Sunday, March 9, 2014

MAPOKEZI YA MWILI WA MAREHEMU MEJA JENERALI BAKARI SHAABANI KATIKA UWANJA WA NDEGE WA ABEID AMANI KARUME,ZANZIBAR

Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Bakari Shaabani Hassan,wakati wa uhai wake.
Maafisa wa vikosi mbali mbali vya Ulinzi vya Zanzibar wakiusubiri mwili wa marehemu Meja Jenerali Mstaafu Bakari Shaabani Hassan ukitokea katika Hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam baada ya kufariki jana.
Baadhi ya wananchi na wanafamilia wa Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Bakari Shaabani Hassan wakiwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,kuupokea mwili wa Marehemu huyo aliyefariki katika Hospitali ya Jeshi Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafamilia wa Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Bakari Shaabani Hassan wakiteremka katika ndege ya Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ,baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,ikiwa na mwili wa Marehemu huyo.
Ndugu na Jamaa wa Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Bakari Shaabani Hassan,wakilia kwa uchungu baada ya kufika mwili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,tayari kwa mazishi yake yatakayofanyika leo kwa heshima zote za Kijeshi katika makaburi ya Tomondo Wilaya magharibi Unguja.
Ndugu na Jamaa wa Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Bakari Shaabani Hassan,wakilia kwa uchungu baada ya kufika mwili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,tayari kwa mazishi yake yatakayofanyika leo kwa heshima zote za Kijeshi katika makaburi ya Tomondo Wilaya magharibi Unguja.
Wanajeshi wa JWTZ hapa Zanzibar wakiuteremsha mwili wa marehemu Meja Jenerali Mstaafu Bakari Shaabani Hassan,kutoka katika Ndege ya jeshi hilo iliyotua leo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ukitokea katika Hospitali ya Jeshi Lugalo baada ya kufariki juzi.
Maafisa wa Jeshi la JWTZ wenye vyeo vya Meja wakiwa wamebeba Mwili wa marehemu Meja Jenerali Mstaafu Bakari Shaabani Hassan,ukitokea katika Hospitali ya jeshi Lugalo baada ya kufariki juzi marehemu amefariki akiwa na umri wa miaka zaidi ya Sitini.
Maafisa wa Jeshi la JWTZ wenye vyeo vya Meja wakiwa wameubeba Mwili wa marehemu Meja Jenerali Mstaafu Bakari Shaabani Hassan,ukitokea katika Hospitali ya jeshi Lugalo baada ya kufariki juzi marehemu amefariki akiwa na umri wa miaka zaidi ya Sitini.
Wananchi na jamaa wa Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Bakari Shaabani Hassan waliofika kuupokea Mwili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ukitokea katika Hospitali ya Jeshi Lugalo baada ya kufariki juzi tayari ukiwa umeingizwa katikagari la Kijeshi kupelekwa Nyumbani kwao Miembeni Mjini Unguja.



 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo nyumbani kwa aliyewahi kuwa mkuu wa kitengo cha maafa katika ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali Bakari Shaabani huko Ada Estate jijini Dar es Salaam kabla mwili haujasafirishwa kwenda Zanzibar kwa maziko. 
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa aliyewahi kuwa mkuu wa kitengo cha Maafa katika ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali Bakari Shaabani nyumbani kwake Ada Estate jijini Dar es Salaam
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho mbele ya jeneza la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha maafa meja Jenerali Bakari Shaabani nyumbani kwake Ada Estate jijini Dar es Salaam kabla mwili wa marehemu haujasafirishwa kwenda Zanzibar na kwa maziko

No comments: