Saturday, March 15, 2014

YANGA VS MTIBWA SUGAR HAKUNA MBABE

Na John Nditi, Morogoro 
 MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga , wameshindwa kutamba mbele ya vijana wa Mtibwa Sugar ya Manungu, Turiani,  baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika leo Machi 15, mwaka huu kwenye uwanja wa Jamhuri wa Mjini Morogoro. 
 Mtibwa Sugar diyo walikuwa wenyeji wa wa mchezo huo , ambao kwa Yanga ni wa kwanza tangu irejee kutoka Misri ilikotolewa katika raundi ya pili ya Ligi la Kombe la Mabingwa wa Afrika na timu ya Al Ahly . 
Hata hivyo Yanga wanaujutia mchezo huo baada ya kukosa mabao mengi hasa kipindi cha pili kutokana na washambuliaji wake kutokuwa makini kutokana na wachezaji karibu wote mabeki wa Mtibwa kurudi nyuma kulinga lango lao.
 BEKI WA TIMU YA SOKA YA MTIBWA SUGAR, 
PAUL NGALEMA AKIMDHIBITI MSHABULIAJI WA YANGA, SIMONI MSUVA.
 MASHABIKI WA YANGA WAKISHANGILIA TIMU YAO
 UWAJA WA JAMHURI WA MOROGORO
 Mchezaji wa Yanga , Didie Kavumbagu akijaribu kuwatoka 
Paul Ngalema ( kushoto) na Hassan Ramadhan 
 NAHODHA WA MTIBWA SUGAR, SHAABAN NDITI ( JEZI BLUU) PAMOJA NA MWEZAKE HAROUB CANAVARO WA YANGA WAKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA MWAAMUZI WA MCHEZO WAO LEO
 Kikosi cha Yanga
 Mashabiki
 Mshambuliaji hatari Emmanuel Okwi akiingia uwanjani kipimdi cha pili
 Kikosi cha Mtibwa Sugar
Beki wa Mtibwa Sugar , Paul Ngalema ( kulia) akimdhibiti Simon Msuva
 ( kushoto) wa Yanga kwenye mchezo wao leo
Picha zote na habari na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro

No comments: