Monday, May 19, 2014

MAFUNZO YA MAADILI NA KUANDIKA HABARI ZA JINSIA NA MIGOGORO YAFANYIKA MASASI, MKOANI MTWARA

SONY DSC
Mkurugenzi wa Fadhila FM Redio, Br. Edwin Mpokasye akiwakaribisha washiriki katika ufunguzi wa warsha ya Maadili na kuandika Habari za Jinsia na Migogoro kwa waandishi wa habari wa Redio za Jamii iliyofanyika Masasi mkoani Mtwara.
SONY DSC
Mkurugenzi wa Fadhila FM Redio, Br. Edwin Mpokasye akikabidhi risala aliyoitoa kwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi Farida Mgomi wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa warsha hiyo.
SONY DSC
Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO Bi. Rose Haji Mwalimu akitoa ufafanuzi kuhusu madhumuni ya warsha hiyo inayoendeshwa chini mradi wa Democratic Empowerment Project (DEP) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na kutekelezwa na UNESCO. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Bi. Farida Mgomi.
SONY DSC
Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Bi. Farida Mgomi, akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha ya Maadili na kuandika Habari za Jinsia na Migogoro kwa waandishi wa habari wa Redio za Jamii iliyofanyika Masasi mkoani Mtwara.
SONY DSC
Mshiriki wa warsha Hassan Hassan kutoka Kituo cha Redio Micheweni FM, Pemba, akiwasilisha kazi ya kikundi kazi.
SONY DSC
Pichani juu na chini ni washirki kutoka Redio Jamii za Micheweni, Mtegani, Zenji, Pangani na Fadhila waliohudhuria warsha ya siku 10 iliyofanyika kwenye kituo cha Redio Fadhila FM Masasi.
SONY DSC
SONY DSC
SONY DSC
Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu akiendesha mafunzo ya Jinsia kwa washiriki wa warsha ya Kuandika Habari za Migogoro Kimaadili kwa waandishi wa habari wa Redio za Jamii iliyofanyika Masasi mkoani Mtwara.
SONY DSC
Mshiriki kutoka Pangani FM Redio, Abdilhali Shukuran (kushoto-mwenye shati nyeupe), akichangia mada ya Jinsia na Uchaguzi wakati Mkufunzi wa mafunzo hayo Bi. Rose Haji Mwalimu akimsikiliza kwa makini.
SONY DSC
Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha pamoja na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Bi Farida Mgomi (wa pili kulia).

No comments: