa hupati hati hizo bila kuwa na kitambulisho cha taifa,”alisema Rose.Alisema kuna huduma za haraka zinazowawezesha wananchi wasio na vitambulisho hivyo wanaohitaji hati za kusafiria.

“Pia  tunaendelea  na usajili wa wanachama wa mifuko yote ya hifadhi ya jamii Tanzania ambapo kwa kushirikiana na  Mamlaka  Udhibitiwa Mifuko  hiyo (SSRA), kusajili wanachama wote wa mifuko hiyo ambao hawana  vitambulisho,’ alisema.

No comments: