Monday, March 10, 2014

Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink yawazawadia wazee wa Yombo Kilakala, Dar es salaam

 Mfanyakazi wa  Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink  Maria Chundu akiteta jambo na Bi.Khadija Sultan (78) wa kituo cha kulelea wazee cha Tushikamane Pamoja Foundation kilichopo Yombo Kilakala mara walipotembelea kituo hicho kutoa misaada mbalimbali kwa wazee wasiojiweza katika kituo hicho.Jumla ya vitu mbalimbali vilitolewa  ikiwemo mashuka ,blanketi , mchele na mafuta ya kupikia chakula vyote vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5.
 Mhasibu wa Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink, Joyna Mwafute akimlisha  chakula mmoja wa wazee waishio katika kituo cha Tushikamane Pamoja Foundation kilichopo Yombo Kilakala Bi.Tabu Juma( 65) wakati  wafanyakazi wa kampuni hiyo walipofika kituoni hapo kutoa misaada wa vyakula,mafuta ya kula,blanketi na mashuka vyote vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5.
 
 Meneja  Mafunzo na Uendelezaji wa Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink,Maxine Makenzie, akimpatia soda mmoja wa wazee wasiojiweza wanaotunzwa katika kituo cha Tushikamane Pamoja Foundation kilichopo Yombo kilakala jijini Dar es Salaam,wakati wafanyakazi wa Kampuni hiyo walipofika kituoni hapo kutoa msaada wa Vitu mbalimbali vikiwemo mashuka,blanketi na vyakula mbalimbali kwa wazee 45 waishio katika kituo hicho.

 Meneja  Mafunzo na Uendelezaji wa Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink,Maxine Makenzie,akihudumia chakula baadhi ya wazee wasiojiweza   wanaoishi katika kituo cha Tushikamane Pamoja kilichopo Yombo Kilakala jijinin Dar es Salaam,wakati wafanyakazi wa Kampuni ya hiyo walipokwenda kutoa msaada wa vitu mbalimbali kama vile Mashuka,blanketi na vyakula mbalimbali.
 
 Mhasibu wa Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink, Joyna Mwafute akisalimiana na  Bi,Julieth Mchanga (80)  wakati  wafanyakazi wa kampuni hiyo walipokwenda kutoa misaada mbalimbali kwa wazee wasiojiweza katika kituo hicho cha Tushikamane Pamoja Foundation kilichopo  Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam.Jumla ya vitu mbalimbali vilitolewa  vikiwemo mashuka ,blanketi , mchele na mafuta ya kupikia chakula vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5.
 
 Mfanyakazi wa  Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink, Zabida Kibiki akimvisha shuka baada ya kumkabidhi msaada huo John Shitundu ambaye ni miongoni mwa wazee waliopo chini ya kituo chaTushikamane Pamoja Foundation wakati  wafanyakazi wa kampuni hiyo walipokwenda kutoa misaada mbalimbali kwa wazee hao wanaoishi katika kituo hicho kilichopo Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam. Jumla ya vitu mbalimbali vilitolewa  ikiwemo mashuka ,blanketi , mchele na mafuta ya kupikia chakula vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5. Kushoto anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa kituo hicho Rose Mwapachu.
 Meneja Mikataba wa  Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink, Taddious Theodore akimkabidhi  msaada wa Shuka Julieth Mchanga  kwa niaba ya wazee wenzake 45,  wakati  wafanyakazi wa kampuni hiyo walitembelea kituoni hapo kutoa misaada mbalimbali kwa wazee wasiojiweza katika kituo cha Tushikamane Pamoja Foundation Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam, vitu mbalimbali vilitolewa  ikiwemo mashuka ,blanketi , mchele na mafuta ya kupikia  chakula vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink  wakiwa katika picha ya pamoja na wazee wasiojiweza wa kituo cha Tushikamane Pamoja Foundation ilichopo Yombo Kilakala wakati walipokwenda kuwapa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo mashuka, blanketi,vyote vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 2.5
 .Wafanyakazi wa  Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink   wakiwa na mizigo mbalimbali ya vyakula wakati  walipokwenda kutoa misaada mbalimbali kwa wazee wasiojiweza katika eneo la Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam,  wanaolelewa na Kituo cha  Tushikamane Pamoja Foundation kilichopo Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam. vitu mbalimbali vilitolewa  ikiwemo mashuka ,blanketi , mchere na mafuta ya chakula vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5.
Baadhi ya wazee wanaoishi na kutunzwa katika Kituo cha  Tushikamane Pamoja Foundation kilichopo Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam,wakicheza pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink  walipowatembelea wazee hao mahususi kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali kama vile mashuka ,blanketi , mchele na mafuta ya kupikia chakula vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5.

No comments: