Na Mwandishi
Maalum
Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kupitia
Uwakilishi wake wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa, imeshiriki kikamilifu katika vikao vya
kawaida vya Bodi Tendaji ya
Mashirika na Mifuko inayosimamia
Maendeleo ya Umoja wa Mataifa.
Tanzania imeingia katika Ujumbe wa Bodi Tendaji ya UNDP ( united nations development
program), UNFPA ( united
nations population fund )na UNOPS( united nations for project services) kwa kipindi cha mwaka
2014- 2016.
Licha ya kuwa mjumbe, Tanzania pia ni Makamu Rais wa
Bodi nafasi inayoifanya Tanzania kuziwakilisha
za Afrika na kupitia umakamu huo wa Rais, Tanzania inakuwa
pia mjumbe wa Ofisi
ya mtedaji wa Bodi(Bureau) yenye jukumu la kuratibu na kusimamia shughuli za vikao vya Bodi.
Bodi Tendaji
ya UNDP, UNFPA na UNOPS yenye wajumbe 36
iliundwa kwa mujibu wa Azimio la
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa la
mwaka 1993.
Mgawanyo
wa wajumbe hao ni kama
ifuatavyo, wajumbe 8 hutoka mataifa ya Afrika, wajumbe 7 hutoka mataifa
ya Asia na Pacific, wajumbe 5 ni kutoka Amerika ya Kati na Visiwa vya Karibiani,
wajumbe 4 hutoka mataifa ya Ulaya Mashariki na
wajumbe 12 kutoka Mataifa ya
Ulaya Magharibi na Mataifa
mengine.
Kwa mujibu wa kanuni zinazosimamia utendaji kazi wa Bodi, wajumbe
wake huhudumu kwa mzunguko wa kupokeza .
Uwakilishi
wa Kudumu wa Tanzania ukiongozwa na Kaimu Muwakilishi , Bi. Maura Mwingira, na kwa kushirikiana na Maafisa wa Uwakilishi, umeshiriki
kikamilifu katika vikao hivyo kwa kuogoza baadhi ya majadiliano na kuchangia mijadala.
Ujumbe
wa Tanzania katika Vikao hivyo vilivyodimu kwa wiki moja, ulitumia ushiriki wake kusimamia
na kutetea maslahi ya
Tanzania. Na
katika nafasi yake ya Makamu Rais kutetea maslahi ya Afrika.
Miongoni mwa
masuala yaliyotiliwa mkazo na
Tanzania katika michango yake ni
pamoja na kusisitiza
fursa na nafasi ya nchi
zinazoendelea kuanisha, kuibua na kumiliki miradi ya maendeleo kwa kuzingatia
vipaumbele ambavyo nchi yenyewe
imejiwekea.
Tanzania
pia ilitambua mchango wa Mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa, katika usimamizi na utekelezaji wa mipango ya
maendeleo na miradi mbalimbai ikiwamo
ile inayosimamia na kutetea fursa
sawa za kijinsia hususani kwa wanawake
na watoto wa kike. Yakiwamo
pia masuala ya kilimo, lishe, elimu na
afya, vita dhidi ya umaskini na maendeleo shirikishi.
Ikizungumza
kwa kwa niaba ya nchi za Afrika, Tanzania pamoja na masuala mengine, imetoa
wito kwa washirika wa maendeleo kuongeza
michango yao katika Mfuko wa Maendeleo
wa Umoja wa Mataifa (UNCDF).
Mfuko huu wa Maendeleo ( United Nations Capital Development Fund) unatoa mchango mkubwa
katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa nchi
zinazoendelea na Tanzania ni mmoja wa wanufaika wa mfuko huo.
Tanzania imebainisha katika vikao hivyo kuwa licha ya kazi
nzuri iniayofanywa na UNCDF), bajeti ya
Mfuko huo imeendelea kupungua
ikilinganishwa na mahitaji yaliyopo. Ni kwa sababu hiyo imeomba wadau wa maendeleo hususani wale
wenye uwezo na nia kuangalia uwezekano
wa kutunisha Bajeti ya mfuko kutoka bajeti ya sasa ya dola za kimarekani 16
milioni angalau ifikie dola milioni 25.
Bodi Tendaji
ya Mashirika na Mifuko ya Maendeleo
ya Umoja wa Mataifa, (UNDP, UNFPA na UNOPS)
imekamilisha vikao vyake vya
kawaida kwa wajumbe wa Bodi kupitisha maazimio na
mapendekezo mbalimbali.
Vikao vya Bodi, ambavyo vilifunguliwa na Bi.
Helen Clark Mkuu wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa, ( UNDP)
ambaye aliainisha na kuelezea
mafanikio na changamoto za utekelezaji wa taasisi hizo kwa mwaka uliopita.
Katika ufunguzi wake, Mkuu
huyo wa UNDP pamoja na kuelezea shughuli za taasisi hizo
pia alielezea ushiriki wa UNDP katika utoaji wa misaada ya
kibinadamu katika nchi ambazo zimekubwa
na machafuko kama vile Sudan ya Kusini, Syria na Afrika ya Kati.
Aidha alitoa taarifa ya kuanza kwa
utekelezaji wa Mpango Mkakati
mpya wa UNDP utakaotekelezwa kwa
kipindi cha 2014-2017.
Kwa mujibu wa Bi.
Clark, mpango mkakati huo mpya unalenga pamoja na mambo
mengine, katika kuratibu na kuboresha utendaji kazi wa taasisi hiyo ,
pamoja na kuleta uwiano,
usimamizi na matumizi bora na yenye tija ya raslimali zake ikiwamo raslimali watu.
Pamoja
na Mtendaji Mkuu wa UNDP kuanisha shughuli zake, Wakuu wa
UNFPA, UNOPS , UN- Women na
UNICEF nao waliwasilisha taarifa
za Taasisi zao na kujadiliwa na wajumbe.
Wajumbe
wa Bodi walipata fursa pia ya kupitia
na kujadili nafasi na mchango wa Taasisi
hizo kuelekea ukingoni mwa utekelezaji
wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (
MDGs) na wajibu wa taasisi hizo katika
maandalizi ya malengo mapya ya maendeleo endelevu baada ya 2015 (SDGs)
Vile
vile wajumbe wa Bodi walipokea taarifa za utendaji na vipaumbele vya taasisi hizo,
ikiwa ni pamoja na bajeti zao na mapendekezo
yaliyotolewa na wakaguzi wa Bodi.
No comments:
Post a Comment