Wednesday, March 26, 2014

MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA AWATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA ZINAZOTOLEWA NA UMOJA WA MATAIFA

P1130382
Afisa habari kitengo cha habari Umoja wa mataifa nchini Tanzania(UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza katika viwanja vya Mazingira Senta mjini Shinyanga kwenye warsha ya siku moja iliyokutanisha shule 10 za sekondari, vyuo na walimu kutoka katika shule na vyuo hivyo vilivyopo katika manispaa ya Shinyanga, ambapo alisema Umoja wa Mataifa(UN) unalipa suala la elimu kipaumbele sana kwa wanafunzi hivyo kuwataka wanafunzi kuwa na malengo katika maisha yao kwa kusoma kwa bidii,kuepuka vishawishi vinavyopelekea kupata ujauzito wakiwa wanafunzi tena chini ya umri wa miaka 18.

Afisa habari huyo pia aLItumia fursa hiyo kuwatahadharisha wanafunzi wa kike kuepuka ngono kwani kwa mujibu wa utafiti wao takwimu zinaonesha kuwa vijana wa kike wenye umri wa miaka 15-19 wana uhusiano wa kingono na wanaume wanaowazidi miaka juu zaidi ya umri wao hivyo kuwepo kwa hatari ya kuambukizwa VVU na Mimba za utotoni.Kushoto ni Mwenyekiti wa taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA) tawi la Shinyanga bwana Ezra Manjerenga.(Picha zote na Malunde1 blog ya Shinyanga)
100_5397
Wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari Busurwa, Uhuru, Mazinge, Buluba, Chamaguha, Kizumbi, wakimsikiliza Afisa habari kitengo cha habari Umoja wa mataifa nchini Tanzania (UNIC) Bi Usia Nkhoma Ledama (hayupo pichani) ambaye alisema kwa mujibu wa sensa yao mwaka 2012 asilimia 65 ya Watanzania wote vijana wenye umri wa miaka chini ya 24,lakini pia asilimia 40 ya vijana wa kike wenye miaka chini ya 18 wanapata mimba za utotoni na wengine kuolewa katika umri huo.Aliongeza kuwa asilimia 23 ya vijana umri wa miaka 15-19 wameanza kuzaa na katika umri huo kati ya vijana wanne basi mmoja anaolewa ama kupata mimba.
P1130388
Wanafunzi wa vyuo vya VETA, MUCCOBS, Shycom , waliohudhuria katika warsha hiyo ya Umoja wa Mataifa wakimskiliza Afisa habari kutoka UN, (hayupopichani) ambaye aliwataka kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na Umoja wa mataifa hapa nchini,lakini pia kuwaomba wazazi na walezi wa wanafunzi kujenga tabia ya kufuatilia mienendo ya watoto wao na kuwasaidia ili kuwafanya wapende elimu ili kufikia malengo ya Millenia.
100_5396
Afisa habari kitengo cha habari Umoja wa mataifa nchini Tanzania Bi. Usia Nkhoma Ledama (hayupo pichani) alisema takwimu zinaonesha kuwa asilimia 52 ya vijana wa kike umri wa miaka 18-14 wameanza kufanya ngono na na asilimia 7 kwa wenye miaka 15-19 wanafanya ngono na wanaume wanaowazidi umri miaka 10 zaidi ,huku vijana wa kiume wakidaiwa kuanza kufanya ngono wakiwa na umri wa miaka 20, akatumia fursa hiyo kuwataka vijana kuepuka ngono kwani wakindekeza ngono UKIMWI upo na hawataweza kutimiza ndoto zao hivyo. Alisema Umoja wa Mataifa haupo tayari kuendelea kuona vijana hawatimizi malengo yao.
P1130428
Mjumbe wa asasi ya vijana ya Umoja wa Mataifa Tanzania, Bw. Innocent akizungumzia kuhusu klabu za Umoja wa Mataifa katika shule za sekondari na vyuoni ambapo alisema miongoni mwa faida ukiwa mwanachama wa klabu hizo ni kupata taarifa nyingi tena kwa wakati kutoka UN kuwa karibu na umoja wa mataifa, kuhudhuria mikutano ya UN, kupata nafasi ya kusaidia jamii lakini pia kuwajengea uwezo wa aina mbalimbali kama vile kuongea mbele za watu,kuandaa ripoti,kupata vyeti n.k
P1130436
Walimu na wanafunzi waliohudhuria warsha hiyo wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika eneo la viwanja vya Mazingira Senta mjini Shinyanga ambapo maafisa kutoka Umoja wa Mataifa walieleza kazi za Umoja wa Mataifa na wakatumia muda fursa hiyo kuitaka jamii kubadilika na kuhamasisha jamii kufuata uzazi wa mpango ikiwa ni pamoja na kuwa tayari kupiga vita suala la vifo vya akina mama wajawazito na watoto,mimba za utotoni ambapo watoto wa kike milioni 7.5 miaka chini ya 18 wanazaa kila mwaka.
P1130444
Mratibu wa taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania kanda ya ziwa (UNA), Bw.Moses Mongo akizungumza katika warsha eneo la Mazingira Senta mjini Shinyanga ambapo alisema taasisi hiyo ilianzishwa mwaka 1964 kote duniani na ndiyo taasisi pekee hapa nchini yenye klabu nyingi yenye lengo la kuwaunganisha watu wa chini na Umoja wa Mataifa. Alisema hivi karibuni wamefungua tawi la taasisi hiyo mkoani Shinyanga na mwenyeki wake ni Bwana Ezra Manjerenga. Mosea Mongo alitumia fursa hiyo pia kuwataka wanafunzi na wanajamii kwa ujumla kubadilika na kwamba mabadiliko yanaanza kwa kutenda na wafanye kazi kwa malengo ili kuleta mabadiliko katika jamii.
P1130455
Bi Usia Nkhoma Ledama akieleza kazi mbalimbali zinazofanywa na Umoja wa Mataifa hususani malengo ya millenia kama vile kuhamasisha Afya ya Uzazi, Haki za Binadamu, kupambana na mabadiliko ya Tabia nchi, umaskini, kuhamasisha Amani na Chakula kwa wenye njaa. Kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Anna rose Nyamubi ambaye alikuwa mgeni rasmi.
P1130452
Mwenyekiti wa taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA) tawi la Shinyanga, Bw. Ezra Manjerenga akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Annarose Nyamubi katika warsha hiyo iliyokutanisha shule 10 za sekondari na vyuo vitatu vilivyopo katika manispaa ya Shinyanga. Katikati ni Mkutubi kutoka kitengo cha habari Umoja wa Mataifa nchini Tanzania(UNIC) Bi. Harriet Macha na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Bi. Anna rose Nyamubi.
P1130457
Mgeni rasmi katika warsha hiyo, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Bi. Anna rose Nyamubi, ambaye ni mdau wa maendeleo na mwanafamilia wa Umoja wa Mataifa (siku za nyuma aliwahi kufanya kazi na Umoja wa Mataifa katika shirika la UNICEF), alisema nchi ya Tanzania inatekeleza malengo ya millenia kupitia ilani ya CCM katika kuwaletea maendeleo wananchi wake hususani katika kupunguza umaskini.
Katika hatua nyingine Bi. Nyamubi aliwataka vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa na Umoja wa mataifa. Mkuu huyo wa wilaya aliongeza kuwa serikali inawajali vijana hivyo kuwataka kusoma kwa malengo kwani bila elimu dunia itawaacha na kuwataka kuacha kutegemea wazazi wao kwamba watarithi mali.
Aidha Nyamubi alitumia fursa hiyo kuwataka wazazi ambao hawajapeleka watoto wao kidato cha kwanza wawapeke haraka kabla ya kuwachukulia hatua.
P1130353
Mapema kabla ya warsha Afisa habari kitengo cha habari Umoja wa Mataifa nchini Tanzania(UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Chamaguha ambapo alisema lengo la ziara yao ni kuhamasisha uanzishwaji wa klabu za Umoja wa Mataifa na kutoa elimu kuhusu shughuli za Umoja wa Mataifa ambapo huwa wanatembelea shule za msingi, sekondari na vyuo mbalimbali kuwaelimisha kuhusu ajenda za Umoja wa Mataifa.
P1130376
Mratibu wa taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania kanda ya ziwa (UNA), Bw. Moses Mongo akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Chamaguha iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga, ambapo alisema shule hiyo ni miongoni mwa shule chache zilizopata bahati kutembelea na Umoja wa mataifa na kuwataja miongoni mwa watu ambao ni mazao ya klabu za Umoja wa Mataifa kuwa ni Zitto Kabwe na John Mnyika.Alisema klabu za Umoja wa Mataifa zinawajengea wanachama wake ujasiri pamoja na kuwafundisha mambo mbalimbali kama vile elimu ya ujasiriamali.
P1130361
Wanafunzi wa Shule ya sekondari Chamaguha wakinyoosha mikono kwamba wako tayari kuwa na klabu ya Umoja wa mataifa katika shule yao baada ya kuridhishwa na maelezo kutoka Umoja wa Mataifa hapa nchini wakiongozwa na Afisa habari kitengo cha habari Umoja wa mataifa Tanzania (UNIC)Bi. Usia Nkhoma Ledama.
P1130367
Awali katika shule ya sekondari Chamaguha katika manispaa ya Shinyanga ,ambako maafisa wa Umoja wa Mataifa walifanya ziara yao, Mkutubi kutoka kitengo cha habari Umoja wa Mataifa nchini Tanzania (UNIC) Bi. Harriet Macha akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo ambao wamedhamiria kuanzisha klabu ya Umoja wa Mataifa katika shule hiyo ambayo itaundwa na wanafunzi kuanzia 10 na kuendelea .

Hapo anaonesha vitabu na vipeperushi mbalimbali vinavyohusu Umoja wa Mataifa ambao ulianzishwa mwaka 1945 baada ya vita ya pili ya dunia.Hivi sasa Umoja wa Mataifa una nchi wanachama 193 duniani kote na nchi 3 pekee siyo nchi wanachama wa Umoja huo, nchi hizo ni Taiwan,Cossovo na Vatican.
100_5382
Ni katika ofisi ya walimu katika shule ya sekondari Chamaguha katika manispaa ya Shinyanga,muda mchache tu baada ya maafisa kutoka Umoja wa mataifa kuwasili katika shule hiyo kabla ya kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo. 
Aliyesimama ni kaimu mkuu wa shule hiyo bwana Malongo Maganga akiwakaribisha wageni hao ambapo aliupongeza Umoja wa Mataifa kwa kuwafikia na kufurahishwa na mpango wake kuhusu elimu ya uzazi wa mpango kwa wanafunzi kwani itawasaidia kuongeza uelewa na kujilinda zaidi ili kutimiza malengo yao.Alisema jamii inaamini kuwa elimu hiyo ni kwa ajili ya akina mama pekee. Aidha mwalimu Maganga alisema tayari shule yake imefungua faili kwa ajili ya klabu ya Umoja wa Mataifa kwa wanafunzi wa shule hiyo.(Picha zote na Malunde1 blog ya Shinyanga)

No comments: