Sunday, May 18, 2014

Ankal Shahada Ibrahim alamba Nondozz yake ya Ualimu

 Ankal wake na Ankal wa Libeneke la Globu ya Jamii, Bi. Shahada Ibrahim (wa tatu kulia) akiwa na Wahitimu wenzake wa Ualimu kwa ngazi ya Cheti wakirusha kwa pamoja kofia zao juu mara baada ya kula Nondozz zao katika Chuo ya Ualimu cha Mtakatifu Rock kilichopo Wilayani Korogwe,Mkoani Tanga,ikiwa ni mahafali ya Nane ya chuo hicho ambayo yalifanyika jana Mei 17,2014 Chuoni hapo.
Ankal Shahada Ibrahim akipozi na Wahitimu wenzake.
 Shahada Ibrahimu akiwa ni mwenye furaha tele baada ya kulamba Nondozz yake hiyo aliyoisotea kwa miaka mibeee...
 Shahada akipongezwa na Ankal wake Ismail Issa Michuzi.
 Ba'Mdogo Itami akimvalisha vizuri kofia Mhitimu Shahada.
 Mama Mkubwa wa Shahada Riziki akimpongeza kijana wake kwa kulamba Nondozz yake hiyo.
 Mama Mzazi wa Shahada, ambaye ni dada wa Ankal, akimpongeza mwanae huku wote wakiwa na furaha tele.
 Mama akiiweka sawa kofia ya Mwanae.Nani kama Mama??
 Mama Mkubwa Margerth akimpongeza Shahada.
 Dada Mwamvita na Shahada. 
Dada Amina akipiga konozz na Mdogo wake Kipenzi Shahada. 
 Keki ya pongenzi
 Dada Fatina akiwa kashika keki huku Shahada akiikata kwa utaratibu,tayari kwa kuwalisha ndugu jamaa na marafiki.
Kaka akisaidia zoezi la kukata keki.
 Picha za pamoja.

No comments: