Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer ambao ni wauzaji wa vinywaji vya Windhoek na Climax, Mama Benadetha Rugemalila akikabidhi baadhi ya misaada kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Bw Kariamel Wandi wakati Kampuni ya Mabibo Beer wakishirikiana na Wasanii wa Bongo movie walipotembelea Hospitali ya Mwanyamala ikiwa wanaadhimisha miaka mitatu ya Kuanzishwa kwa Klabu ya Bongo Movie.
Wasanii wa Bongo Movie wakiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi mkuu wa Mabibo beer na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala mara baada ya wasanii wa bongo movie na Kampuni ya Bia ya Mabibo kutembelea na kukabidhi misaada katika hospitali ya Mwananyamala mapema leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer, Mama Benadetha Rugemalila(kulia) akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi misaada katika Hospitali ya Mwananyamala leo, Katikati ni Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Bw Kariamel Wandi na Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Tanzania.
Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya Mwananyamala, Bw Kariamel Wandi (kulia) akitoa maelekezo kwa Wasanii wa bongo movie pamoja na Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer, Mama Benadetha Rugemalila (pili kulia) ambao ndio wauzaji na wasambazaji wa Vinywaji vya Windhoek na Climax wakati walipotembelea Hospitali ya Mwananyamala leo kwaajili ya kutoa Misaada mbalimbali kwa wagonjwa ikiwa ni maadhimisho ya miaka 3 ya Kuzaliwa kwa Klabu ya Bongo Movies huku Kampuni ya Mabibo Beer ikiwa wadhamini wakuu wa Bongo Movie.
Wasanii wa bongo movie wakielekea kwenye wodi za wagonjwa katika hospitali ya mwananyamala mapema leo kwaajili ya kutoa misaada kwa wagonjwa wakati bongo movie wakiadhimisha kilele cha Miaka 3 tokea kuanzishwa kwake.
Bi Sada Abasi (kushoto) akipokea misaada kutoka kwa mmoja wa wasanii wa bongo movie ambao walitembelea hospitali ya Mwanyamala leo ikiwa wanaadhimisha miaka 3 ya kuzaliwa kwa Klabu ya Bongo Movie.
Msanii wa Bongo Movie Sandra (kulia) akikabidhi misaada kwa mmoja wa wagonjwa waliopo kwenye Hospitali ya Mwananyamala wakati wasanii wa bongo movie kwa kushirikiana na Kampuni ya Mabibo Beer wakati walipotembelea hospitali ya Mwananyamala leo.
Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Bw Steve Nyerere (kushoto) akisisitiza jambo kwa Wasanii wa Bonngo movie wakati walipotembelea hospitali ya Mwananyamala leo ikiwa wanaadhimisha miaka 3 ya kuzaliwa kwa klabu ya Bongo Movie.
Jackline Wolper (katikati) akimsaidia Mmoja wa wagonjwa waliopo kwenye hospitali ya Mwananyamala wakati wasanii wa bongo movie walipotembelea hospitali ya Mwananyamala leo.
Mwenyekiti wa Bongo Movie, Bw Steve Nyerere akiongea na Waandishi wa habari wakati walipotembelea hospitali ya Mwananyamala leo na kukabidhi misaada ikiwa wanaadhimisha miaka 3 ya Kuzaliwa kwa Klabu ya Bongo Movie.
Shamsa Ford akiongea na Waandishi wa Habari.
............................................
Kampuni ya Mabibo Beer ambao ni wauzaji wa Vinywaji vya Windhoek na Climax kwa kushirikiana na Wasanii wa Bongo Movie leo wametembelea hospitali ya Mwananyamala ikiwa wanaadhimisha miaka 3 ya kuzaliwa kwa Klabu ya Bongo Movie ambapo Kampuni ya Mabibo Beer wakiwa wadhamini wakuu wa Bongo Movie kwenye kilele cha Kuadhimisha Miaka Mitatu ya kuzaliwa kwa klabu ya Bongo Movie.
Wasanii wa Bongo Movie wakiongozwa na Mwenyekiti wao Bw Steve Nyerere Wameweza Kutoa misaada kwa wagonjwa katika hospitali ya Mwananyamala ikiwa wanadhimisha Miaka mitatu ya Kuzaliwa Kwa Bongo Movie.
Misaada iliyotolewa leo na Wasanii wa Bongo Movie kwa kushirikiana na Kampuni ya Mabibo Beer ni Mabeseni ya Kuoshea watoto wadogo, pampers, sabuni na mafuta ya kujipaka.
Kampuni ya Mabibo Beer ndio wadhamini wakuu wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kudhaliwa kwa klabu ya Bongo Movie ambapo kilele chake kitafanyika katika Ukumbi wa Arcade East 24 uliopo Mikocheni ambapo kutafanyika bonge la Sherehe huku FM Academia, Banana Zoro Band, na Msanii Shilole watatoa Bonge la Burudani
No comments:
Post a Comment