.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe wakizungumza na washiriki wa hafla hiyo.
Benki ya Rasilimali nchini (TIB Development Bank) na Benki ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (Development Bank of Southern Africa, DBSA) zimeingia mkataba wa makubaliano ya kiuwekezaji katika sekta ya uchukuzi nchini jana jioni.
Makubaliano hayo yatasaidia kufufua miundombinu ya uchukuzi ikiwemo Reli ya Kati, Viwanja vya Ndege vya Arusha na Mwanza pamoja na Upanuzi wa Bandari.Zifuatazo ni picha mbalimbali za hafla hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam jana jioni.
Mkurugenzi wa Mipango Mikakati wa Benki ya Rasilimali nchini (TIB Development Bank), Jaffar Machano akifungua mkutano huo wa hafla ya utiaji saini mkataba wa makubaliano.
********
Benki ya Rasilimali nchini (TIB Development Bank) na Benki ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (Development Bank of Southern Africa, DBSA) zimeingia mkataba wa makubaliano ya kiuwekezaji katika sekta ya uchukuzi nchini jana jioni.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rasilimali nchini (TIB Development Bank), Peter Noni akizungumza na wadau wakati wa hafla hiyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (DBSA), Patrick Dlamini akizungumza na wadau katika hafla hiyo.
Sehemu ya washiriki kutoka Taasisi mbalimbali za Kiserikali,Bunge na Binafsi wakifuatilia matukio ya hafla hiyo.
Kutoka kushoto ni Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Ofisa Mtendaji Mkuu wa DBSA, Patrick Dlamini, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rasilimali nchini (TIB Development Bank), Peter Noni wakifuatilia kwa makini sehemu ya matukio wakati wa hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment