Monday, May 26, 2014

Mama Mwanamwema Shein akabidhi madawati kwa Skuli ya Msingi Mgenihaji Wilaya ya Kati Unguja

MWAKILISHI wa Jimbo la Uzini Unguja Mhe. Mahammed Raza, akitowa maelezo kwa Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, wakati wa kukuabidhi madawati kwa Skuli ya Msingi Mgenihaji Wilaya ya Kati Unguja.jumla ya madawati 100 na viti 100 vimekabidhiwa skuli hiyo jana.
MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi Madeski Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Mgenihaji Ndg.Ali Mohammed Nassor, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya skuli ya Mgenihaji kulia Mwakilishi wa Uzini Mhe. Mohammed Raza madawati hayo yametolewa na Ndg Abdulhamid Mohammed Ali Mhoma, kupitia kwa Mwakilishi wa Uzini Mhe Mohammed Raza.
WANAFUNZI wa Skuli ya Msingi ya Mgeni haji Wilaya ya Kati Unguja wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia katika hafla ya kukabidhi madawati kwa ajili ya skuli hiyo.
MWALIMU Fatma Suleiman, akisoma risala ya Wananchi wa Mgenihaji wakati wa hafla wa kukabidhi madawati yaliotolewa na Mhe Mohammed Raza kwa ajili ya Skuli ya Msingi ya Mgeni haji Wilaya ya Kati Unguja.
MKE wa Balozi wa Mdogo wa China Zanzibar Bi Wu Yan, akiwasalimia Wananchi na Wanafunzi wa Mgenihaji wakati wa hafla ya kukubidhi madawati na Vifaa mbalimbali kwa Wanawake wa Mgenihaji.
MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Uzini Unguja wakati wa hafla ya kukubidhi Vifaa kwa ajili ya Vikundi vya Ushirika na Madawati ya Skuli ya Msingi Mgenihaji, kulia Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt Idris Muslim Hija na kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif.
MWAKILISHI wa Jimbo la Uzini Mhe Mohammed Raza, akimkabidhi zawadi Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, wakati wa hafla ya kukabidhi madawati ya Skuli ya Msingi Mgenihaji Wilaya ya Kati Unguja.
MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi msaada wa fedha Kiongozi wa Kikundi cha Wanawake cha Hatukati Tamaa.Bi Siwa Khamis, shilingi laki tatu kwa ajili ya kukiendeleza kikundi chao.
MKE wa Raisc wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi Vyarahani Viwili, Nyuzi na Vitambaa. Kiongozi wa Kikundi cha Kasi Mpya.Ndg. Mwanaisha Mtumwa.
MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi Nahodha wa timu ya Hatuna Yawa ya Bambi ilichukuwa nafasi ya Pili ya michuano ya Kombe la Muungano lililofanyika viwanja vya bambi Wilaya ya Kati Unguja. Anayeshuhudia Mke wa Balozi Mdogo wa China Zanzibar Bi Wu Yan.(Picha na Othman Maulid

No comments: