Monday, May 26, 2014

KATIBU MKUU WA CCM,KINANA AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU NANE MKOANI SINGIDA,KESHO KUELEKEA MKOANI MANYARA

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia Wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Msange,kata ya Msange,Singida Vijijini mkoani Singida. Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikad,siasa na Uenezi Nape Nnauye,leo wanahitimisha siku nane za ziara yao ya Kukagua kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi ya serikali za mitaa,kusikiliza kero za wananchi na kuzitafututia ufumbuzi.Kinana na Msafara wake kesho unaelekea mkoani Manyara ambako ataendeleza ziara yake.
 Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia Wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Msange,kata ya Msange,Singida Vijijini mkoani Singida jioni ya leo. 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimdondoshea tone la chanjo ya Polio mtoto Erick Gabriel alipokwenda kukagua mradi wa Zahanati mpya ya Mkenge,Singida Vijini mkoani Singida jioni ya leo. 
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (wa tatu Pichani) akishiriki kuvuna Mtama katika shamba la Bwa.Khamis katika kijiji cha Mkenge,Singida Vijijini akiwa sambamba na Mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini ,ambaye pia Waziri wa Maliasili na Utalii,Mh.Lazaro  Nyalandu. 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kupembua Mtama kwa njia ya mashine,ambayo ndiyo njia ya kisasa inayoweza kurahisha kazi kwa mkulima,mashine hiyo ina uwezo wa kupembua magunia sita mpaka kumi kwa saa.kulia kwake ni Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi Nape Nnauye akishuhudia.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa sambamba na Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini,Mh.Lazaro Nyalandu wakishiriki ujenzi katika Kiwanda cha kusindika na kusafisha mafuta ya Alizeti,katika kijiji cha Mtinko,Singida Vijijini mkoani Singida jioni ya leo
Kinana akitoka kukagua mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha kusindika na kusafisha mafuta ya Alizeti,katika kijiji cha Mtinko,Singida Vijijini mkoani Singida jioni ya leo.









 











No comments: