Saturday, March 8, 2014

TAASISI YA TWA YASHEHEREKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI NA KITUO CHA CHAWAWAKI MJI MWEMA KIGAMBONI

Taasisi ya wanawake wenye mafanikio Tanzania (TWA) imesheherekea siku ya wanawake duniani na kikundi cha wanawake wenye watoto wenye ugonjwa wa mtindio wa ubongo na mgongo wazi wa Kigamboni (Chawawaki), yenye lengo la kusaidia wamama hao ili waweze kupata msaada kutoka serikalini na taasisi mbalimbali.

Wamama hao wanaomba msaada wa kujengewa jengo na vifaa vya mazoezi kwa ajili ya watoto wao. Kwa sasa wanatumia darasa kwenye shule la msingi Mjimwema, siku moja kwa wiki tu, ambayo haikidhi mahitaji yakuwahudumia watoto wao. Kikundi hicho kina jumla ya watoto 117 ambao wanaletwa kila ijumaa kwa ajili ya kufanyiwa mazoezi na CCBRT.

Akizungumza na waandishi wa habari, mwenyekiti wa kikundi hicho Bi. Reberata Jovin, ameiomba serikali, watu na taasisi binafsi, ziweze kusaidia kikundi cha wamama hao ili wapate msaada. Aliendelea kusema, "Kutokana na mazingira waliokuwa nayo kwa sasa kwenye shule hiyo, hayafai kuwahudumia watoto hao kwa sababu ya kuchangia vyoo na chumba kidogo cha kufanyia mazoezi". 

 Pia alisema elimu inahitajika kwa jamii kuhusu kuondoa dhana ya unyanyapaaji kwa watoto hao na wazazi. "Mfano tunapokua kwenye mabasi au kwenye mikusanyiko wa watu, watoto wetu wanaonekana kama misukule. Na wazazi wa kiume wana tabia ya kuwaachia mzigo wa kulea mtoto huyo kwa wamama peke yao".

Wito; naomba serikali iangalie jamii zenye watoto wenye matatizo kama haya, iwajengee vituo maalum ili waweze kupata huduma bila tatizo.

"Nashukuru Taasisi ya wanawake wenye mfanikio Tanzania (TWA) na CCBRT kwa kuwa nasi bega kwa bega kusaidia watoto wetu". Alimalizia Bi. Reberata Jovin.
Mrembo wa Tanzania Happiness Watimanywa akikabidhi baiskeli kwa mwenyekiti wa Chawawaki Bi. Reberata Jovin kwenye sherehe zenye lengo la kusaidia kikundi hicho, ambazo zimeandaliwa na taasisi ya TWA.
Mshauri nasaha na mtoa mafunzo wa CCBRT,Bi. Mgaya Mhamanda akiongea na kinamama wenye watoto wenye ugonjwa wa mtindio wa ubongo na mgongo wazi kituo cha kigamboni(Chawawaki) kwenye sherehe ya siku wanawake Duniani, ambayo iliandaliwa na taasisi ya wanawake wenye mafanikio Tanzania TWA.
Katibu wa kikundi cha Chawawaki,Bi. Upendo Ikombe katikati akiwa na Miss Tanzania Happiness Watimanywa (kushoto) na Bi. Grace Rubambeyi mshindi wa tuzo za Twaa, kwenye sherehe ya siku ya wanawake duniani zilizofanyika shule ya msingi Mji Mwema Kigamboni.
Kina mama wa kikundi cha Chawawaki Kigamboni wakimsikiliza rais wa Taasisi ya Wanawake wenye Mafanikio Tanzania TWA Bi. Irene Kiwia(hayupo pichani) kwenye sherehe ya siku ya wanawake duniani yenye lengo la kusaidia kikundi hicho.

No comments: