Saturday, March 15, 2014

CCM YAHITIMISHA KAMPENI ZA KALENGA KWA KISHINDO, ROSE KAMILI ADAKWA KWA TUHUMA ZA KUGAWA PESA KWA WAPIGA KURA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimnadi mgombea wa ubunge jimbo la Kalenga kupitia CCM Ndugu Godfrey Mgimwa wakati wa mkutano wa mwisho wa kampeni uliofanyika Kidamali leo tarehe 15 Machi 2014.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Kidamali wakati wa kuhitimisha kampeni za ubunge jimbo la Kalenga ambapo aliwaambia wananchi wao CCM inatekeleza ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2010 hivyo kushinda uchaguzi huo kutaharakisha maendeleo ya Kalenga.
 Naibu Katibu Mkuu CCM(Bara) Ndugu Mwigulu Nchemba akihutubia wakazi wa kata ya Nzihi,kijiji cha Kidamali wakati wa kufunga kampeni za ubunge jimbo la Kalenga ambapo CCM imemsimamisha Godfrey Mgimwa.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Seif Shaaban Mohamed akihutubia wakazi wa kata ya Nzihi na kuwasihi kushikamana katika zoezi la kupia kura ili kuhakikisha ushindi unabaki CCM.
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM Sixtus Mapunda akihutubia wakazi wa kata ya Nzihi kijiji cha Kidamali na kuwaambia Umoja wa Vijana ipo kamili na itahakikisha ulinzi wa kutosha kwa kila mpiga kura.
 Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Shaibu Akwilombe akihutubia wakazi wa kata ya Nzihi kijiji cha Kidamali na kuwaambia CCM ipo imara na inatekeleza sera zake zenye misingi bora kwa maendeleo ya Kalenga na Tanzania kwa ujumla.
 Mbunge wa Ludewa ndugu Deo Filikunjombe akihutubia wakazi wa kata ya Nzihi wakati wakufunga kampeni za ubunge ulofanika kjiji cha Kidamali.
  Mbunge wa jimbo la Mwibala Ndugu Kange Lugola  akihutubia wakazi wa kata ya Nzihi wakati wakufunga kampeni za ubunge zilizohitimishwa leo kwenye kijiji cha Kidamali na kuwataka wananchi hao kumpa nafasi Godfrey Mgimwa kwa kumpigia kura za ndio siku ya tarehe 16 Machi 2014.
Mbunge wa Viti Maalumu Pindi Chana akiwasisitiza wakina mama kupiga kura kwa mgombea wa ubunge wa CCM Godfrey Mgimwa.
Katibu Mkuu wa CCm taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akipeana mkono na Chifu Abdul Sapi Mkwawa katika viwanja vya kata ya Nzihi
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akibadilishana mawazo na Naibu Katibu Mkuuwa CCM (Bara) pamoja na mgombea wa ubunge jimbo la Kalenga kupitia CCM Ndugu Godfrey Mgimwa wakati wa mkutano wa mwisho wa kufungia kampeni uliofanyika katika kata ya Nzihi kijiji cha Kidamali.
Msanii Dokii akiongoza wakazi wa kata ya Nzihi kucheza nyimbo za kampeni maalumu kwa ajili ya Godfrey Mgimwa.
Godfrey Mgimwa akishindwa kujizuia na kuamua kudua pamoja na msanii Dokii na wakazi wa kata ya Nzihi wakati wa kuhitimisha mkutano wa kampeni kupitia CCM
Mgombea Ubunge jimbo la Kalenga akiwa amebebwa juu na wananchi wa kata ya Nzihi wakati wa kuhitimisha kampeni za ubunge jimbo la Kalenga.

 Mgombea wa Ubunge jimbo la Kalenga CCM Ndugu Godfrey Mgimwa akimtambulisha mke wake Robby Salehe Mgimwa mbele ya umati wa wakazi wa kata ya Nzihi wakati wa kuhitimisha kampeni za ubunge zilizofanyika leo tarehe 15Machi 2014.
 Kamanda wa Vijana wa mkoa Iringa Salim Faraj Abri  alikuwepo kuhakikisha mkutano unaenda vizuri wakati wa kuhitimisha kampeni za ubunge jimbo la Kalenga katika kata ya Nzihi kijiji cha Kidamali.
Sehemu ya wakazi wa kata ya nzihi wakifuatilia kwa makini mkutano wa mwisho wa kampeni za ubunge CCM
Wananchi wakiwa wamembeba kwa furaha mgombea wa Ubunge jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, kwa tiketi ya CCM, Godfrey Mgimwa, wakati wa mkutano wa kufunga kampeni uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi, kwenye Uwanja wa Mnada, Kijiji cha Kidamali, Kata ya Nzihi, leo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Naibu Katibu Mkuu (Bara) Mwigulu Nchemba na Mgombea wa CCM jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa wakisalimia wananchi baada ya kuwasili kwenye mkutano huo.
Kinana na Mgimwa (kulia) wakisalimia wananchi baada ya kuwasili Uwanjani
Mwigulu akihutubia kwenye mkutano huo wa kufunga kampeni
Kinana akimnadi Mgimwa kwenye mkutano huo wa kufunga kampeni
Wananchi waliofurika kwenye mkutano huo wakinyoosha mikono kuahidi kumchagua Mgimwa  kesho
Mgimwa akihutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano huo wa kufunga kampeni
Mgimwa akiionyesha hadhara mkewe Robi, kwenye mkutano huo wa kufunga kampeni za CCM. Picha zote na Bashir Nkoromo wa CCM Blog 

 Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Mhe Rose Kamili, ambaye pia ni mke wa Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Wilbroad Slaa, akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kukamatwa kwa madai ya kukutwa akigawa rushwa kwa wapiga kura leo jioni katika Kijiji cha Kitawaya, Kata ya Luhota, wakati ikiwa ni siku ya mwisho kabla ya kufanyika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga kesho. Hadi tunakwenda mitamboni Rose alikuwa bado anashikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi mkoa wa Iringa.
 Rose akipandishwa kwenye karandinga la Polisi
Mhe Rose Kamili akipandishwa kwenye karandinga la Polisi

No comments: